Uchaguzi 2020 Godbless Lema: Arusha leo kuna Mechi ya Simba bure na Tamasha la Wasanii bure ili kuhujumu Mkutano wa Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Godbless Lema: Arusha leo kuna Mechi ya Simba bure na Tamasha la Wasanii bure ili kuhujumu Mkutano wa Tundu Lissu

Sidhani kama CCM wanaamini uwepo wa Mungu,yaani CCM yenyewe ndio Mungu wao kwahiyo dunia inaweza ikazunguka lakini Tanzania ikasimama kwa uwezo wa Mungu wao, hawajawahi kufikiria kwamba lolote wakati wowote linaweza likatokea kwasababu wamejenga imani kubwa sana kwa huyo Mungu wao CCM.

Ni kweli kabisa. CCM ndiyo mungu na mchawi wao wanayemuabudu na kumsujudia. Hawaangalii wala kuzingatia tena kipi ni bora na sahihi kwa maslahi ya taifa.

Huyo mungu wao amewajaza roho za ujinga, kibri, ubinafsi, roho mbaya, ukatili, uongo, na mauchafu mengine mengi.

Tuendelee kujidanganya, ila Tanzania haitapata maendeleo ya kweli bila kukifutilia mbali hiki chama.
 
Wanachama na wapenzi wenu watawafuata popote mlipo, Ila wanamichezo na mashabiki wa SSC watakwenda uwanjani, mnyime watu starehe kisa shughuli zetu?
 
Simba kama inajiunga na genge la wahalifu Yanga kuwa upande wa wakandamizaji narudisha kadi, haina maana,
Kuanzia mdhamini mpaka msemaji mikia wote ni ccm, naona hata mashabiki pia wote mtakuwa ccm kama hamtaki anzisheni timu yenu
 
Dar Jana kulikuwa na Yanga day lakini Lissu alifanya kampeni kama kawaida.Kwenye kampeni hatuhitaji watazamaji tu kama miaka mingine tunataka anayeenda kwenye kampeni awe mpiga kura kweli hao wa matamasha waache waende

Hii ndiyo point muhimu. Hawatakiwi kutetereka kwa maneno ya kejeli ya idadi za watu. Najua nguvu kubwa inatumika kutaka kutuaminisha umma kuwa CHADEMA ni irrelevant.

Nguvu kubwa sana inatumika kwenye huu mpango! Ngoja tuone ni kwa jinsi gani mpango huo utafanikiwa.
 
Lema aanze kutafuta kazi nyingine ya Ubunge tayari ni Gambo.
Ila amevuna aisee, miaka kumi si mchezo, kwa umaskini ulionao najua unatamani upewe ubunge hata mwaka mmoja tu
 
Sidhani kama CCM wanaamini uwepo wa Mungu,yaani CCM yenyewe ndio Mungu wao kwahiyo dunia inaweza ikazunguka lakini Tanzania ikasimama kwa uwezo wa Mungu wao, hawajawahi kufikiria kwamba lolote wakati wowote linaweza likatokea kwasababu wamejenga imani kubwa sana kwa huyo Mungu wao CCM.
Acha kufuru ya kipumbavu namna hiyo.
Sir God yupo kila mahala huwezi mlinganisha na kitu chochote. Usifikiri kuwa upinzani ndo kwenda mbinguni . Hebu fikirini vizuri jamani laana Zingine tunajitakia wenyewe. Kumlinganisha Mungu na chama kweli? Big noooooooooo.
 
Popote pale Magufuli atakanyaga mambo yatadhibitiwa.

Huu upumbavu wakutumia fedha za walipakodi behind the seen kulipia hizi Fujo ili kuwahujumu Chadema ni matumizi mabaya kabisa ya pesa zetu.
Mkuu wanajiamini mbona mwalalamika tena
 
Ila amevuna aisee, miaka kumi si mchezo, kwa umaskini ulionao najua unatamani upewe ubunge hata mwaka mmoja tu
Mimi kazi ninayofanya inanitosha sana mkuu. Pesa ya mboga si haba!
 
Hii nature anaiita weka uugoko niweke jiwe weka kigingi niweke chuma.
 
Tume wawe na heshima kuruhusu vishughuli na hivi. Kwanza kama mshabiki tunaweza kuhama hiyo timu
 
Mkuu, hili la bure si kweli, jana nlkuwa kwenye game, na usiku gari la matangazo lilikuwa linataja kiingilio. Sababu zingine ni za kitoto kabisa. Kwa hiyo ile siku ya jana ya mwananchi mbona hamkulalamika?

Kama unajiamini, kuna haja gani kuanza kulalama mitandaoni? Your poor campaign strategy, usiwe mzigo Kwa wananchi. Ama kweli kama nilivyosema Chadema haina mathink tanks kwa sasa.
Mkuu, usijifikirie wewe tuu. Unapolazimisha mgongano usiyo wa lazima ni kwa faida ya nani
 
Back
Top Bottom