God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Umeshawahi kuthibitisha Mungu yupo? Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Thibitisha Mungu yupo.
Hili kila siku nalithibitisha na hapa nathibitisha :

35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? (at-Tur : 35)
 
Logic ni nini?

Daraja lina ukomo? Daraja linakidhi mahitaji ya kuvuka mto?

Yani hapo ulichoandika ni sawa na kusema hutaki kutumia daraja kuvuka mto kwa sababu daraja lina ukomo!

Kufikiri kwamba kitu kikiwa na ukomo hakikidhi mahitaji ni logical non sequitur.
 
Hili kila siku nalithibitisha na hapa nathibitisha :

35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? (at-Tur : 35)
Wewe sio tu huthibitishi, hujui hata kuthibitisha ni nini.

Unachanganya kuhubiri na kuthibitisha.

Hapo umehubiri, hujathibitisha.

Kuhubiri si kuthibitisha.
 
Wewe sio tu huthibitishi, hujui hata kuthibitisha ni nini.

Unachanganya kuhubiri na kuthibitisha.

Hapo umehubiri, hujathibitisha.

Kuhubiri si kuthibitisha.
Nimecheka sana. Sasa unatakiwa ukosoe nilichokiandika usilete dibaji.

Nifundishe kuthibitisha ni nini na kuhubiri ni nini ? Shida yenu huwa mnaishia juu juu.

Aya imekamilika hiyo, ukisoma sababu za kushuka aya hiyo ndipo utakapo jiona wewe ni mjinga na logic ni elimu ya kupigwa vita sababu inawafanya watu kuwa wajinga. Wakana mungu hawajaanza juzi wala jana, bali wale wa kale ni tofauti na nyinyi wale walikuwa wananua kuhoji, wanajua historia na wanajua lugha, nyinyi hamna vyote hivyo.

Kuhubiri ni nini ?
 
Logic ni nini?
Ni fano kupitia fani hiyo humfanya mtu asikosee katika katika kujenga hoja. Zimekuja maana nyingine zikisema logic ni elimu inayo mfunza mtu namna ya kujenga hoja bali zimekuja katika maana za logic (Mantiki) ni elimu ya kutumia akili.
Daraja lina ukomo? Daraja linakidhi mahitaji ya kuvuka mto?
Daraja lina ukomo kwa kile kilichosanifiwa kwacho, maana yake ilikuwa vizuri zaidi kuwa zaidi ya hapo.
Yani hapo ulichoandika ni sawa na kusema hutaki kutumia daraja kuvuka mto kwa sababu daraja lina ukomo!
Hii si maana yangu, naposema akili ina ukomo, ni kwamba ukom wake inakidhi haja na kwa muongozo mzuri wa namna ya kuitumia akili hiyo, lakini kwa ukomo wake pakawa na visaidizi vya kuitoa katika huo ukomo na kwenda mbali zaidi. Hizi ala wanafalsafa wa kale hawakuwa nazo.

Shaykhul Islam Ibn Taymiyah katika kitabu chake "Raddi 'al mantiqiyiin (Ukosoaji kwa watu wa mantiki (logic)) akasema Wanafalsafa walikuwa na maswali sahihi lakini walikosa nyenzo za kufikia majibu sahihi.
Kufikiri kwamba kitu kikiwa na ukomo hakikidhi mahitaji ni logical non sequitur.
Hili kosa lingine.

Kingine uwe unajibu maswali ninayo kuuliza.
 
Uthibitisho unatumia ushahidi na hoja kuonesha uhalisia naukweli , evidence na argument to establish fact and truth.

Wewe umehubiri, hujaweka ushahidi wala hoja, hujaweka evidence wala fact.

Kuhubiri ni kama ulivyofanya hapo, unaweka aya halafu unasema aya imeshuka hiyo.

Una uhakika gani imeshuka na haijatungwa na watu hapahapa duniani? Unaweza kuthibitisha aya hiyo imeshuka na haijaandikwa na watu kama hadithi tu?
 
Umesema logic imeanzishwa na Aristotle.

Mpaka hapo umejionesha ungumbaru wako.
 
Kama ndivyo kwamba Mungu hawazi kama sisi, basi yote tunayoamini hata yaliyoandikwa kwenye so called "vitabu takatifu" bado ni upuuzi cause nayo pia yaliandikwa na binadamu kama sisi. Na the fact kwamba hakuna aliyemuona Mungu na kupiga naye stori mahali, hata wanaosema wamemuona hatuna uhakika sababu, its not in our experience. Hivyo bottom line ni kwamba we don't know nothing.
 
Umesema logic imeanzishwa na Aristotle.

Mpaka hapo umejionesha ungumbaru wako.
Basi vizuri. Kielimu ulitakwia uonyeshe kama logic kama fani haikuanzishwa na Aristoto. Hivi ndivyo wajuzi wa mambk wanafanya.

Nasuburi uje kuionyesha nani muanzilishi wa fani ya Logic.
 
Uthibitisho unatumia ushahidi na hoja kuonesha uhalisia naukweli , evidence na argument to establish fact and truth.
Safi kabisa huwa napata mashaka sana na ufahamu wako, yaani akili yako ni ndogo sana kiasi kwamba huujui uhalisia na hoja.

Aya niliyo kuwekea ina uhalisia ambao ndiyo fack, tena ile self evident truth.

Ngoja nikuonyeshe hualisia na uthibitisho katika hiyo aya. Hiyo aya imetoa changamoto kwa wale wanao mkana Mola, na kuwauliza maswali mawili :

1. Je sisi tumejiumba wenyewe au
2. Tumetokana pasi na kitu chochote ?

Sasa ili hayo maswali yasiwe hoja wala yasiwe na uhalisia unatakiwa ututhibitishie ya kuwa aidha sisi tumejiumba wenyewe au tumetokana pasi na chochote.

Sasa nasubiri majibu ya maswali hayo.
Wewe umehubiri, hujaweka ushahidi wala hoja, hujaweka evidence wala fact.
Kwanini hujifunzi maana za maneno kabla ya kuyatumia. Hapo nimehubiri nini ? Kwamba dunia imejiumba au nyinyi mmejiumba ?

Hapo hakuna facts ? Huo siyo uhalisia ? Sasa jifunze kuifata hoja na kuikosoa siyo kuikimbia na kulalama. Yaani hujawahi kuifata hoja bali siku zote huwa unaikimbia hoja.
Kuhubiri ni kama ulivyofanya hapo, unaweka aya halafu unasema aya imeshuka hiyo.
Hapo sija hubiri bali nimehoji na kuthibitisha yaani kunukuu yale ambayo wajinga wenzako wa kale walikuwa wakikanusha.
Una uhakika gani imeshuka na haijatungwa na watu hapahapa duniani? Unaweza kuthibitisha aya hiyo imeshuka na haijaandikwa na watu kama hadithi tu?
Hili swali huwa unalikwepa sana, hujawahi kunijibu kwanini unasema ni hadithi ?

Mimi nina uhakika sababu kuna chain ya mapokezi ya hizo habari.
 
Basi vizuri. Kielimu ulitakwia uonyeshe kama logic kama fani haikuanzishwa na Aristoto. Hivi ndivyo wajuzi wa mambk wanafanya.

Nasuburi uje kuionyesha nani muanzilishi wa fani ya Logic.
Aristotle systematized logic, but logic was there before Aristotle.

Plato and Socrates used logic.

The pre-Socratic philosophers used logic.

Anyone who used language in a systematic way used logic.

Surely, you are not saying Aristotle started language, are you?

Saizi umebadilisha kutoka picha ya Mungu kubadilika mpaka kuongeza taswira akilini mwetu?

Vipi kama kubadilika kwa taswira ya Mungu akilini mwako ni kutokana na kutokuwepo kwake kiasi cha kufanya upate ugumu unapojaribu kumfikiria katika uhalisia?
 
Kukiwa mahala pema maana yake hakuwezekani kufanyika uovu ambao upo ndani ya free will

Kwa maana hiyo mbinguni kuna uroboti
 
Yes, exactly na Mungu will always be mystery. Na atapoteza nguvu zake zote pale mwanadamu atakapomjua complete.
 
Asee nomaa
 
Point
 
Maswali yako ni boring.

Yamejaa logical non sequitur.

Umeuliza.

1. Je sisi tumejiumba wenyewe au
2. Tumetokana pasi na kitu chochote ?

Hapo hakuna swali ambalo linalazimisha uwepo wa Mungu.

Yani nibsawa na mtu anayesema yeye lazima ni mtoto wa Komredi Kipepe . Kwa sababu hajajiumba mwenyewe na haiwezekani awe hakutokana na chochote.

Sawa, labda hajajiumba mwenyewe, labda haiwezekani awe hakutokana na chochote.

Lakini, amefikia vipi hitimisho kwamba yeye ni mtoto wa Komredi Kipepe? Anaweza hata kuthibitisha kwamba huyo Komredi Kipepe yupo kweli nje ya hadithi tu?

1. Kama tumejiumba wenyewe, au hatujajiumba wenyewe, hilo halilazimishi Mungu awepo.

2. Dhana nzima ya "kutoka" ni umasikini wa mawazo tu.

Ni hivi, suala zima la kwamba lazima kuna hiki cha kwanza, halafu hiki cha kwanza kinasababisha kingine cha pili (cause and effect) ni ujinga wetu tu. This is not an indispensable fundamental of the universe.

At the quantum level, the effect can happen before the cause, and the cause can happen after the effect.

Sasa, kama hujui mambo hayo, unaweza kuwa hujui ujinga wako halafu ukanikashifu mimi kuwa sina akili.
 
Hili kila siku nalithibitisha na hapa nathibitisha :

35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? (at-Tur : 35)
Kwa hiyo hapo ndo unakuwa umethibitisha?
 
Yes, exactly na Mungu will always be mystery. Na atapoteza nguvu zake zote pale mwanadamu atakapomjua complete.
Kwa hiyo maana yake hata watu wa dini nao wanapuyanga tu ingawa wanajifanyaga wao ndo wapo sahihi kweli kweli!?
 
Self evident truth unaielewa au unaandika tu imradi umejisikia?

Hiyo uliyoandika wewe hapo ni fallacy of appeal to self evident truth
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…