Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 22,981
- 47,826
Yupo sahihi..
Mkuu kila aina ya usafiri ina hatari zake. Cha muhimu ni sheria za usalama kufuatwa kikamilifu. Tukizungumzia bodaboda na baiskeli China wanazo nyingi mno ila hawana ajali za kipuuzi. Tatizo hapa kwetu jeshi la polisi likisema lihakikishe sheria zinafuatwa tunaanza tena kuwapinga na kudai wanaonea wanyonge. Tanzania hata mtembea kwa miguu huvunja sheria sana za barabarani. Mimi naona jeshi la polisi lichukue hatua zaidi.Hizi pikipiki zimerahisisha sana siyo tu usafirishaji wa abiria na mizigo bali hata taasis za umma kwa sasa pikipiki ndiyo usafiri no 1 anzia TANESCO na Mamlaka za maji za miji yote.
Ila ukweli ni usafiri hatarishi mno mno hasa kwa mijini,watu wanazungumzia vifo tu.
Majeraha ya uti wa mgongo ni mwiba kwa uchumi wa familia, yamewafanya vijana wadogo kabisa wawe tegemezi wa kila kitu ie kulishwa hadi kuchambishwa.
Hao wanaopoteza kumbukumbu huko MOI baada ya kuumia vichwani,wengine kumbukumbu huwa hazirudi 100% milele yaani anamsahau hadi mkewe na watoto.
Nina miaka 7 now sijagusa boda na sitokaa nitumie hasa town na highway.
Aisee 😂Huo ni msimomo wake kwahiyo hata wewe unavyowasujudia Ccm na huyo bibi yako huo pia ni msimamo wako na mimi pia, kuna kazi kama ya bodaboda siwezi kuifanya huo ni msimamo wangu
Hujambo Jeni?Kuna Uzi niliwahi kuandika kwanini naona bodaboda sio sahihi kwa kijana hasa kwakuzingatia ndio taifa la kesho
Kibaya ni kwamba hao watunga Sera hawana uelewa na startup,.na wala hawahangaiki na future ya kijana, Leo kuna mbunge anadhamini Vijana bajaji na pikipiki lakini nilimpelekea proposal kuwa anifanikishie ule mkopo WA 10% WA 500m then ntatoa Ajira rasmi ya kudumu Vijana 20Hujambo Jeni?
Tukiacha ubinafsi kuanzia raia mmoja mmoja hadi serikali tutatengeneza ajira nyingi na hakutakuwa na haja ya kuwa na bodaboda wengi. Kwa mfano badala ya mtu kununua gari la milioni zaidi ya 500 anaweza fungua mradi fulani ukatoa ajira. Pia wabunge nao kufanya marekebisho ya sheria na kufutilia mbali sheria zinazofanya watu waone shida kufungua viwanda na kuwekeza nchini. Vijana wakulima wangewezeshwa mitaji na kutoa ajira kwa wenzao.
Nigeria imeendelea na ina bodaboda kibao, nchi za asia, india, china kuna bodaboda wengi sana, unalijua hilo?
Huko Ulaya Ujerumani, Ufaransa wanaandamana kwa ukosefu wa ajira, hakuna nchi inayojitosheleza kwenye ajira. Kwa iyo chadema ndio wataleta ajira ?..usafiri wa umma unapaswa kuwa wa kujitosheleza ili wananchi waachane na bodaboda.
..pia serikali inapaswa kuweka mazingira ili ajira za kutosha za kudumu, na zilizo na mafao, zizalishwe, ili vijana wasilazimike kubangaiza kwa kuendesha bodaboda.
Nitajie nchi ambayo wananchi wake wote wana ajira za kudumu..usafiri wa umma unapaswa kuwa wa kujitosheleza ili wananchi waachane na bodaboda.
..pia serikali inapaswa kuweka mazingira ili ajira za kutosha za kudumu, na zilizo na mafao, zizalishwe, ili vijana wasilazimike kubangaiza kwa kuendesha bodaboda.
Huko Ulaya Ujerumani, Ufaransa wanaandamana kwa ukosefu wa ajira, hakuna nchi inayojitosheleza kwenye ajira. Kwa iyo chadema ndio wataleta ajira ?
Nitajie nchi ambayo wananchi wake wote wana ajira za kudumu
Hujambo Jeni?
Tukiacha ubinafsi kuanzia raia mmoja mmoja hadi serikali tutatengeneza ajira nyingi na hakutakuwa na haja ya kuwa na bodaboda wengi. Kwa mfano badala ya mtu kununua gari la milioni zaidi ya 500 anaweza fungua mradi fulani ukatoa ajira. Pia wabunge nao kufanya marekebisho ya sheria na kufutilia mbali sheria zinazofanya watu waone shida kufungua viwanda na kuwekeza nchini. Vijana wakulima wangewezeshwa mitaji na kutoa ajira kwa wenzao.
Tatizo huna exposure, hapo kenya tu mpaka wapiga debe wana masters, nigeria ndio usiseme, Tanzania tuna nafuu sana upande wa ajira. Kazi mfano kilimo, uvuvi, zipo nyingi ,tuna ardhi ya kutosha, mito,maziwa, nenda kenya kupata hata ardhi ya hatua moja ya kuweka tuta la mboga ni mtihani, Tanzania bado tuko vizuri, ni uvivu tu wa vijana. Ungejua wakenya, Wazambia,Wamalawi wanavyoitamani Tanzania ungeshangaa..hakuna nchi yenye full employment 100%.
..lakini kwa TANGANYIKA tatizo la ukosefu wa ajira limezidi viwanga vinavyostahimilika.
..Serikali inatengeneza BOMU ikiwa itaamini kwamba BODABODA ndio muajiri mkubwa kuliko wote.
Tatizo huna exposure, hapo kenya tu mpaka wapiga debe wana masters, nigeria ndio usiseme, Tanzania tuna nafuu sana upande wa ajira. Kazi mfano kilimo, uvuvi, zipo nyingi ,tuna ardhi ya kutosha, mito,maziwa, nenda kenya kupata hata ardhi ya hatua moja ya kuweka tuta la mboga ni mtihani, Tanzania bado tuko vizuri, ni uvivu tu wa vijana. Ungejua wakenya, Wazambia,Wamalawi wanavyoitamani Tanzania ungeshangaa
Sasa ni hivi; hata mimi ninamuunga mkono. Tanzania kuna kazi nyingi tu zimegeuzwa kuwa ni laana na nyinyi maccm! Hiyo bodaboda ni sehemu tu ya hizo kazi nyingine.Wadau kibao ❎ wajinga kibao ✅
Mtu kusema nimwonyeshe mtoto wa waziri anayeendesha bodaboda ni upuuzi uliopitiliza. Huko China anapopataja Lema kuna bodaboda na baiskeli kibao zimeajiri watu. Mtoto wangu kutoendesha bodaboda haimaanishi iwe haramu kwa wengine.
Ni muda sasa CCM iingilie kati kwa kuwapa semina hawa wanufaika wa michango ya tonetone huko CHADEMA ili waweze kujenga hoja wanapokuwa jukwaani. Ukisikiliza maneno ya Lema utagundua yeye ndo laana hapa nchini. Kaongea maneno ya kijinga sana kwa hadhi yake.
Hii CHADEMA ya sasa inapaswa kupelekwa darasani kwenye chuo cha CCM Kibaha ili kujifunza namna sahihi ya kufanya siasa na sio huu ujinga wanaoufanya kwa sasa.
View: https://www.instagram.com/reel/DeuEdn9IR1q/?vrfl=N2lhaHoyNHRkb3Q0
Inaweza kuwa ya kipumbavu ila haijafikia ya kwako ambayo haikubali uhuru wa Mawazo.Familia ya kipumbavu kama yako ni sahihi mtoto kujitenga.