Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

Ayubu Alirudishiwa Kila Mali mara Mia.

Hudumieni huyo Mzee.
 
Kama unewahi kuuguza wala huwezi kushangaa maneno ya huyu jamaa, unajua kuna ile kumpeleka mtu hospitali, anapata vipimo, anaganyiwa procedure zote, analazwa a few days na kutoka.

Njoo scenario nyinhine, amelala tu, ni vipimo tu, majibu hayaeleweki, Doctor anatoa kipimo kimoja tu ndugu mnaambiwa hiki ni 1,200,000 mchange kama ndugu, keshokutwa kuna kipimo kingine, costs za hospitali zinaongezeka, baada ya mwezi mnapewa gharama mnashika kichwa, ukute sasa familia ndio hizi za kwetu...aaagr.

Tumtie moyo, tusimlaani hata kidogo. Anayeumwa na anayeuguza wote wanahitaji kutiwa moyo.
 
Unatumia IDs nyingi. ila nimeepuka tu mjadala wa kidini hapa maana kuna mambo sisi wenye hekma tunayaacha hatujazi watu ambao si sehemu yao hapo. hakuna kitu ambacho huwa najaribu kwanza kuepuka kama kuanza mchambulia mtu dini hasa ya uislamu. naifahamu sijakariri. naifahamu kwa ukaribu sana...sisi ni baadhi ya watu ambao marhamu sheikh yahya alikuwa anakuja mpaka nyumbani kukaa kuongea na mzee habari za dini ya kiislamu. nami nimesoma tena kwa kusoma Mombasa na Lamu... ila mwishowe nimebaki na akili zangu timamu.
 
Mtoa mada huyo ni baba yako au kuna taarifa uliwah kupata kuwa wewe sio mwanaye au hayo ni mawazo ya mkeo....Kumbuka na wewe ni mzazi na <b> hujui utaishia wapi</b>
 
Pole sana kwa kuuguza ila unapouguza usitazame kile utoacho kama unacho toa kama huna basi usimsimange mgonjwa bali muombe Mungu akusaidie pale unapokuwa na uzito akufanyie wepesi,Ila heshima ya wazazi wetu inatakiwa iwepo wangali wapo hai ama wametangulia mbele ya haki,
 
Ayubu Alirudishiwa Kila Mali mara Mia.

Hudumieni huyo Mzee.
Hizo ni habari za Ayubu, njoo kwenye uhalisia wa dunia ya leo utaniambia, tuwaombee wazee wetu wawe na maisha mazuri na mwisho wao uwe mzuri. Ikiwezekana kuwe na bima ya afya ya wazee ili kupunguza machungu ya kuuguza na kumaliza rasilimali zote za familia.

Kuna ndugu yangu wa kule Kijichi, mzee alilazwa Agha Khan just three weeks kwa shida ya figo, hapo kabla walishatoa mapesa kama yote, by the time anafariki deni lilikuwa 40m.
 
Biblia imeandika mwisho wa kuishi ni miaka 75 sasa huko kwingine anatafuta nini, mkuu kwani hakuna daktari umpe dili?
 

Wengine kwenye familia zao hawana Wazee hata WA miaka 80 hivyo hawawezi kuelewa unazungumzia Jambo gani.
 
Miaka ya nyuma kidogo early 2003 brother'angu alikuwa na frame ya biashara mitaa ya Kariakoo kwenye jengo la hawa waarabu wapemba wenyewe wanajiita Wayemen so mimi nilikuwa naenda kushinda pale kusaidia saidia kazi,huyu mzee alikuwa na mdogo wake alikuwa anasumbuliwa sana na nyonga na pressure.

Kuna siku huyu mdogo maradhi yake yalimng’ang‘ania akalazwa Muhimbili ndugu wakachoka wakamrudisha home wasubiri afe sasa ipo siku hali ilibadilika kwa macho ya kibinadamu wakaona huyu kesho hafiki,ilikuwa asubuhi huyu kaka mtu tukawa tumekaa nae nje kwenye bench tunakunywa kahawa akawa anawataarifu kwa simu ndugu zao walioko Zanzibar kwamba wajiandae muda wowote watakuwa na safari ya kuvuka bara kuja kuzika,siku zikaenda mara tukaanza kumuona Sharifu anatoka nje kuota jua,mara akarudi kuishi kwake na akawa anaendelea na kazi zake kama kawaida(alikuja kuugulia kwa kaka yake kwa sababu miezi saba iliyokuwa imepita nyuma alimzika mkewe).

Sasa siku moja asubuhi kufika pale eneo tukakuta turubai tukasema Sharifu atakuwa ameondoka,mara tunamuona Sharifu na ndugu zao wengine wanaratibu msiba kuuliza wanasema mzee Omar ambaye alikuwa mzima zaidi ya mzima amefariki ghafla na huyu Sharifu tulikuja kumzika miaka miwili mbele,binadamu hakuna mwenye haki ya kujadili uzima au kifo cha mwenzake as long as yeye mwenyewe hayuko guaranteed na kile kitamjia dk 30 zinazokuja mbele yake.
 
Sasa unataka tukushauri ummalizie afe au???
Mzazi naye angesema amechoka heka heka zako asikuhangaikie hadi umri wa kujipambania ungepata hata hyo laki 7 unayochangia??
Niliuguza mama yangu hadi kufikia kuacha kazi pale alipozidiwa lakini sikuwahi kufikia kuwaza haya na kuyaleta kwa watu hadharani. Nia yangu nilijua siku moja ataamka ila hakuamka hadi nilipomzika 😭.
Usichojua ni kwamba Mungu Ana riziki ya kila mtu na kama unapata cha kumhudumia basi ujue hiyo ni riziki yake Mungu ameipitishia kwako.
Kuna baraka nyingi sana katika kumhudumia mtu asiyejiweza awe mzazi au mtu baki. Ila baraka ni nyingi zaidi kwa mzazi. Ninashuhudia kwa macho yangu. Baada ya msiba nilijua nitataabika sana ila kila ninapoona giza mwanga unakuja. Na Kila ninachokifanya kinafanikiwa mnoo ...radhi ya mzazi ni kitu cha kukiombea sana na kukifanyia jitihada ukipate kabla mzazi hajaondoka duniani.
 
Kwa hiyo unatakaje sasa,
Tumwambie Baba ako ajitoe Roho, tukupe mbinu ya kummaliza Baba ako au unataka nini hasaaa hebu funguka ewe Chizi Maarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…