Kwa kweli nakubaliana na Lema:
Mtu kama Chalamila, hana sifa hata ya kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa. Aliipata nafasi hiyo kwa vile marehemu alionekana kuwapenda zaidi vichaa kuliko wazima. Yeye mwenyewe aliwahi kutamka, 'nimekuteua wewe Mpina kwa sababu wewe ni kichaa kama mimi'.
Mtu kama Kabudi, nimewahi kunena mara kadhaa, hana faida kwa Taifa. Alichangia sana kumpotosha Magufuli, na ameshiriki kwa kiasi kikubwa kuua uwekezaji nchini, japo wajinga wanadanganywa eti ni mzalendo sana.
Kabudi ni mbishi na arrogant, lakini hakuna anachokijua kwenye diplomasia wala uchumi. Masomo yaliyompa uprofessor ni Familiy Law yaani mirathi na ndoa. Hili ni eneo ambalo kwa wale wanasheria, huwa wanasoma wenye uwezo mdogo, ni sawa na kule shule ya msingi zamani kulikuwa na somo la sayansikimu, mnafundishwa kupika na kupiga pasi nguo.
Mama Samia akitaka aibadilishe nchi hii kuipeleka kwenye maendeleo ya kweli awaondoa viongozi wote ambao ni vichaa, wajinga na wanafiki na wale walioteuliwa kwa misingi ya ukabila, undugu na ukanda, na siyo uwezo wao, kama vile:
Kabudi
Chalamila
Mwigulu
Jafo
Sabaya
Kalemani
Doto wa Fedha
Biswalo Mganga
Elias Kwandikwa
Hapi
Kitila Mkumbo
Waziri wa uwekezaji, anahitajika mtu mwenye uwezo mkubwa, exposure ya masuala ya uchumi na uwekezaji, maana uwekezaji ni maeneo ambayo uongozi wa marehemu, uliua kabisa. Ni katika kipindi chake, tuliwapoteza wawekezaji wakubwa wa kimataifa kwenye sekta ya gas na madini, mpaka kuifanya Tanzania kwa sasa kufikia kuwa ndiyo nchi inayoongoza duniani kuwa na mazingira mabaya ya uwekezaji kwenyenmaeneo hayo. Hakuna mwekezaji wa kimataifa anayetaka kuja Tanzania. Wamejitahidi kuwabembeleza wawekezaji wa gas warudi, lakini hakuna mafanikio ya wazi.
Tunahitaji waziri wa sheria na katiba mwenye akili timamu, siyo mropokaji na mnafiki kama huyu wa sasa. Sheria za nchinzina uwezi wa kuua uchumi na uwekezaji.