Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Kwani hospitali tunazoongelea hapa ni za binafsi? labda kama umekurupukia mada....
 
Muulize the same doc. Muhimbili ni shilingi ngapi?

CT ya 700,000/= huko unaipata kwa 250,00/= MNH????

Kwa hiyo kigezo cha bei ni % fulani tu ya huko private?
 
Kwa hiyo kigezo cha bei ni % fulani tu ya huko privat

Kwa hiyo kigezo cha bei ni % fulani tu ya huko private?
Hii inayoonyesha kiasi gani haujaupanda mlima wenyewe na huku unapiga yowe.
 
Unaonaje badala ya kujihoji hivi kukafanyika independent audit Ili masuala mazima ya bei yakawekwa wazi?

Tungependelea bei iwe actual reflection ya gharama za consumables.

Au waona je mkuu?
Inaweza kufanyika, ingawa lazima itaanzia kwenye mapato na matumizi; na ili kuwepo na uelewa wa pamoja, ni muhimu kujua wao (hospitalini) wanagharamia nini kifedha (dawa, ukarabati, mafunzo, posho n.k)? Kama wamepewa sehemu kubwa ya kujigharamia, lazima gharama za matibabu zipande.
 
Hii inayoonyesha kiasi gani haujaupanda mlima wenyewe na huku unapiga yowe.
Kwanini ni vigumu kujibu waziwazi?

Bei hospitali za umma ni a % replica ya zile za private?
 
Madelu anakamua hadi tone la mwisho kiasi kwamba ndama anaambulia shombo tu pamoja na kwamba maziwa ni haki yake.....

Pamoja na tozo na kodi yuko kwenye hospitali za umma anajua mtakuja tu kwa bima au binafsi kama mnataka ndugu zenu waishi, na atahakikisha mmekuwa mafukara.

Anajua bila dialysis mtu atakufa dhahiri baada ya muda mfupi. Bei zimepangwa si kwa gharama halisi bali kwa sababu ni kifo au kuishi.

Kwa hakika hata kwenye ubeberu haiko hivi.
 
Kwanini ni vigumu kujibu waziwazi?

Bei hospitali za umma ni a % replica ya zile za private?
Hawa tayari wameshaelewa, sema wanaona aibu kukubali.........sisi tunachowashauri wakapitie upya hizo rate zao ili kuwaokoa hawa wananchi maskini. Wakianza kutusema sisi kwamba tulipe bei hizo kubwa, huenda sisi hatuwakilishi mamilioni ya watanzania walio wengi ambao wanaishi katika hali duni za vipato.​
 

Soma hiyo: DIALYSIS REQUIREMENTS

Nunua hizo ulete tufanye bure kwani machine ipo.
 
Hakika..
 

Unajua hospitali hizi investment cost ni 100% umma.

Hospitali hizi zinapata mgao kutoka kwenye kodi na raslimali za umma.

Biashara yoyote ya halali Bei ni kulingana na matumizi Kwa kitu, labda ya mihadarati.

Tunachoona hapa mahospitalini wamekaa wakapanga bei dhidi ya kifo.

Kwamba Kwa sababu usipolipa utakufa haihalalishi malipo kupangwa na bepari.

Bei ya bepari kwenye hilo itakuwa ni vyote mlivyo navyo!

Ndivyo ilivyo hapa. Hospitali za umma ziwe regulated ndipo lilipo suluhisho.
 
View attachment 2519275
Soma hiyo: DIALYSIS REQUIREMENTS

Nunua hizo ulete tufanye bure kwani machine ipo.

Ninafurahi kusikia ukweli kuwa mashine za zipo na wafanyakazi wa umma wapo na bajeti ya serikali ipo Kwa maana kuwa minus consumables gharama A dialysis zilipaswa kuwa bure.

Hapa sasa ndipo palitakiwa uwepo wa uzalendo kujua bei gani na kipi kinachopungua kwa mgonjwa mmoja mmoja Ili hiyo kuwa sehemu halali ya mchango wake. Ikawa zero kama haihitajiki au 5/- kama ndicho kinachopungua.

Hamuoni aibu kuibia wagonjwa au marehemu?
 
Uko sahihi, utatuzi wa hii changamoto lipo kwenye sera ya wizara/serikali.
Mfano; hospitali A kwa mwaka huu wa fedha inahitaji bilioni 5 ili iweze kutoa huduma kwa ufanisi/kwa bei nafuu; badala ya kupelekewa bilioni 5 wakapelekewa bilioni 1; hapo patatokea nini?
 
Kanunue minus consumables boss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…