PostGE2025 Gen Z hawapoi: Desemba 9, 2025 kuja na maandamano mapya

PostGE2025 Gen Z hawapoi: Desemba 9, 2025 kuja na maandamano mapya

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Bado sijajua kiongozi wa hay maandamano ni nani Hadi sasa!

Lakini namwambia hiyo sio njia sahihi Kwa watz kudai haki zao!!

Tuzungumze na samiah aliahidi katiba mpya kwenye kampeni,tumdai aitishe bungee la katiba!
Tulishazungumza mara ngapi mkuu au hujawahi kumsikiliza Mange ,kiujumla serikali inayoongozwa na sa100 imeziba masikio na ukiongea tu uko ndani so hakuna solution nyingine
 
Gen Z hawapoi hawaboi, wanasema hii kesi haijaisha, wapo kwenye plan ya kuja na maandamano mapya siku ya uhuru 09/12.

Wanasema maandamano hayo yatapewa jina la Liberation Day.

Aione
IGP
Jumanne Muliro
I see
 
Naona neno la keyboard worriers limepotea ghafla humu mitandaoni. Maandamano ndio lugha inayoeleweka kirahisi. Sasa tutaandamana kwa amani kabisa. Atakayepora mali za watu tutamdhibiti wenyewe ili msipate kisingizio. Lakini madai ya katiba mpya lazima yafanyiwe kazi, na serekali ya mpito ni lazima. Hatuwezi kukubali kuongozwa na mtu aliyejitangaza kwa kura uongo.
Huna uwezo huo wewe!! Mmewadanganya vijana nyumbu wengine wamekufa na wengine sasa wanaozea magerezani nyinyi bado mpo kama ma-keyboard worriers tu. Key worrier bado wapo tu humu kama kawaida yenu wala hamkutoka kukinukisha sasa mnanuka wenyewe.
 
Unyama na matendo ya kikatili yaliyofanywa na Polisi hayazungumziwi kabisa. Cha ajabu, kila siku wapo bize kutoa matamko ya kusaka na kushughulikia watu.

Lakini, tukiwa wakweli, ninyi polisi dhalimu ni nani atawawajibisha kwa matendo yenu maovu? Mnajipa utukufu wa juu sana kuzidi hata malaika kwamba ninyi hamkosei, kila mnalofanya lipo sawa.

Mnasahau hata gadhabu ya wananchi ninyi ndiyo mmeichangia kwa kiasi kikubwa sababu mmekuwa wajivuni, dhalimu na waonevu kwa kipimo kisicho mithilika.

Mkishamaliza kuwasaka watu wa CHADEMA na Gen Z waliopambani nchi yao, hakikisheni mnatuambia ninyi mlio dhalimu, ni nani atawashughulikia kwa matendo yenu ya ovyo yasiyo na utu mliyofanya kwa watanzania?

Mfano halisi ni video hii ya tukio la Kituo cha Polisi Kisesa. Na kama sisi hatutawaadhibu, Mungu wa mbinguni atawapa mapigo ambayo vizazi vyenu vitauona utukufu wake.

View attachment 3498880
Hii mimba inayotungwa hapa! Ikikomaa na kuzaa.. Mungu tusaidie
 
Wanakuwaga wana power wakiwa wengi, akiwa mwenyewe hata ww unamtandika vizuri
Yani hapo roho inauma kweli.

Yani wapo wanne sijui wanawapiga watu waliowafunga wa kuwaamuru walale chini.

Sasa tofauti yao na mkoloni ni nini?
 
Back
Top Bottom