Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Kwa kumbe ni mashindano ya posho na mhanga ni mgonjwa au marehemu?

Matokeo yake ndiyo Bei hIzi?

Kwa hakika tunakoelekea siyo kwenyewe.
uzalendo ni mgumu; ndio maana wengine hawakatwi kodi
 
Una miaka mingapi binti?
 
Juzi mwanangu ana bima NHIF lkn nikaambiwa nitoe 250000 kwa ajir ya ctscan aisee kidogo nizimie lkn shukran kwa wanandugu walisapot sana within a minute ilipatikana [emoji1545]
Kwanini bima haikulipa CTScan?
 
Bima ilikwisha muda nikampeleka Mzazi hapo Hospital ya Rufaa Mbeya aisee kuandiaka andika tuu na Dr bado hatujamuona zilitoka Bill utadhani tupo India...nikasema sawa sawa..hao jamaa wanachaji aisee...
 
Ndivyo wanavyoichaji mifuko ya bima na hapo bado wanavyo bambikiwa bima. Mifuko ya bima itaacha kufilisika?

Kumbuka ni hospitali za umma. Gharama za malipo hayo ni kwa vigezo gani?
 
Ndivyo wanavyoichaji mifuko ya bima na hapo bado wanavyo bambikiwa bima. Mifuko ya bima itaacha kufilisika?

Kumbuka ni hospitali za umma. Gharama za malipo hayo ni kwa vigezo gani?
Hata sielewi Mkuu hizi sio Hospital za Umma kama watu wanavyoaminishwa...
 
Hata sielewi Mkuu hizi sio Hospital za Umma kama watu wanavyoaminishwa...

Inataka kujitoa ufahamu kwanza kupata ujasiri wa kutetea uhalali wa bei hizi.

Hili si jambo la kuachia hewani.

Kupitia matibabu Pana wajanja wamejipanga kuwafukarisha watu na kujineemesha wao kupitia hospitali za umma.

Bima ni kama conduit kwenye kufanikisha hilo.

"Muhimu kwao ni pesa."

The end justifies the means.
 
Ukija kwenye bei ya hizo dawa utadhani nazo zina Kodi au kikokoteo kama cha magari huwa nashangaa tofauti kubwa ya bei...pana mwaka mmoja mjomba angu alikua na maradhi ya Moyo daah hapo Bongo ilikua kama mrija wa kujipatia pesa sijui kipimo mara Aga Khan mara dozi ya mwezi mmoja karibu laki nane nilipowasiliana na madaktari huko Cape Town Groot Skill hospital walisema mlete aje na passport yake muhuri uwe valid tuu atatibiwa bure kweli alivyofika nilidhani ni ishu ya muda mrefu alikaa hospital siku tatu walimpa dawa na gharama zote buree kabisa mpaka kesho karudi kwenye kazi zake ngumu wakati Tanzania walisema asifanye kazi ngumu na atakua anapewa dozi kila mwezi...Matibabu Tanzania ni ghari sana sana
 
Angalia huyu:

Kwenye hospitali kama hiyo uwezakano wa kupona ulikuwa mkubwa na bei isingefika huko.

Kuuvaa ujasiri wa kuwakomalia watu hawa si jitihada mfu.
 
Angalia huyu:

View attachment 2521351

Kwenye hospitali kama hiyo uwezakano wa kupona ulikuwa mkubwa na bei isingefika huko.

Kuuvaa ujasiri wa kuwakomalia watu hawa si jitihada mfu.
Nchi ina watu wenye laana hii unawezaje kuwadai wananchi wako kwa kukaa na mwili faida ya wao kuwa Watanzania ni nini wakati wao wabatibiwa Nje kwa kodi zetu...inakera sana kwa kweli..
 
Hospitali za umma investment cost 100% kutoka kwa umma. Mishahara ya wafanyakazi ni 100% kutoka kwa umma. Zinapata pia allocation ya operation costs kutokea kwa umma.

Kwa Nini bei hIzi?

Angalia hata ufanisi wao:

"Kwenye hospitali kubwa hizi kama Muhimbili siyo tiba kupona, bali ka transition to death huku wakiifilisi mifuko ya bima au familia inayolipa."

Ukiiona ankara, terminologies na jargons kibao na za kubambikiana humo humo.

Nani ataweza kuwa na ujasiri wa kufanya verifications hizo ndani ya changamoto za kuuguliwa au kufiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…