God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Kwa nini logic kilugha au logic kifani tu?

Kwa nini unajichagulia swali?

How about logic the concept?
 

Limeanza jambo kabla ya taaluma.

Logic kilugha au logic kiistilahi ? Logic hhaikuwahi kusimama nje ya fani. Sasa hili swali lako si sahihi. Ndiyo maana huwezi kuiongelea leo logic nje ya fani. Na ukisoma falsafa na logic wa Watu wa Magharibi ya kale utaona kabisa ni mtindo mpya uliowekwa wa kufikiri.

Aristoto ni muanzilishi wa logic. Kwanini hutaki kutuambia maana ya logic mzee ? Unakimbia kimbia swali rahisi kama hili.

Nawajua wanafalsafa wengi kabla ya Aristoto kama vile Homeri mshairi kadhalika Thales na wengine. Nitajie ambao walikuwa wanatumia logic kabla ya Aristoto.
 
Kwa nini logic kilugha au logic kifani tu?

Kwa nini unajichagulia swali?

How about logic the concept?
Shida yenu mlisoma hizi fani bila kufundishwa ile misingi kumi ya kila fani.

Maneno hufasiriwa kwa namna mbili hakuna zaidi kwa namna ya kilugha na kwa namna ya kifani. Mfano maji, maji huelezewa kilugha na kifani, na kifani ni kwa mujibu wa Kemia. Kilugha ndiyo ile kawaida ya mtu akiona maji anajua tu haya ni maji na vingine.

Logic kama wazo huangukia katika fani, kwamba fulani ameelezea vipi tamko logic huyu anakuwa amemili katika mlengo fulani.

Ndiyo maana nimekupa kazi wewe utuambie maana ya logic, lazima utaangukia katika fani. Huwezi kutoka nje sababu najua hamkufundishwa haya mambo.
 
Logic.

reasoning conducted or assessed according to strict principles of validity.

Sasa Aristotle ndiye aliyeanzisha ku asses reasoning according to strict principles of validity?

Hawa pre-Socratic philosophers waliishi kabla ya Aristotle, na walitumia logic.

Aristotle mwenyewe kajifunza dialectic argument kwa Zeno.

Kwa hivyo, haiwezekani Aristotle awe kaanzisha logic.

 
Safi kabisa ndiyo maana nikataka uweke maana ya logic. Maana yako umeielezea kifani na si kilugha. Sasa hapo tunakuja kukutaka ututajie hizo kanuni. Hizo kanuni sasa ndizo zinazo tofautisha logic na Falsafa, logic na Fizikia, kadhalika logic na Metafizikia.

Safi kabisa, tuwekee hizo kanuni walizo zitumia kuainisha hoja kwenye kuutafuta ukweli. Haya mambo mepesi sana, ndiyo maana nilitaka uweke maana.
 
Umesoma link na kujua kwamba Aristotle hajaanzisha logic?

Au Kiingereza mgogoro?
 
Umesoma link na kujua kwamba Aristotle hajaanzisha logic?

Au Kiingereza mgogoro?
Nimesoma mwanzo naona wanamrejelea Aristoto,naendelea kusoma mpaka pale nitakapo ona mfumo na hizo kanuni zilizowekwa kabla ya Aristoto.

Hili la kwanza. Pili, naona umekubali ya kuwa huwezi kuiongelea logic nje ya fani, vyovyote itakavyo kuwa. Kwa minajili hiyo kusema kwako logic ilianza kabla ya Aristoto mathalani, bado inaongelewa kama fani na si kama msamiati wa kilugha. Hili kwanza unatakiwa ukiri.
 
Soma umalize kwanza kabla ya kurudi hapa wakati hujapata elimu kamili.

Wapi nimekubali kwamba siwezi kuiongelea logic nje ya fani?
 
Soma umalize kwanza kabla ya kurudi hapa wakati hujapata elimu kamili.

Wapi nimekubali kwamba siwezi kuiongelea logic nje ya fani?
Kiri kwanza nilichokuandikia kwamba huwezi kuelezea logic nje ya fani. Mimi naendelea kusoma hii link.

Namaanisha ya kuwa kuna vitu hutakiwi kuvibishia wakati vipwazi mno.

Kingine katika makala hii nimeona wanaongelea suala la "Concepts" na "Definitions" hili pia litahitaji mjadala na kujua msingi wa wazo kwa watu hao na suala la definitions je walikuwa wanapatia kulielezea ?
 
Kama fani ni taaluma, vitu kuwekwa rasmi kitaalamu, formalized logic, unaweza kuiongelea logic nje ya fani.

Kwa sababu kuna informal logic. Ni informal, lakini nayo ni logic pia.

Same thing kwenye hesabu.

Watu walijua tofauti ya chungwa moja na mawili kabla hesabu hazijaanza kuwekwa kwenye taaluma na kuwa formal subject, kutengwa kwenye geometry, arithmetics, algebra etc.

Sasa, wewe unachosema ni kwamba, kabla ya hesabu kuwekwa kwenye taaluma rasmi, watu walikuwa hawajui tofauti ya chungwa moja na machungwa mawili.

That is ridiculous.
 
Unapouliza nani...kwani hapa unajadiliana na nani?

Pengine hata fallacy of Appeal to self evident truth huijui na ndio maana huelewi kama umekosolewa
 
Wewe naon unaleta utoto. Ngoja nijadiliane na mwenye afadhali kuliko wewe potelea mbali.
Utoto umeanza kuuleta wewe kwa kile ulichokiandika halafu ukakiita uthibitisho
 
Unapouliza nani...kwani hapa unajadiliana na nani?

Pengine hata fallacy of Appeal to self evident truth huijui na ndio maana huelewi kama umekosolewa
Kijana jenga hoja kutaja hii misamiati ni jambo dogo sana, naweza nikakutajia mpaka ya Kiarabu. Sasa wewe jibu hoja na kosoa hoja.
 
Utoto umeanza kuuleta wewe kwa kile ulichokiandika halafu ukakiita uthibitisho
Sasa ulitakiwa uonyeshe kama si uthibitisho, mwenzako nimemuonyesha kwamba ule ni uthibitisho na ni uhalisia. Sasa kama jambo limekushinda waache wenye kuliweza waende nalo.

Sasa wewe unasema siyo self evident truth, na unashindwa kuonyesha hilo, mimo nimekuonyesha kama ni selft evident truth, nani analeta utoto kati yangu mimi na wewe ?
 
Kama fani ni taaluma, vitu kuwekwa rasmi kitaalamu, formalized logic, unaweza kuiongelea logic nje ya fani.

Kwa sababu kuna informal logic. Ni informal, lakini nayo ni logic pia.
Yaani sasa hapa ulitakiwa uonyeshe kuwezekana kwa hilo jambo kuliko kupoteza muda namna hiyo.

Mfano mimi nikisema siyo lazima usome au ujifunze falsafa ndiyo uwe hodari wa kujenga hoja na kukosoa, ujue hiki nilichokisema au kukiandika naweza kukithibitisha.

Sasa unaposema kuna "Informal Logic" unatakiwa uonyeshe hilo na uweke mifano. Hivi ndivyo watu wanao yajua haya mambo wanafanya.
Same thing kwenye hesabu.

Watu walijua tofauti ya chungwa moja na mawili kabla hesabu hazijaanza kuwekwa kwenye taaluma na kuwa formal subject, kutengwa kwenye geometry, arithmetics, algebra etc.
Hili pia linaonyesha uchachefu wa maarifa yako, suala la kujua idadi ya mambo, miaka kitofautisha mambo haya ameyaweka Mola tangu alipo umba mbingu na ardhi.

Kuelezea hesabu kwa mtindo huu ni kulazimisha ya kuwa hapakuwa na hesabu kabla ya ya kina al-Khawarizm na wengineo wakati wakati suala la kujua idadi ya machungwa hakuhitaji kanuni za kihesabu unazozitaja wewe.
Sasa, wewe unachosema ni kwamba, kabla ya hesabu kuwekwa kwenye taaluma rasmi, watu walikuwa hawajui tofauti ya chungwa moja na machungwa mawili.

That is ridiculous.
Mfano wa hesabu ni mfano maalumu na unavyo hoji kwa mtindo huu unatoka nje ya uhalisia. Ndiyo maana huko nyuma nilikuonyesha wazi namna elimu zinavyoundwa, na ndiyo maana nikatolea mfano maalumu wa tamko logic. Shida yanu mnashindwa kutofautisha mambo ya jumla na mambo maalumu.

Ndiyo maana hao wote waliokuja baadae hawasemwi walimevumbua hesabu, bali vijisehemu tu vya mahasebu.
 
Kwa hivyo kabla ya hesabu kuwa taaluma, watu hawakujua tofauti ya chungwa moja na machungwa mawili?
 
Kwa hivyo kabla ya hesabu kuwa taaluma, watu hawakujua tofauti ya chungwa moja na machungwa mawili?
Unauliza swali ambalo nimeshakujibu tayari.

Hakuna mtu aliye vumbua kwamba moja jumlisha moja ni mbili au mbili toa moja ni tatu au machunga mawili machungwa matatu, hili ni jambo la kimaumbile lipo tangu Mola alipoumba mbingu na Ardhi.

Ndiyo maan leo hii hatusemi fulani kavumbua hesabu, kisha tukakomea hapo. Tunasema fulani alivumbua hesabu za Aljebra, mwingine Culculus na mfano wa hayo.

Jbo la kujua kumi, kujua mbili kujua ngai, ni la azalia mitume wote walikuwa wanajua haya mambo.
 
Nilipoandika 'maana hata kama tupo nje ya logic ya moja kwa moja, logic sio tool pekee inayotusaidia katika kuielewa reality.' Nilimaanisha sio zile logic zamojakwamoja; kama A imemzaa B an B imemzaa C basi C ni mwana wa A. Hapa kuna mtiririko kutoka msingi hadi paa lake.

Bali hii ni analojia ambayo mfano wake ni kusema; unaona jinsi ABC inavyosaundi gudi! basi hata XYZ inasaundi gudi pia😏. Usiandike YXZ haipendezi iga ABC ilivyo ndio sahihi. Tunatumia hiyo kwa sababu kuna mifanano inaweza kutusaidia kujenga mantiki katika vitu vingine hata vyenye asili tofauti. Naitumiaga zaidi kulinganisha mifumo.

Analogy huwa sio uthibitisho wa moja kwa moja wa kitu kama ilivyo logic. Mfano katika sehemu moja ukusaidie kuielewa sehemu nyingine. So hizo non sequtor zako za kufanya uikatae analogy wakati ingekusaidia kuelewa vizuri unajipunguzia mbinu za kuielewa reality.
 
Saizi umebadilisha kutoka picha ya Mungu kubadilika mpaka kuongeza taswira akilini mwetu?

Vipi kama kubadilika kwa taswira ya Mungu akilini mwako ni kutokana na kutokuwepo kwake kiasi cha kufanya upate ugumu unapojaribu kumfikiria katika uhalisia?
Sijabadilisha, nimefafanua. Nimeamua kutafsiri neno picha ili uelewe zaidi maana mimi mda wote ninasisitiza kuwa sisi tunajenga picha/taswira fulani akilini mwetu.

Kubadilika kwenyewe sio kubadilika kihalisi nilikupa mfano nikiwa kadogo nikasema baba ni mkali nikawa na miaka ishirini nikasema baba ni mpendaji. Haimaanishi kuwa sasa hivi ameacha kuwachapa wadogo zangu na wajukuu. Bali nimemuelewa vizuri zaidi kiasi kwamba hata nikimuona kashika kiboko kichani kwangu sitawaza MKALI bali nitawaza MWENYE-UPENDO anatupenda.

Kumbuka baba hajaacha kuwachapa watoto wenye ujinga yupo vilevile anatembeza bakora, ila ni mimi ndio nimemujua zaidi nikaelewa kumbe huo ni upendo na sio hasira na ukali. Au hata nikisema ni hasira na ukali vinavyoashiria upendo alionao. Hakuna kilichokufa, hakuna aliyejidanganya au kudanganya..... ila maarifa yamekua na yaliyokuwapo yameeleweka zaidi.
 
Unaiponda logic na kusisitiza analogy.

Unanionesha hujui kwamba hata analogy ni logic.

Unashusha sana viwango vya mjadala na frankly naona napoteza muda kujadiliana nawe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…