God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

Mada hizi za kumuuliza Mungu nyingi huletwa na wakristo mna dini yao haina mafundisho sahihi
 
Tutajitambua vizuri kabisa na tutatambuana vizuri tu.

Kitu kimoja ni kwamba hata hapa duniani, kadri unavyozidi kuwa na upendo, kupanua wigo wako wa upendo ndivyo 'attachment yako' kwa ubinafsi inavyozidi kupotea. Namaanisha mtu asiye na regard na mwingine bali yeye tu anao upendo sifuri. Lakini atakayempenda ndugu wa damu tu huyo anao upendo assume wa moja. Yule atakayeongeza na upendo kwa kila jirani yake huyo labda anao wa elfu na akizidisha hadi akapenda nature na mawe na fisi na majani na swala huyo anaelekea upendo infinity, upendo ambao ni upendo wa kimungu anayependa hadi magalaxy mazimamazima!

So mtu kujimilikisha 'ooh huyu mke wangu nampenda' au 'mtoto wangu ningependa kuwa karibu naye na sio mtu baki katika kula raha' hapo bado unakuwa na ego attachment kujimilikisha vitu/watu.
Angalia mfano wa Yesu aliwapenda jirani zake kwa kiwango cha kimungu na ndio maana hata ndugu zake hadhi yao ilikuwa sawa na wooooote wanaolishika na kulifuata mapenzi ya Baba. Nadhani hii ndiyo kiashiria cha 'kujikana nafsi yako' yaani kutokuwa na ubinafsi bali kujawa na upendo. Upendo haubagui, hautafuti vya kibinafsi etc etc
 
wapi ulichagua kuzaliwa, unafikiri ungepewa nafasi ya kuchagua ungechagua kuzaliwa maxingira uliyopo. Why ulikuwa walia ulivyozaliwa tu
Kisayansi kulia wakati wa kuzaliwa ni ishara ya uhai, pia ni matokeo ya reaction inayosababishwa na kubadilika kwa mazingira ya mtoto kutoka tumboni hadi duniani.

Hauchagui mahali ama mazingira ya kuzaliwa kwa kuwa Mungu anakupa akili na utashi the moment anapokuumba. And just like personality; intellect and will develop in the course of time.

Ndio maana tunaamini athari (consequence) ya maamuzi yetu inategemea na levels za uelewa wetu juu ya jambo husika.

Atakavyohukumiwa shetani si sawa na atakavyohukumiwa Baba Mtakatifu au atakavyohukumiwa Padre wa kawaida au tutakavyohukumiwa sisi au watakavyohukumiwa wapagani.

Kila mmoja atahukumiwa kulingana na level yake ya uelewa wakati anafanya maamuzi husika. Luka 12:48


- wapi ulichagua kuwa muumini wa dini unayoabudu. Jee wazazi wako wangekuwa dini tofauti na yako uliyonayo sasa hivi, ungekuwa na dini hii unafikiri?
Ndiyo, kuna watu wengi wamezaliwa na wazazi wapagani ila wao wamekuwa Wakristu.

Kuna watu wengi wamezaliwa na Wakristo ila wao wameamua kuwa Wapagani.

Kuna watu wengi tu wamezaliwa dini A nao wameamua kubadili na kuwa dini B.

Wanatumia freewill zao watakavyo.



- kwa wale walio na magonjwa ya kurithi, hivi kuna sehemu walichagua kuwa nayo au the whole sequence of events was predetermined from moment their parents fall in love to moment they conceive.
Magonjwa hayahusiani moja kwa moja na mtu kuwa mwema ama muovu.
 
Did you use your freewill to write this comment, or you were programmed to write it?
As I said there is no freewill at all, it is just an illusion

Free will haipaswi kuwa na mipaka, na kwa perception ya kimungu, hiyo comment sijaandika kwa utashi wangu na nilikuwa sina uwezo wa kuepuka kutoiandika. ikiwemo na hii nayoandika sasa

Ephesians 1:11


11 All things are done according to God's plan and decision; and God chose us to be his own people in union with Christ because of his own purpose, based on what he had decided from the very beginning.

Ikiwa kila kitu ni mipango ya Mungu utasemaje tuna freewil?

Kama tuna free will kivipi kila jambo liwe ni sehemu ya mipango yake?
 
Kwa hiyo Mungu alidhamiria kabisa kumuumba Shetani ili kuleta balance, sasa kwa nini shetani alaumiwe wakati kumbe yeye aliumbwa ahamasishe ubaya ili alete balance?
Mungu hakumuumba shetani, ila Malaika mwema kabisa anayeitwa Lusifa. Kila alichokiumba Mungu kilikuwa chema (Mwanzo 1:31).

Shetani ni matokeo ya uamuzi wa malaika mwema Lusifa kuamua kuwa muovu.

Hivyo, Mungu hakuumba na haumbi uovu ama waovu. Ni sisi ndio tunaamua kuwa wema ama waovu.

NB: Uovu ni terminology tu inayotumika kuelezea vitu au watu wasio wema. In fact, evil do not exist but merely a terminology that depicts the absence of good and goodness.


Mbona wakati wana wa Israel walipikuwa wanatenda hiyo iitwayo dhambi alikuwa anaona na alikuwa akikasirika sana?
Aliona na hakuingilia uamuzi wao. Na hiyo ndio freewill, upo huru kuamua chochote. Changamoto inakuja kwenye matokeo ya uamuzi wako.

Vipi kuhusu Daudi kuzini na mke wa mwanajeshi wake na utamu ukamkolea akaamua asuke mpango wa kumuua huyo mjeshi ili amchukue kabisa mke wa huyo jamaa mbona alimuona hadi akamtuma nabii kwenda kumweleza ni jinsi gani yeye (Mungu) amekasirika...?
Mungu aliona yote lakini hakuingulia, maana hajihusishi na kuingilia uhuru wa watu. Na hiyo ndio freewill yenyewe tunayoiongelea.

Unakuwa huru kufanya uamuzi huru. Mungu anachokifanya ni kukupa taarifa zote ili ufanye informed decision na uwe tayari kuwajibikia matokeo ya uamuzi wako - bila kujali kama ni mema ama maovu.


Mnona kaini alipomuua nduguye Abeli
Bado Mungu hakuingilia uamuzi wa Kaini, maana Kaini pia alikuwa na freewill.

Mifano yote uliyoitoa inathibitisha Mungu haingilii uamuzi wetu. Ni sisi ndio tunaamua hatma yetu.

Yeye anatusaidia kutupa taarifa zote muhimu ili tufanye informed decision na tuwajibikie consequences zake.
 
Umeielewa vizuri sana. Wengi tunamlaumu Mungu kwa matokeo ya uamuzi tulioufanya badala ya kuuwajibikia.
 
Mimi kuna rafiki yangu kutokana na kumjua yeye na demu wake niiliwahi kumtabiria kuwa haitopita muda fulani lazima wataachana ,sababu za kuachana na aina gani ya mwanaume atakaye mfuata na nikampa na muongozo wa kufanya kuepusha hilo jambo lkn akanipuuza siku baada ya siku kadhaa kila kitu nilichokisema kilitimia kila kitu mpk muda jamaa aliniona mimi mtu wa ajabu lakini siku mlazimusha na tahadhari nilimpa na nikajua matokeo kutokana na uzoefu wangu mpk akawa akipatwa na majambo yake aninifata nimpe muongozo.
 
Huwaga najiuliza Yuda sana kimaelezo Yuda alikua ashaandaliwa sikuona kosa !!
Lakini niliwahi kupewa jibu kwamba Mungu ametoa uwezo wa kusamehe yaani kutubu hivyo basi hata kama kuna maandiko tunapaswa kutimiza tunapewa nafasi kurudi kundini…
 
Unakakubali kuwa kila jambo hutokea kwasababu au kuna bahati mbaya?
 
Naam, twende taratibu, utaelewa.

Ni kweli kabisa Mungu anajua yote kabla hata haujaumbwa. Anajua kabisa utakuwaje, utaishije, na utakufaje. Anajua yote.

Freewill haihusiani na yeye kujua yote. Freewill is all about Mungu kutupa uhuru kamili wa kuchagua tuwe akina nani, tuishi vipi na ama tuwe wema ama wabaya.

Utashi huru unaupata kwa kuwa Mungu amekupa uhuru kamili wa kufanya uamuzi uwao wote.

Look; Mungu anajua kila kitu lakini hajakupangia chochote. Mungu anajua matokeo ya uamuzi utakaoufanya lakini hajakupangia ufanye uamuzi wowote. Amekuacha wewe uamue.

Kwa kuwa anajua kila kitu, amekupa akili na utashi ili vikusaidie ufanye uamuzi sahihi ukiwa na taarifa zote (informed) za uamuzi unaochagua kuufanya na matokeo (consequences) yake.
 
Huwaga najiuliza Yuda sana kimaelezo Yuda alikua ashaandaliwa sikuona kosa !!
Lakini niliwahi kupewa jibu kwamba Mungu ametoa uwezo wa kusamehe yaani kutubu hivyo basi hata kama kuna maandiko tunapaswa kutimiza tunapewa nafasi kurudi kundini…
Mungu ndiye anayepaswa kuomba msahama kwa Yuda kwa kumuumba na hali ya usaliti kwa kusudio maalumu ambapo Yuda hakuwa na option ya kuepuka
 
Ndio mkuu upo sahihi Mungu hatuamulii wapi pa kwenda ila swaki la Muhimu ni je Mungu anajua mimi nitachagua Uzuri au ubaya??
Hilo ameliwekea siku ya hukumu ,ila uwezo WA kujua anao , alishaamua amekupa uchaguzi , so in between hapo utamua mwenyew hatma yako ambayo itajulikana siku ya hukumu
 
First of all, freewill haina mipaka, not even God can intervene.

Waefeso 1:11
na ndani yake sisi nasi tulifanywa urithi,
huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye,
ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.


Hapa Mtume Paulo anaelezea namna Mungu aliye huru anavyotumia uhuru wake kutusaidia tuendelee kuwa wema.

Yaani kama ambavyo mimi nina freewill kwa mambo yangu, na ambavyo wewe ulivyo na freewill kwenye maamuzi yako, ama ambavyo mtu mwingine yeyote alivyo na freewill kuamua mambo yamhusuyo; Mungu naye ana freewill.

Na ameamua kuitumia freewill yake kuwa mwema na kusaidia wanadamu kuwa wema kama yeye alivyo.

Hayo ndiyo mapenzi yake aliyoamua kuyachagua, kama ambavyo sisi nasi tuna mapenzi yetu tunayoyachagua.
 
Pamoja na kujua kila kitu lakini haukuingilia uamuzi wake. Ndivyo afanyavyo Mungu. Anajua kila kitu, anaweza kila kitu na yupo kila mahali ila haingilii uamuzi wetu.
 
Huwaga najiuliza Yuda sana kimaelezo Yuda alikua ashaandaliwa sikuona kosa !!
Lakini niliwahi kupewa jibu kwamba Mungu ametoa uwezo wa kusamehe yaani kutubu hivyo basi hata kama kuna maandiko tunapaswa kutimiza tunapewa nafasi kurudi kundini…
Maandiko gani yamemtaja Yuda kuandaliwa kumsaliti Kristo? Tuwekee hapa.
 
Kujua kwa Mungu mambo yote hata kabla sijazaliwa kunanizuia kufanya mimi nayo taka unless niwe na option ya kufanya kile ambacho yeye hajakiona au kwenda kinyume na alivyoona

Kupitia mfano wa calvin aliyeua makumi ya watu. Sasa kama mimi tu nimetengeneza madai lakini hakuna mtu yeyote rational ambaye ameweza kuniamini kuwa sihusiki na mauaji hayo aliyosababisha calvin na kuwa sikujua kitachokwenda kutokea baadaye

If this is what people would think about me, then what should we think about God?
 
Kabla ya kuzaliwa kwako Mungu akijua utaua, una option ya kutoua?

Kama huna option ya kutoua utasemaje sijazuliwa kufanya nachotaka?
 
Kama waliweza kumsulubisha bila kuwa na ushahidi wa kweli, wangeshindwa vipi kumkamata bila hata ya usaliti wa Yuda?
Wangeshindwa kwa sababu walikuwa hawamjui ni nani, alikuwa sometimes anashinda maporini kusali. Afu pia ukisoma vizuri maelezo yanaonyesha kama hakutaka kukamatwa hivi. Maana pale yuda alivyokuja kuzuga kwa kumkisi, yesu akamkata kabda hajatoka karibu nae akwambia una msaliti mwana wa adamu kwa kumkisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…