Godbless Lema, hospitali zote hizi nchini lakini unaenda Kenya ukaangaliwe bega, una hofu gani?

Mwalimu Nyerere alienda kutibiwa Uingereza, Jakaya alitibiwa Marekani, Magufuli mzena
Madaktari wetu wa hospital kuu ya taifa ndio wanaotoa rufaa za kwenda kutibiwa nje ya nchi. Kumbuka kuwa watu na passports zao ni mali ya taifa sawa na wanyama na madini. Taifa linayo haki ya kukuzuia, kukunyonga, kukutibu na hata kukunyang'anya passport yake na hata uhai kama ikibidi. Nadhani elimu yetu Ina kasoro ndio maana watu wanahoji sana.
 
Imeripotiwa kuwa ndugu Lema alizuiwa mpakani Namanga akidai kuwa alikuwa akienda kwa akina Martha Karua kuangaliwa afya ya bega lake na shida nyingine ambayo hakuitaja. Ukweli hii ilinifikirisha sana kama mtanzania kama kweli tumefika hapo.

Ni kweli Tanzania hakuna hospital na wataalam ambao wanaweza kumsadia mtanzania mwenzao kujua na kurekebisha afya yake hadi aende Kenya?.

Maswali:
1. Kuacha kutibiwa nchini ni ukosefu wa utaalamu au ni hofu tu ya kuhujumiwa na madaktari wa hapa?
2. Je, anakwenda kwa matibabu kweli au kwa mengineyo?
Viongozi wenu kama wanaoenda India kutibiwa na wao wanahofu gani?imefikia mahali mtu anaadika kitu mpaka unajiuliza huyu zimo kichwani kweli,utashangaa na wewe ni kiongozi mkubwa tu kwenye Nchi hii.
 
Kwani Tanzania kwasasa hakuna uhuru wa kusafiri nje ya nchi, sasa itafika wamikoani tutapigwa marufuku kuja dar
Hebu wewe safiri Leo kwenda Kenya tuone kama utazuiwa pia. Kama na wewe utazuiwa kusafiri ndio uje na hoja hako hiyo. Toa hicho kinachotoa harufu kwenye mfuko wako wa koti ili kupunguza inzi wanaokufuata.
 
Mbona nyie hospitali zimejaa lakini hamtibiwi nchini?
 
Sasa hivi MUHIMBILI wanapandikiza figo..pale mpaka wahindi au wazungu wapo kwenye foleni ya matibabu..
Hao viongozi wanaokwenda kuuguzwa India na wengi siku za karibuni wamefia huko, hizo huduma zilizoko Muhimbili hawakuwahi kuzisikia? 😲
 
Kurud canada si lazima aende huko, hapa hapa bongo, mara nyingi anaondokea hapa
Ingekuwa rahisi angeondokea hapa, we huoni kasema anaenda kenya na kapigwa pini asiende tayari wanajua mbinu zake za kutoroka nchi, nae alivyohatumii akili anatumia mbinu ile aliyotumia zama za mawe kutoroka nchi anadhani watu ni wajinga 😆.. Halafu kwanini anapenda kutoroka nchi abaki hapa hapa na aendelee kuimba wimbo wao anataka akaimbie huko mbali ili awaponze watu huku yeye akiwa salama
 
Imeripotiwa kuwa ndugu Lema alizuiwa mpakani Namanga akidai kuwa alikuwa akienda kwa akina Martha Karua kuangaliwa afya ya bega lake na shida nyingine ambayo hakuitaja. Ukweli hii ilinifikirisha sana kama mtanzania kama kweli tumefika hapSuo.

Ni kweli Tanzania hakuna hospital na wataalam ambao wanaweza kumsadia mtanzania mwenzao kujua na kurekebisha afya yake hadi aende Kenya?.

Maswali:
1. Kuacha kutibiwa nchini ni ukosefu wa utaalamu au ni hofu tu ya kuhujumiwa na madaktari wa hapa?
2. Je, anakwenda kwa matibabu kweli au kwa mengineyo?
Hivi matibabu ni dawa au inatakiwa uridhike unapokea je matibabu.

Suala la matibabu bama hata akiamua kutibiwa mbinguni ni haki yake.

Sasa kama alikuwa anakwenda hospitali mkamzuia akidondoka akizidiwa mikononi mwenu hiyo kesi na mungu mtaimaliza kweli? Afya ni ya kwake nyinyi mnampangia pa kutibiwa kweli. So haki kabisa.
 
Kipengele gani katika katiba kinasema mtu huruhusiwi kwenda kutibiwa nje kwa sababu hata Tanganyika kuna hospitali?

Mbona huwa hamuhoji kina Ndugai "mgonjwa ghali" kuwahi kutokea katika ardhi ya Tanganyika alipokwenda India kwa matibabu na kuleta bill ya mabilioni wakati angeweza kutibiwa hapo hapo Muhimbili?

Pia hujui katika taaluma ya afya kuna haki za mgonjwa 5 na mojawapo ya haki ni kuchagua aina ya matibabu ikiwemo nani anayetaka ampe matibabu?

Hujui hata Magufuli alipozidiwa alipelekwa Nairobi ndio akarudishwa Mzena kwanini hawakumpeleka Muhimbili?

Na ndio maana naona sasa mtawehuka mnasema mmefungia mtandao wa X sababu ya maudhui yasiyofaa halafu bado taasisi hizo hizo za serikali zinapost taarifa hizi huko huko X.

Mwisho , Lema hakukuomba wewe hata senti 5 ya kwenda Nairobi bali ni taasisi za serikali zimeanza kutumika kisiasa na mnapobanwa mnaleta diversionary tactics.
Kwani alikuwa nakwenda kutibiwa hospitali gani na dk nani lini? kumbuka Lema ni senior citizen, amepata kuwa mabunge wa taifa letu, anazo siri nyingi kuhusu nchi. Hawezi kupuyanga tu anavyotaka.
 
Imeripotiwa kuwa ndugu Lema alizuiwa mpakani Namanga akidai kuwa alikuwa akienda kwa akina Martha Karua kuangaliwa afya ya bega lake na shida nyingine ambayo hakuitaja. Ukweli hii ilinifikirisha sana kama mtanzania kama kweli tumefika hapo.

Ni kweli Tanzania hakuna hospital na wataalam ambao wanaweza kumsadia mtanzania mwenzao kujua na kurekebisha afya yake hadi aende Kenya?.

Maswali:
1. Kuacha kutibiwa nchini ni ukosefu wa utaalamu au ni hofu tu ya kuhujumiwa na madaktari wa hapa?
2. Je, anakwenda kwa matibabu kweli au kwa mengineyo?
Umewahi kufika na kuishi KENYA? Nimesoma medicine KENYA nimeishi KENYA kwa miaka 9 .

Ukweli matibabu yao ni standard sana na wana madkatri compitent sana kuliko Tanzania
 
Matibabu ya aina hiyo lazima yaidhinishwe na serikali kupitia hospital ya taifa.
 
Ingekuwa rahisi angeondokea hapa, we huoni kasema anaenda kenya na kapigwa pini asiende tayari wanajua mbinu zake za kutoroka nchi, nae alivyohatumii akili anatumia mbinu ile aliyotumia zama za mawe kutoroka nchi anadhani watu ni wajinga 😆.. Halafu kwanini anapenda kutoroka nchi abaki hapa hapa na aendelee kuimba wimbo wao anataka akaimbie huko mbali ili awaponze watu huku yeye akiwa salama
Mtu akitoroka nchi huwa anapitia migration?

Unajua kutoroka kukoje kisheria?

Embu kasome kwanza halaf urudi hapa
 
Mtu anatumia hela yake bado unahoji wakati hao wengine wanatumia kodi zako wanapeleka hadi wajomba zao kucheki mafua SA upo kimya Tanzania wacha wale watoto wa Kenya watudharau tu aisee..
 
Imeripotiwa kuwa ndugu Lema alizuiwa mpakani Namanga akidai kuwa alikuwa akienda kwa akina Martha Karua kuangaliwa afya ya bega lake na shida nyingine ambayo hakuitaja. Ukweli hii ilinifikirisha sana kama mtanzania kama kweli tumefika hapo.

Ni kweli Tanzania hakuna hospital na wataalam ambao wanaweza kumsadia mtanzania mwenzao kujua na kurekebisha afya yake hadi aende Kenya?.

Maswali:
1. Kuacha kutibiwa nchini ni ukosefu wa utaalamu au ni hofu tu ya kuhujumiwa na madaktari wa hapa?
2. Je, anakwenda kwa matibabu kweli au kwa mengineyo?
Mbona viongozi wenu wanatibiwa nje a sio Tanzania
 
Unamuamulia akatibiwe wapi? Mbna viongozi huenda India Kwa matatizi ambayo hata hapahapa nasovika?
 
Matibabu ya aina hiyo lazima yaidhinishwe na serikali kupitia hospital ya taifa
 
Mtu akitoroka nchi huwa anapitia migration?

Unajua kutoroka kukoje kisheria?

Embu kasome kwanza halaf urudi hapa
Kwani kipindi kile aliendaje kenya kisha akaenda Canada, si alipita boda la namanga au?
 
Kwani Tanzania kwasasa hakuna uhuru wa kusafiri nje ya nchi, sasa itafika wamikoani tutapigwa marufuku kuja dar
Inashangaza sana maafisa wetu wa uhamiaji wanavyofanya kazi zisizowahusu; kwenye kugonga mhuri wa kutoka utakutana na afisa wetu anakuhoji unaenda wapi na kufanya nini wakati ni kazi ya afisa upande wa nchi unayoingia.... Siwezi kushangaa mkasa uliompata Godbless Lema pale Namanga.... Mwaka 1995 niliwahi kusumbuliwa sana pale bila hata sababu za msingi.
 
Kwani kipindi kile aliendaje kenya kisha akaenda Canada, si alipita boda la namanga au?
Kwann alivyorud hqkufunguliwa kesi ya kuvuka mipaka bila kufuata utaratibu?

Kasome sheria ya uhamiaji namba 7 ya 1995.
Wamelezea vizuri

Jijengee tabia ya kujisomea
 
Back
Top Bottom