Somo tulilolipata ni kubwa na linatosha, hatutaki lijirudie tena kuhusu mnayoyaita maandamano, kwani tumewapoteza watu wengi tu ambao wengine si kuwa waandamanaji bali kutokana na athari za hayo yanayoitwa maandamano. Kwa hiyo ndugu zanguni tukae chini na tufikiri kwa kina wapi tunaweza pata suluhisho la matatizo yetu angalau hata la muda mfupi tu mpaka pale tutakapo kaa sawa.Tarehe 9/12 nimeona kuna maandamano makubwa sana kuliko yaliyopita nime thibitisha hilo ufisadi hautakiwi kutunikiwa tuzo bali mapambano. Wazee, watoto, kwa vijana wataandamana wote.
Nunua vitu vya msingi weka ndani kuwa na umeme wa ziada, tumia huduma za internet za kimataifa badala ya zile za mitandao ya Tanzania ambazo zinaweza kuzimwa kwa vitisho na mafisadi.
Lazima tujue nazi haishindani na jiwe.

