Ok sawa Kijana nimekueleea ila Naendelea Kukukumbusha na kukushauri Kuwa Speed si zaidi ya 80 Kwenye Maeneo yasiyo na watu Na speed 50 kwa maeneo mengi na Speed 30-50 Kwa maeneo ya Watu..
Usitembelee Speed 150 Kwenye Gari ukajiona Mjanja..
Ni Ulimbukeni na Nilimbukeni peke Yake Atayekwenda Speed 150 Na akajisifu..
Vijana Okoeni maisha Yenu na Kuambizana Ukweli bila kupepesa macho Speed Kubwa Inaua na Inasababisha Ajali..
Haijalishi utanitukana Ama utaniona Mchawi ila kwa speed Hiyo naomba Nikuambie Kuwa Tumechoka Kuona ajali barabarani ambazo zinasababishwa na Uzembe wa Dereva,..
Kuhusu Magari nimeanza kuendesha Magari huenda hata Miaka hiyo hujazaliwa Nimeanza kuendesha One 10 na Chaser Enzi hizo miaka ya 1990 Nikiwa Chuoni mwaka wa nne sijui Ulikuwa na Miaka Mingapi?
Tumechoka Kupokea Kesi za Ajali barabarani Mahospitali zinazosababishwa na Uzembe wa Mtu kwa makusudi kwa kuendesha spidi zaidi ya Inayotakiwa na kushindwa kucontrol gari..
Mimi kama Mzazi wako Nakuonya Kwa hiyo speed Unayoendesha ukichukia Chukia na ukitukana Tukana