Gerson Msigwa: Rais ameagiza kufunguliwa kwa Online TV tu na sio Vyombo vingine vya Habari

Abbas na Msigwa bado wa elements za mwamba yule sasa wasije wakalaumu baadaye.
 
Reactions: PNC
Mbona Hii ilikuwa clear toka mwanzo?! Mainstream media ndizo zilizoingiza ushabiki katika kutangaza lakini Rais alikuwa clear
 
Hawana akili.
Bando wamliongeza then wanafungulia online tv .
Huu si wehu?
 
Ukuweka chuki pembeni, je unaushahidi wenye kushikika au kuonekana kwamba walifanya hivo ulivyosema.??
Mahakama zote hapa nchini, na mahakama ya afrika mashariki, zilithibitisha kwamba walilawiti watoto.
 
Spana ziendelee?
 
Magazeti lisening skills zero .Raisi alitamks kabisa TV za mitandaoni wao hilo la magazeti walilitoa wapi? nenda youtube hotuba nzima ya Raisi imo alitaja online Tv tu
Hao Abbas na Msigwa ni wapuuzi. Rais alitamka kuwa "Kuna vyombo vya habari vimefungiwa....sijui hivyo vi tv vya mkononi. Vifungulieni" Sasa wao wanaleta ujuaji ngoja waone.

Yani Rais alimaanisha vyombo vyote vya habari. Gerson na Abbas waelewe kuwa Jiwe lao halipo tena ooohooo!
 
Binafsi naona sisi kama taifa tunajadili vihoja vyepesi sana, hizo online tv a.k.a youtube channels l, vifurushi vya data, CV za waliopewa dhamana n.k ni hoja ndogo sana...

Kuna mambo ya muhimu kama katiba mpya, kuna wakati SSH aliweka bayana kabisa kuwa ishu ya katiba mpya tusahau, nilidhani hili sasa wananchi wangeweka mashinikizo ili mchakato wa katiba mpya urudishwe...
 
Kamfichia aibu subordinate wake, for sure soon atatoa tena tamko la kufungulia vyombo vya habari kifasaha zaidi ingawa tamko lake kwangu mimi niliona limelenga vyombo vyote na Online TVs zilikuwa mfano. Aliposema Vi TV na ile Vifunguliwe, wale wenye akili zile zetu wameenda kwenye hizo VI mbili na kusahau kuwa msingi ulikuwa VYOMBO VYA HABARI....Vifunguliwe.

Lakini ni vizuri tutoke kwenye matamko na kurekebisha sheria ili akija mwingine asije tena na matamko yake bali sheria zi govern.
 
Kama ni kweli huu utakuwa ujinga wa hali ya juu,na mambo yatakuwa ya hovyo tu kama enzi za Jiwe
 
Kama manyoka akina Abbas yapo basi hakuna jipya sasa nimewaelewa vizuri wale wanaosema ni suala la muda tu umagufuli utaendelea kama kawaida
 
Yani halafu wanajiita wasomi wameshindwa kuelewa kuwa pale alopoweka neno Vi tv vya mkononi ni ulikuwa mfano tu. Hawa watu wawili wana akili za hovyo na sijui Samia aliwapa hizo nafasi kwa kigezo gani. Watu dull hivyo unawapa majukumu muhimu kama hayo?

Yani walishaona wapi hotuba ya kiongozi wa nchi inakuwa nusu nusu?
 
Mama naye naona ameanza kuwa mwanasiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…