Kwanini uiambii serikali isikilize raia. Lakini wewe umekaa upande wa mtesaji ukiwalazimisha wateswaji waache kuandamana nikuambie tu tanzania inaenda kubadili rangi ya bendera soon
Sijakaa huo upande unaosema bali sipendi kuwa mnafki
Mimi sio zezeta nina akili timamu
Tumeona kwa ndugu zetu wakenya na slogan yao "RUTO MUST GO" kiko wapi?
Huwezi kushindana na watu ambao wana zana zote za kukushinda wewe na hawathamini tena maisha yako
Mtu umeshika mawe mikononi mwenzako ana SMG mbona haiingii akilini
Wazee wetu wenyewe katika vita vya majimaji walihoji kwamba sisi tuna mishale na mikuki wenzetu wana bunduki itakuwaje? Ndo kinjeketile Ngwale akaja na mbinu yake ile kama aliyokuja nayo Mange ya kwamba jeshi lipo pamoja na ninyi wananchi
Tumeishi kama wanyama kwa kipindi kile kifupi mnataka turudi kulekule? Mnataka maiti ziendelee kutapakaa barabarani na mitaani?
Imeripotiwa kuna viongozi wa chama fulani wanaomba hifadhi Kenya, hawa wamesoma alama za nyakati wanaona wanachuzwa tu na kina Sarungi,hilda,sativa na Mange, wenzao wanaenjoy wanaacha Gen Z wajifie uko
Wanaishia kusema dunia nzima imeona video zote sasa wakiona ndiyo nini? Ndo ndugu zetu watarudi? mpaka sasa hatua zipi zimechukuliwa?
Nawaheshimu wanaharakati ila sio wanaharakati hao uchwara Boniface Mwangi kipindi cha maandamano ya Kenya yote alikuwepo Kenya na aliungana nao
Hawa wetu sisi wanatumia ignorance ya watanzania kutimiza matakwa yao binafsi