PostGE2025 Gen Z hawapoi: Desemba 9, 2025 kuja na maandamano mapya

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Somo tulilolipata ni kubwa na linatosha, hatutaki lijirudie tena kuhusu mnayoyaita maandamano, kwani tumewapoteza watu wengi tu ambao wengine si kuwa waandamanaji bali kutokana na athari za hayo yanayoitwa maandamano. Kwa hiyo ndugu zanguni tukae chini na tufikiri kwa kina wapi tunaweza pata suluhisho la matatizo yetu angalau hata la muda mfupi tu mpaka pale tutakapo kaa sawa.
Lazima tujue nazi haishindani na jiwe.
 
Kama ni gari limekata break kwenye mteremko mkali... Alieko mbele ni hajui alipeleke wapi na kuruka huwezi maana spidi ni kali sana ... bila ujuzi utulivu hekima na busara za suka lazima lianguke. Tz yangu 😞
 
Usitupangie namna ya kufanya mkuu. Lolote litakalowezekana litakelezwa kikamilifu pasina kumuogopa mtu yeyote yule!
 
Huwezi kumtoa mtu ikulu kwa maandamano ya amani hiyo ni riadha isiyokuwa na tuzo mzee
 
Naam yawe ya amani japo CCM na serekali yake hawatataka, watapandikikiza wahuni wa kuleta vuruguiwe ili wapate sababu za kuua katika jina la kuyazuia.
Utayari wa kukabiliana na wahuni watakaopandikizwa na serekali ya CCM ufanyike, ifikirie namna ya kuwadhibiti mapema ili maandamano ya amani yasiyo na kikomo yafanyike.
Haiwezekani tuendelee kutekana na kuhukumiana nje ya mahakama, utekaji haukubaliki na utakomeshwa kwa gharama yoyote.
 
Kuanzia Leo hatutafanya maandano kwenye tarehe husika Bali tutafanya siku moja kabla ili itakapofika tarehe ramsi kusiwepo na MTU hata mmoja wa kutoka nje
Hata Ile tar 29 kama yangefanyika tar 28 hakuna MTU angepiga kura
 
Maoni yako yanatosha kumwambia mkeo si hapa jukwaani
 
Hii nchi haitakuwa sawa tena
Kama ni gari limekata break kwenye mteremko mkali... Alieko mbele ni hajui alipeleke wapi na kuruka huwezi maana spidi ni kali sana ... bila ujuzi utulivu hekima na busara za suka lazima lianguke. Tz yangu 😞g
 
Sijawahi kuwa mdhaifu kwenye kuongea ukweli.

Mm sio keyboard fighters ndo mana nilitoka kuandamana na sio kubaki online.

Anyway, watanganyika walinipa surprise, nami nikaungana nao.
 
Nyumbani kwa mtu mwenye kifua kipana, mzee wa hamieni Burundi nao kutembelewa siku hiyo
Ha haa🤣🤣
Code zingine nimekupata Ila huyo kifua kipana akili umeshindwa ku-decode. Nani huyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…