God's Conscience vs Free Will: Je, Mungu anajua hatima ya wanadamu itakuwaje?

If God is both omnipotent and benevolent, the precence of evil is a contradiction. How can He allow evil? Then He is not omnipotent.
What has omnipotent got to do with benevolent?

Two totally different attributes.

You are confused. Totally.
 
Omnipotent=all powerful, benevolent=loveness or kindness. Although I'm not good in language, try to check from the dictionary. Now check the statement "God is both benevolent and omnipotent". Can you comment? But rationally.
 
Omnipotent=all powerful, benevolent=loveness or kindness. Although I'm not good in language, try to check from the dictionary. Now check the statement "God is both benevolent and omnipotent". Can you comment? But rationally.
Where is the contradiction? Or you also don't know the meaning of contradiction?

Don't waste our time, since you admit that you're "not good in the language", you have no right to argue on "contradiction".
 
Basi Mungu hayupo, tunapoteza mda kutafuta kitu ambacho hakipo. Hivi ni wa kike au kiume? Labda tuseme kitu ambacho ndicho mwanzo wa vyote ambacho hakina jinsia. Ila tupambane na vinavyoonekana ili tujue asili yake ni nini.
 
Basi Mungu hayupo, tunapoteza mda kutafuta kitu ambacho hakipo. Hivi ni wa kike au kiume? Labda tuseme kitu ambacho ndicho mwanzo wa vyote ambacho hakina jinsia. Ila tupambane na vinavyoonekana ili tujue asili yake ni nini.
Mungu yupo... Na utathibitisha uwepo wakepale tu utakapoacha kumjumuisha katika muda. He exist beyond time and space
 
Where is the contradiction? Or you also don't know the meaning of contradiction?

Don't waste our time, since you admit that you're "not good in the language", you have no right to argue on "contradiction".

[emoji23]
 
What is the meaning of the term "contradiction" according to Aristotle "logic" . I said God cannot be Omnipotent and Benevolent, my point is that if He is omnipotent, how can He allow evil? You can't find any sign of contradiction? Space and time try to look at the femous man known as "Albert Einstein".
 
Una maoni gani/perception kuhusu Mungu??
 
Swali la Msingi katika mada hii ni Uhalisia wa uwepo wa Hiyari(free will) kwa Mtu.

Maswali yako yanaihoji zaidi imani yako Juu ya Mwenyezi Mungu Kama ipo sahihi au la!.

Ikiwa hupati Majibu katika Imani yako basi ujue tatizo lipo kwenye Imani yako na si Uhalisia wa Jambo ambalo unaliuliza.

Katika Bibilia na Quran vyote vimeandika Mungu baada ya kuumba vitu vyote na kabla ya kumuumba Mtu alionyesha azma ya juu ya alivyo viumba!
Kwenye Bibilia Mungu anaonyesha lengo la kumuumba Mtu ni kwa ajili ya kuwa msimamizi na mtunzaji wa vitu vyote katika nchi. Zingatia kwamba lengo limetangulia kabla ya kumuumba.
Katika Quran Mungu pia anaonyesha lengo la kumuumba Mtu kabla ya kumuumba pale alipo waambia Malaika" Mimi nitaweka katika Ardhi kiongozi(Khalifa) Msimamizi na mwangalizi wa vitu vyote.

Kabla ya kwenda kutafuta Majibu mbele ya tukio yakupasa utulie katika lengo hili na kutafakari ili kupata Majibu.

Unatakiwa kutafakari huyu kiongozi ,Msimamizi,Mwangalizi wa vitu vyote anatakiwa awe vipi ili aweze kuifanya kazi iliyo kusudiwa!.

USIMAMIZI JUU YA KITU: kitu mpaka kuwa na sifa ya kusimamiwa,au kutunzwa au kuongozwa, Ni kwamba kitu hicho kinakuwa na sifa kutoleta ufanisi kisipo simaniwa, kuharibika kisipo tunzwa,na kuto ongoka kisipo ongozwa.

MSIMAMIZI: Msimamizi ili aweze kutenda kazi kwa ufanisi ulio kusudiwa ni lazima awe na sifa zinazo weka kukidhi majukumu anayo pewa!
Kujua namna kusimia kitu ambacho kina sifa ya ulazima wa kusimamiwa, ikiwa na maana kisipo simamiwa hakitaleta faida na badala yake kitaleta madhara.
Msimamizi ni lazima ajue faida ya usimaimizi na ubaya wa Kuto simamia!
Kwa maana nyingine ni lazima aujue wema wa kitu na ubaya wa kitu ili aweze kukisimamia kibaki katika wema ambao anaujua na kisilete ubaya anao ujua,
Vile vile kutunza kitu, Ina maana ni lazima kile chenye kutunzwa kiwe kina sifa mbili sifa ya kubaki katika uzuri kikitunzwa au kuharibika kisipo tunzwa!
Ni lazima mtunzaji awe na sifa ya kujua uzuri ni upi katika anacho kitunza na ubaya ni upi asipo kitunza!
Hivyo kwa kuwa kaumbwa kwa ajili ya kutunza Basi ni lazima ajue wema na ubaya wa kile anacho kitunza ili akitunze kisiharibike.
Vile vile kuongoza ni lazima kiongozi ajue hii ndiyo njia sahihi na hii siyo njia sahihi( njia ya wema ni ipi na njia mbaya ni ipi).

Tafakari hii ni kabla Mtu hajaumbwa ,unatakiwa kujua sifa anazo takiwa kuwa nazo kwa kuangalia lengo analo letwa kwa ajili ya kulitimiza.

Tukija Ndani ya Edeni tunamkuta Adamu akiwa hajui kuchanganua lililo sawa na lisilo sawa hata hajui Kama yupo uchi au kavaa!
Ni sawa sawa na Mtoto ambaye bado hajaweza kuchanganua Mambo!.

Kwa kawaida Mtoto mdogo, au Mnyama hapewi Usimamizi wa vitu si kwa sababu wao si viumbe la!
Bali ni kwa sababu ya kukosa sifa ya uchanganuzi(hili sawa na hili si sawa).

Kwa hali ya Adamu aliyo kuwa nayo Edeni ya kukosa Elimu ya upambanuzi bado ilikuwa haimpi sifa ya kuwa msimamizi wa vitu vyote.

Si Jambo rahisi kusimamia kitu ambacho hukijui Wala hujawahi kukiona katika Maisha , Adamu alihitajia kupata semina elekezi ya namna gani ataweza kutimiza majukumu yake.

Mungu alimwambia Adamu "KULA KATIKA BUSTANI HII CHOCHOTE UPENDACHO" hapa Adamu anaongozwa na Mungu nini cha kufanya!
"USILE KATIKA MTI HUU" hili ni katazo!
Kwa hiyo tunapata KULA ni Muongozo sahihi wa Mungu!
USILE: Ni katazo la Mungu.
Adamu anafundishwa namna ya Kufuata Muongozo na kukatazika kwa Maonyo.

Mungu anamleta Ibilisi Edeni, huyu Ibilisi aoishafukuzwa katika rehema ya Mungu iweje awepo tena Eden?
Ukitafakari utagundua Mungu alimleta Makusudi kwa Adamu ili ajifunze ubaya wa Ibilisi.
Akamuacha Ibilisi amdanganye ili ale katika Mti alio katazwa!
Kitendo cha Adamu kula katika Mti ule ni kukiuka katazo la Mungu.
Mti ule ulikuwa ni kielelezo cha ile sifa ambayo Adamu alikuwa bado hajaipata sifa ya kujua wema na ubaya ambayo ilikuwa ni lazima awe nayo ili kutimiza lengo la kuumbwa kwake.

Kwa ushawishi wa Ibilisi Adamu anakula katika mti aliyo katazwa na Elimu ya Utambuzi wa wema na ubaya unambainikia!
Ili kutambua Madhara ya ubaya wa kitu na uzuri ni lazima uwe katika hali ya utimamu wa akili.
Ndiyo maana Mungu aliruhusu Utambuzi upatikane katika tukio hili.
Ili Adamu aweze kuona na kutambua kosa lake na aweze kumtambua Adui mwenye kumshawishi kuacha Makatazo ya Mungu.

Kwa Mujibu wa Quran baada ya Adamu kufanya kosa kwa kula Katika mti ule,Mungu aoimfundisha Adamu Jinsi ya kuomba msamaha,
Si rahisi kwa Kiumbe kipya kujua nini maana ya kosa na nini maana ya kuomba msamaha bila mafunzo ya vitendo!
Hivyo Mungu alimfundisha Jinsi ya kuomba msamaha anapo fanya makosa!
Baada ya Adamu kuomba Msamaha Mungu akamsamehe!
Ila alimfukuza asikae Eden(peponi Mahali pa Ahadi ya Maisha ya Milele) kwa sababu haikuwa lengo .
Lengo ilikuwa ni kuishi katika dunia hii tunayo Ishi akiwa na utambuzi na Elimu kamili ya Usimamizi .

Kwa hiyo katika tukiobla Edeni Adamu Alijifunza baada ya kutolewa kwenye neema!
Anajua kilicho msababisha kutoka katika neema ni kutifuata Muongozo wa Mungu na kuto katazika na katazo la Mungu!
Na kamuona Ibilisi kuwa ni adui kwa sababu huyo ndiyo aliye mshawishi kuacha Kufuata Muongozo na kufanya aliyo katazwa!
Kwa hivyo amejifunza!

Huku katika Maisha haya ya Dunia halisi adamu kapewa Muongozo yeye na kizazi chake ,atakuwa mwalimu mwema wa kuongoza kizazi katika Kufuata na kutii Muongozo.
Kapewa Makatazo atakuwa Mwalimu mwema kwa kizazi chake kutii Makatazo ya Mungu.

Kauona uadui wa Ibilisi,atakuwa Mwalimu kwa kizazi chake kuwafundisha wamuepuke Ibilisi na ushawishi wa kutotii Makatazo ya Mungu.

Aliishi Padiso, atawahadithia kizazi chake mahali pa ahadi ya Milele kwa kuwa yeye ameishi kwa Muda.

Sasa hizo hadithi za Mungu alikuwa anapunga upepo hazina maaana! au hajui nini Adamu atafanya ni hadithi za kupuuza!
Umesha ambiwa ndani ya konde Hilo kuna Magugu na ngano wewe kwa kuwa unaakili salama,inaweza kutambua hii ngano na hili gugu.

Kuhusu Adamu kuto kuwa na Mke kabla! haimaanishi kwamba Mungu alikuwa hajui kuwa Adamu atahitajia mke.
Kabla ya kujenga dhana hiyo hasi kwa Mungu kwanza tafakari umbile la Adamu mpaka yeye kuwa na umbile la namna ile ni maana kwamba Mungu alimuumba vile kuwa Mwanamume anaehitajia mke kwa hiyo ni suala la muda tu.
Kabla Mungu hajamuumba Mtu alisema atamuumba Mtu mume na Mtu mke wakaijaze dunia!.
Lazima aliweka mpango wa kjzaana ambao ndiyo unaupata katika umbile la Adamu.
Tazama wanyama ndege wote waliwekwa dume na Jike kwa ajili ya kuzaana ! Kwa hiyo Adamu kuwa dume kwa wakati huo Mungu alikuwa anajua kabla suala Hilo.

Kuhusu free will ni kwamba binaadamu wamepewa Jambo na lipo wazi hata kwako wewe!
Suala la kuamini au kuto kuamini ni swala la Hiyari Ila Mungu anakuta uitumie hiyari yako kwa kufuata Muongozo wake na kumuabudu yeye peke yake.
Jambo hilo ndilo litakalo kupa faida na ufanisi wewe!
Wakati hiyari ya kuchagua uovu ni maangamivu kwako.

Mungu anataka tutumie uhuru wa maamuzi utufikishe katika mafanikio yetu,
Adhabu anazo zitoa kwa wale wanao tumia hiyari zao vibaya kwenda katika njia ya maangamivu si kwa ajili ya kumpokonya mtu uhuru wa kuchagua bali ni adhabu za kutulea tukumbuke njia sahihi.

Ni Kama mwalimu anapotoa adhabu kwa wanafunzi lengo likiwa ni kuleta ufanisi kwa watu.

Lengo la Maisha ni wapatikane walio tumia hiari zao kwenda katika Njia ya wema!
Hawa wanao tumia hiayari zao nje ya lengo hawatokuwa na faida katika Maisha ya duniani Wala peponi.
 
Hakuna free will duniani.

Yani hapa nikikuuliza tu kati ya Pele, Maradona na Messi nani zaidi, nishakutoa mawazo yako kutoka unachowaza na kukupa mawazo ya kupambanisha Pele, Maradona na Messi.

Hatujui hata wazo litakalotujia sekunde ijayo, hapo freewill itatokeaje?
 
Sijajua hiyo hiyari unataka kuiweka kwenye Mrengo gani.!

Hiari ipo kwenye maamuzi sio fikra!.
Siwezi kutoka katika wazo kwa kuulizwa swali tu! naweza kutoka pia kwa kutazama kitu kikanitoa katika wazo nililo nalo

Hiyari si sifa ya kujua nini kitatokea mbele!

Hiyari ipo katika kuchagua .
 

Unakubali kwamba external factors zinaweza kukuonesha kwamba huna control ya mawazo na matendo yako. Hivyo, huna freewill.

Wewe ukiona chakula kizuri tu mwili wako una respond bila kutaka, ukiona mwanamke mzuri tu mwili wako una respond bila kutaka, hapo kuna freewill gani?

Wewe hujaamua hata uzaliwe wapi, tarehe gani, na wazazi gani.

Hujaamua utakuwa na vinasaba gani.

Na haya ni mambo yanayokusababishia mengi sana katika maisha yako.

Mfano, hapa naandika Kiswahili, hii ni lugha uliyoifahamu kutokana na ajali ya kuzaliwa ulipozaliwa mwaka uliozaliwa.

Ungezaliwa Nantes Ufaransa mwaka 1600 usingeongea Kiswahili, usingekuwa JF, usingekuwa katika mjadala huu.

Halafu leo unaweza kujiona umeamua kutumia Kiswahili, umeamua kuingia JF na ndani ya JF umeamua kuchagua kuingia katika mjadala huu.

Kumbe hujaamua wewe, yote yamewezekana kutokana na ulipozaliwa na mwaka uliozaliwa.

Wewe unajiona umechagua, kumbe hata seti ya unavyochagua ishachaguliwa na chance events.

Wewe ni kama mtu anayeangalia movies Netflix. Mwenyewe anajiona anachagua movies za kuangalia. Kumbe na yeye kashachaguliwa movies gani achague, movies ambazo hazipo Netflix hana uwezo wa kuzichagua aziangalie Netflix.

Hamna free will hapo, kuna illussion ya freewill tu.
 
Nini maana ya Mungu kujua kila kitu kabla Mtu hajafanya?.

Jibu; Kwa sababu Mungu kamuumba Mtu Kisha akampa sifa ya kubaini Kisha akambainishia Njia mbili njia ya sawa na njia ambayo si sawa!
Kisha akamfundisha kwamba ili afikie lengo la kuwa mtu mwenye sifa ya ukamilifu ni lazima afuate njia iliyo sawa!
Kisha akampa na usaidizi wa waalimu wakumsaidia kuweza kuiona njia ya sawa na akampa na vitabu vya maelekezo ya Kufuata njia iliyo sawa!
Kisha kampa hiyari ama achague njia iliyo sawa ili afikie lengo kusudiwa au achague njia isiyo sawa apate maangamivu.

Lengo likiwa afikie njia ya sawa!
mfano umwambie Mtu kaa hapa fanya Mambo yote ila usishike hiki chuma ni cha Moto !
Mtu kushika chuma au kuto shika ni hiyari yake! akishika na kuungua ni kwa sababu yeye kachagua kuungua baada ya kupewa maonyo!.

Mwalimu anajua wanafunzi wake kwamba kwa mtihani huu huyu atafaulu na huyu atafeli!
Kujua kwake hakumfanyi afaulishe mtu bila mtihani au kumfelisha bila Mtihani.
Atakae faulu mtihani ni kwa Juhudi zake na atakae feli ni kwa uzembe wake!.
Mwalimu kujua kuwa utafaulu au kufeli hukubadili matokeo!

Matokeo mabaya ya Maisha tunayo yapitia yanatokea kwa uzembe wetu!
Kwa sababu Maisha ndiyo Mtihani wetu !
Mungu kujua nani atafaulu na nani atafeli haina maana kwamba aingilie hiyari alio tupa!.
Yeye anasubiri siku hiyo wewe Mwenyewe utajijua kuwa umefeli.
 
Maisha yote yana lengo moja!.
Hiyari ipo katika yale Maisha uliyo pangiwa!
Siyo Maisha uliyo chagua!

Hukupewa hiyari ya kujichagulia Mahali,lugha ,wazazi au wakati!
Maisha yako yanaanzia pale mahali ulipo zaliwa ,wazazi walio kuzaa lugha uliyo ikuta na wakati ulio ukuta!
Kwa kuwa Maisha yako yameanzia hapo basi hiyari ya kuchagua baina ya njia mbili inaanzia hapo!.
 
Msamiati wa hiyari umepatikana katika Maisha haya tunayo yaishi.
Kwa hiyo maana halisi ya hiyari huwezi kuitoa nje ya Maisha haya!.

Hicho unacho kiita hiyari kwa tafsiri yako ni dhana ya kufikirika isiyo weza kutekelezeka katika mfumo huu wa Maisha tunao uishi.

Nyumba yoyote utakayo ingia utaona Kuna choo chumba cha kulala n.k!
Kuingia katika choo ni kufuata kilipo wekwa sio kwa sababu unataka wewe choo kiwe sitting room Basi kiwepo!.

Msamiati wa hiyari umeundwa juu ya uhuru wa kuchagua vilivyoko siyo visivyo kuwepo!.

Ukitumia msamiati huu nje ya Maisha haya utakuwa hukuutendea haki
 
Huyo Mungu mwenyewe mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote katungwa na watu tu, hayupo kiuhalisia nje ya tungo hizo.

Kama unabisha, thibitisha yupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…