Godbless Lema: Mtoto wangu hawezi kuendesha bodaboda, ni laana

Godbless Lema: Mtoto wangu hawezi kuendesha bodaboda, ni laana

Ni muda sasa CCM iingilie kati kwa kuwapa semina hawa wanufaika wa michango ya tonetone huko CHADEMA ili waweze kujenga hoja wanapokuwa jukwaani. Ukisikiliza maneno ya Lema utagundua yeye ndo laana hapa nchini. Kaongea maneno ya kijinga sana kwa hadhi yake.

Hii CHADEMA ya sasa inapaswa kupelekwa darasani kwenye chuo cha CCM Kibaha ili kujifunza namna sahihi ya kufanya siasa na sio huu ujinga wanaoufanya kwa sasa.

View: https://www.instagram.com/reel/DeuEdn9IR1q/?vrfl=N2lhaHoyNHRkb3Q0

Waende chuo cha siasa cha ccm wakati ccm wenyewe wanategemea kuteka, chaguzi za wizi na upuuzi wa aina hiyo? Sasa kama Polepole hayupo, na Nchimbi kavuliwa uanachama kwa kusema katiba mpya, kuna chuo hapo kweli? Subiri ukikuta mtoto wa Lema anaendesha bodaboda ndio uje uwaambie watu kuwa Lema ni muongo.
 
Ule ni mkutano wa chama kama anachosema sio msimamo wao wanawajibu kukanusha, Lema anajua anachofanya. Support ya Chadema ni hao vijana wa bodaboda na wananchi wa kipato cha chini ambao hawana uwezo wa kusomesha hizo shule anazosema anachofanya ni kuwaambia kwamba hata sisi hatupo pamoja na nyinyi sisi sio wenzenu ni strategic kabisa kupunguza ushawishi wa makundi fulani
Lema anamaanisha wao wakipata madaraka watahakikisha vijana wanaingia kwenye shughuli za uzalishaji mali kama mashambani na viwandani, na si kuendesha bodaboda. Huoni kwa kuendesha bodaboda unaua nguvu kazi ya uzalishaji mali, na kuzalisha taifa la watoa huduma zaidi. Ili taifa liendelee kwa Kasi na gharama za maisha zishuke, uzalishaji Mali ni muhimu zaidi. Una lingine boss?
 
Root cause aliyokuwa akiongea Bw. Lema kwa namna ya mifano ndio hiyo hiyo unaiona kwa muweka uzi...

Ujumbe wa Lema ulikuwa katika maeneo haya.

1. Ukosefu wa Exposure
Watanzania wengi wanaamini wameendelea kwa sababu hawajui nchi zilizoendelea zinafananaje, akatoa mifano ya nchi kama Singapore, HongKong n.k kwamba wengi wa wapiga kura wakiweza hata kukanyaga tu kwenye nchi hizo na kuona maendeleo mathalani kama ya barabara halafu wakarudishwa kwenye nchi yao, lazima wataandamana kufika Ikulu kushinikiza maendeleo hata ikiwalazimu kufanya hivyo wakiwa uchi.

2. Matibabu duni
Utashi wa Daktari kwenye kushindwa kutambua shida ya kiafya (bega) iliyokuwa inamkabili Lema. Akataja namna ambavyo wagonjwa wengi hufariki si kwa sababu magonjwa yao hayatibiki bali uduni wa matibabu.

3. Umaskini
Hapa ndipo ambapo aliyemnukuu Lema kaamua kupoteza lengo zima la ujumbe wake.
Umaskini ndio chanzo kikubwa kinachopelekea watu waamue kurisk maisha yao kwa kuendesha bodaboda, hivyo huu utitiri wa waendesha bodaboda ni kielelezo cha ukubwa wa umaskini ulioizunguka jamii ya vijana.
Kwa mujibu wa Lema, umaskini ni matokeo ya laana (hii reference kaitoa kwenye mafundisho ya imani ya Ukristo)...

Sasa miCCM kama kawaida yao huwa ikiambiwa ukweli A, inageuza maneno ili aliyeongea ukweli aonekane kazungumza uongo B...
Angalia mfano Waziri Mkuu akiongea na Diaspora UK au USA, kwanza anaongea kwa heshima na anatoa hoja zilizonyooka akijua anaongea na watu wenye uelewa na exposure.

Huwezi kuwapiga blah blah za mfano wanazoongea wakiwa bongo. Bongo atasema boda boda ni ajira na inalipa. Akijua kabisa ni vile vijana hawana pa kwenda wameamua wakomae tu.
 
Ukweli mchungu sana kaongea.....
Namsapoti... Boda boda sio kazi
 
Ni muda sasa CCM iingilie kati kwa kuwapa semina hawa wanufaika wa michango ya tonetone huko CHADEMA ili waweze kujenga hoja wanapokuwa jukwaani. Ukisikiliza maneno ya Lema utagundua yeye ndo laana hapa nchini. Kaongea maneno ya kijinga sana kwa hadhi yake.

Hii CHADEMA ya sasa inapaswa kupelekwa darasani kwenye chuo cha CCM Kibaha ili kujifunza namna sahihi ya kufanya siasa na sio huu ujinga wanaoufanya kwa sasa.

View: https://www.instagram.com/reel/DeuEdn9IR1q/?vrfl=N2lhaHoyNHRkb3Q0

Ameongea ukweli mchungu! Kama amekosea, nakupa kazi ya kunionesha mtoto wa Mwigulu au Samia anaye endesha bodaboda! Halafu nitachukua sumu na kunywa hadharani ili kufa kifo cha kishujaa.
 
Ameongea ukweli mchungu! Kama amekosea, nakupa kazi ya kunioneshela mtoto wa Mwigulu au Samia anaye endesha bodaboda! Halafu nitachukua sumu na kunywa hadharani ili kufa kifo cha kishujaa.
Punguza wivu..
 
Punguza wivu..
Wadau kibao wamekutolea mifano hii kwa nia nzuri kabisa isiyofungamana na huo wivu unaotaka kuwaaminisha watu hapa.

Lema yuko sahihi. Iwapo wewe mwenyewe hauko tayari kumuona mtoto wako anafanya hiyo kazi ya bodaboda! Na badala yake unamtengenezea mazingira ya kuja kukirithi cheo chako! ni kwa nini unataka watoto wa wenzako wafanye?

Acheni kuwafanya watu hawana akili. Halafu muache ubinafsi. Au mnafikiri ni nyinyi pekee ndiyo mnaotakiwa kuishi maisha ya kifahari?
 
Kwahiyo hizi bodaboda hazifai kumilikiwa na watu au azifai kufanyiwa biashara maana sisi wengine tuna mipango ya kununua boda zetu binafsi kwaajili ya matembezi tu!
 
Huo ni msimomo wake kwahiyo hata wewe unavyowasujudia Ccm na huyo bibi yako huo pia ni msimamo wako na mimi pia, kuna kazi kama ya bodaboda siwezi kuifanya huo ni msimamo wangu
Sio bodaboda tu, Na Mimi pia mtoto wangu hawezi kufanya kazi ya Polisi, akijiunga kwenye kazi hiyo ajijue amejitenga na familia yangu.
 
Sema kiongozi gani wa CCM au yeyote yule mwenye kuanzia Mkuu wa idara katika Serikali mtoto wake ni bodaboda ...weewe ndio mpuuzi mnaotumia lugha ya "wananchi wanyonge maskini" jinga kabisa.... Nchi gani iliyoendelea Ina sekta Kubwa ya bodaboda kama matanzania!?! Bodaboda sio kazi Ile... Haya kafuate buku7 lumbumba
Nigeria imeendelea na ina bodaboda kibao, nchi za asia, india, china kuna bodaboda wengi sana, unalijua hilo?
 
Wadau kibao wamekutolea mifano hii kwa nia nzuri kabisa isiyofungamana na huo wivu unaotaka kuwaaminisha watu hapa.

Lema yuko sahihi. Iwapo wewe mwenyewe hauko tayari kumuona mtoto wako anafanya hiyo kazi ya bodaboda! Na badala yake unamtengenezea mazingira ya kuja kukirithi cheo chako! ni kwa nini unataka watoto wa wenzako wafanye?

Acheni kuwafanya watu hawana akili. Halafu muache ubinafsi. Au mnafikiri ni nyinyi pekee ndiyo mnaotakiwa kuishi maisha ya kifahari?
Wadau kibao ❎ wajinga kibao ✅
Mtu kusema nimwonyeshe mtoto wa waziri anayeendesha bodaboda ni upuuzi uliopitiliza. Huko China anapopataja Lema kuna bodaboda na baiskeli kibao zimeajiri watu. Mtoto wangu kutoendesha bodaboda haimaanishi iwe haramu kwa wengine.
 
Sio bodaboda tu, Na Mimi pia mtoto wangu hawezi kufanya kazi ya Polisi, akijiunga kwenye kazi hiyo ajijue amejitenga na familia yangu.
Familia ya kipumbavu kama yako ni sahihi mtoto kujitenga.
 
Sio bodaboda tu, Na Mimi pia mtoto wangu hawezi kufanya kazi ya Polisi, akijiunga kwenye kazi hiyo ajijue amejitenga na familia yangu.
Huyo huyo lema akishamaliza kuwatukana bodaboda, anawaomba michango ya tone tone, lakin lema alifukuzwa shule kolila sekondari kwa ajili ya bangi, itakuwa bado ziko kichwani
 
Ni muda sasa CCM iingilie kati kwa kuwapa semina hawa wanufaika wa michango ya tonetone huko CHADEMA ili waweze kujenga hoja wanapokuwa jukwaani. Ukisikiliza maneno ya Lema utagundua yeye ndo laana hapa nchini. Kaongea maneno ya kijinga sana kwa hadhi yake.

Hii CHADEMA ya sasa inapaswa kupelekwa darasani kwenye chuo cha CCM Kibaha ili kujifunza namna sahihi ya kufanya siasa na sio huu ujinga wanaoufanya kwa sasa.

View: https://www.instagram.com/reel/DeuEdn9IR1q/?vrfl=N2lhaHoyNHRkb3Q0

Lema yupo sahihi ✔️ issue ya bodaboda ile sio kaz kiukweli ni vile vijana hawana ajira. Pia hua inakera sana bodaboda kupewa jina la.. Maafisa usafirishaji ❌jina la hovyo kbs toka kwa wanasiasa ku brainwash vijana!!!
 
Back
Top Bottom