Hoja zako zimejikita katika uwepo wa Mungu ambaye huwezi kuthibitisha yupo.Maisha yote yana lengo moja!.
Hiyari ipo katika yale Maisha uliyo pangiwa!
Siyo Maisha uliyo chagua!
Hukupewa hiyari ya kujichagulia Mahali,lugha ,wazazi au wakati!
Maisha yako yanaanzia pale mahali ulipo zaliwa ,wazazi walio kuzaa lugha uliyo ikuta na wakati ulio ukuta!
Kwa kuwa Maisha yako yameanzia hapo basi hiyari ya kuchagua baina ya njia mbili inaanzia hapo!.
Hii hiyari mnaitafsiri vibaya!Huenda Mungu alishapanga mtu wa motoni na Mbinguni, hakuna free Will. Ukiua mtu ilishapangwa hivyo ili upalilie moto wako. Ukitenda mema ilishapangwa hivyo ili kuandaa njia ya Mbinguni. Ila duniani wa motoni wapo wengi sana.
Huo ni utumwa wa fikra kufikiria kwamba wayahudi wanaakili kuliko binaadamu wote!.Akili yako binadamu hata wale Wayahudi wenye akili kuliko binadamu wote, ni finyu mbele ya Mungu, hivyo hawezi kukuachia maamuzi, anakuamulia. Linganisha wewe na mtoto mdogo, hapo wewe ni Mungu na mtoto ni binadamu, je unaweza kumuachia mtoto ajiamulie? Basi hata sumu atalamba kwa kutokumchunga. Basi akili zetu mbele ya Mungu ni finyu kuliko huyu mtoto.
Hilo la Wayahudi ni Maoni yako binafsi ,Kwanza kabisa swala la Wayahudi kuwa na akili nyingi hulikwepi, mahali popote duniani penye mafanikio makubwa hasa ya kisayansi ni Myahudi au asili ya Uyahudi. Waliogunndua maformula mengi ya sayansi wana asili ya Kiyahudi. Ni hao hao waliokudanganya ufunge macho usali ili wazidi kukunyonya. Twende kwenye mada, ni swala zima la "free Will" for me is big NO, we are determined. One philosopher spoke about "pre-destination" study a bit about it.
Kwanza Mimi si katika hiyo imani ya kanisa!.Unachoamini huenda ni uwongo, zamani kanisa liliamini jua ndilo linazunguka Dunia, waliopinga waliuwawa. Mpaka wakati wa Copernicus revolution. Basi huenda hoja zako za kuamini uwepo wa Mungu si kweli. Duniani hakuna maabara ya kuhakikisha uwepo wa Mungu. Tuamini tu kwa umbaaaaali! Kuwa kuna "first cause" Hiyo utaijua wakati roho itakapotengana na mwili.
Ufafanuzi mzuriKwanza Mimi si katika hiyo imani ya kanisa!.
Pia Kuna kitu ambacho hukielewi au hukutumia neema ya akili kutafakari na kufanamu.
Tunapo sema Ujumbe wa Mungu umekuja kwa watu wanao ishi katika dunia!
Maekezo yoyote yatakayo tumika kuelezea Jambo ni lazima yachukue uoni wa mahali husika!.
Nakupa Mfano Chukua Mpira wa Miguu,
Fanya upande wa kitundu cha kujazia upepo kiwe kimeelekea Juu na upande huo upe Jina la Mashariki,
Ule upande ulio elekea chini upe Jina la Magharibi,
Upande wa ubavu wa kulia upe Jina kaskazini na Upande wa kushoto wa mpira upe Jina la kusini.
Jenga taswira kwamba Kuna viumbe wanao ishi Kuzunguka Mpira ambao upeo wao wa uoni hauvuki mpira.
Bila shaka ile Mashariki ya Mpira haitokuwa ni Mashariki ya Dunia!
Ule Mpira hata ukiupindua juu chini ule upande wa kitundu upepo utakuwa ni Mashariki.
Ujumbe utakao wapelekea viumbe wanao ishi katika huo mpira ni kwa Mujibu wa uoni wao! Sio kwa uoni wa wanao utazama mpira!
Utatoa maelekezo viumbe wale Mashariki itakuwa ni Mashariki yao sio Mashariki ya walio nje ya Mpira!.
Bahati nzuri Maandiko matakatifu yamezingatia hali ya uoni wa watu na uhalisia wa kitu!.
Maandiko yanapo waambia watu watazame Jinsi Jua linavyo toka Mashariki kuelekea Magharibi yanazingatia kile wanacho kiona wakusudiwa ujumbe siyo walio nje yake.
Hakuna Mtu anae weza kuona Mwendo wa Mzunguko akiwa katika ardhi hii bali anaona jua likitoka Mashariki kuelekea Magharibi kwa macho safi.
Ujumbe unapo kuja kumwambia atazame unamaanisha kwa mtazamo wa aliyepo hapo si kwa mtazamo wa nje yake!
Kwa sababu ujumbe haukuletwa kwa alie nje!.
Huyo MwanaSayansi mpaka kugundua kuwa Dunia ndiyo inajizungusha katika muhimili wake kutengeneza usiku na Mchana alitoka nje ya eneo!
Ukitoka nje ya eneo husika ule ujumbe sio wako tena kwa sababu utakuwa na mtazamo tofauti haukusu na haukuletwa kwa sababu ya mtu aliye nje!
Mfano wa pili: Nakupa maelekezo kulingana na Mahali ulipo!
Kuna mti wewe unautazama Kuna chupa nimeiweka upande wa pili wa Mti Kisha nakutumia ujumbe kwa kuzingatia uoni wako na mahali ulipo kaa kwamba chupa ipo nyuma ya Mti,
Ujumbe huu kwako ni sahihi kulingana na hapo ulipo!
Lakini utakuwa ni ujumbe wa uongo ikiwa utausomea upande wa pili kwa sababu itaonekana kwako ipo mbele ya mti na si nyuma ya Mti.,
Hakuna anaweza kuona Mzunguko wa dunia akiwa anaishi katika mgongo huu wa ardhi, Hata Mwana sayansi hawezi kuthibitisha Mzunguko wa dunia ikiwa katika ardhi!
Akitaka kuthibitisha kuwa Dunia ni tufe ni lazima ushahidi wake aulete kwa mtazamo wa nje ya ardhi hii.
Sasa ujumbe wa dunia tambarare ulikuja kwa wale wanao ishi katika ardhi kwa kuzingatia uoni wao si kwa uoni wa mtu aliyetoka nje yake kwa sababu hata mtu akitembea kutaka bara moja kwenda jingine hato experience Mzunguko wa dunia.
Kwa hivyo ujumbe sahihi wa maelekezo mtu aliyoka katika mgongo wa ardhi ni dunia iliyo tambarare!.
Kwa Bahati nzuri Mungua alijua kuwa Kuna watu watakao toka nje ya Dunia na kuiona katika umbo tufe au Duara akatoa Maelezo yanayo ashiria umbile hilo katika baadhi ya aya.
Pia alitoa Maelezo ya jinsi usiku na Mchana unavyo patikana na katika maelezo hayo unapatikana ushahidi unao kubaliana na tafiti za kisayansi!
Kuwa Dunia inaumbo la Mzunguko inafanya mwendo na kujizungusha .
Hivyo Maandiko yamezingatia uoni wa Aina mbili!
Ule ujumbe unaonzungumzia Maisha na wanachomipitia watu katika Maisha unazingatia uoni wao!
Ujimbe unao onyesha kwa mtazamo wa pili ni ule unao toa dalili ya Uwepo wa Mungu kwa wafafiti.
Sasa wewe Kama hujajitosheleza kwa utafiti wako ni suala lako binafsi.
Ni kwamba hujui ku Quote mtu au dharau?Umejieleza vizuri, kutokutambua rotation na revolution ni sawa na ukiwa kwenye gari lenye speed kali, ukitazama chini hapo ulipokaa huoni gari ikikimbia kwani uko palepale ila gari linakuwa kila wakati sehemu tofauti. Hapa duniani unabaki hapo ulipo ila utashuhudia usiku na mchana, majira ya mwaka.
Sasa kama yeye ndo amekupangia kwanini Tena akuadhibu kwa kitu alichokupangia?Huenda Mungu alishapanga mtu wa motoni na Mbinguni, hakuna free Will. Ukiua mtu ilishapangwa hivyo ili upalilie moto wako. Ukitenda mema ilishapangwa hivyo ili kuandaa njia ya Mbinguni. Ila duniani wa motoni wapo wengi sana.
Kwa maelezo yako haya naomba ufafanuzi wa Mwanzo 3:22We live in the universe of 'duality'
Good|bad, juu|chini, kulia|kushoto, ukweli|uongo
MUNGU | SHETANI
Ili ulimwengu uwe balanced ilibidi MUNGU amuumbe shetani
Kosa kubwa watu hufanya kwenye majadiliano yahusuyo Imani ni kuuliza swali la MUNGU ni Nani badala ya MUNGU ni nini? Na ndicho kinachojadiliwa hapa
Kwanza kabisa tujiulize MUNGU ni nini?
Nikupe mfano huu,
MUNGU katika kusudi lake la milele kabla hajamuumba binadamu aliuliza HAKI,KWELI NA HURUMA endapo ni vema wamuumbe binadamu au lah
Haki akajibu "usimuumbe binadamu Kwa kuwa atazivunja Sheria na kanuni zako zote"
Kweli akajibu "usimuumbe Kwa kuwa binadamu atakuwa mbaya na daima atatafuta uwongo na hila( udanganyifu)
Huruma akajibu "ninajua mwanadamu atakuwa mbaya Sana lakini Mimi nitamuhifandhi na kutembea naye katika njia zake za Giza mpaka mwishowe nitamrejesha kwako"
Umejifunza nini hapa mkuu kuhusu free will mkuu?
Kuna tofauti Kati ya dhambi na nakosa.Ukifanya dhambi MUNGU hawezi kukuona maana ni mtakatikfu ,ndy maana Adam alipokula tunda, MUNGU hakumuona Adam ndy maana akauliza "Adam uko wapi"
Binafsi free will ipo limited, kuna vitu hatuna maamuzi navyo kabisa tena vinaumizafre will is illusion
Ambao mnadhania kuna free will mnijibu haya.
- wapi ulichagua kuzaliwa, unafikiri ungepewa nafasi ya kuchagua ungechagua kuzaliwa maxingira uliyopo. Why ulikuwa walia ulivyozaliwa tu
- wapi ulichagua kuwa muumini wa dini unayoabudu. Jee wazazi wako wangekuwa dini tofauti na yako uliyonayo sasa hivi, ungekuwa na dini hii unafikiri?
- kwa wale walio na magonjwa ya kurithi, hivi kuna sehemu walichagua kuwa nayo au the whole sequence of events was predetermined from moment their parents fall in love to moment they conceive.
Acha hizo bhana hivi Mimi kujua unaenda kupata ajali nimekuamulia au wewe uliamua kuendesha spidi.Twende taratibu..
Mungu anajua yote, sivyo.?
Hii inamaanisha kuwa ana uwezo wa kuona yote kabla hata hayo yote hayajaanza kutokea.
Kabla mimi sijazaliwa alishajua kuwa mimi nitakuwaje kwa kuwa yeye ajua yote, then huo utashi huru nautoa wapi wakati mimi naishi kile ambacho kilionekana kabla ya hata mimi kuwapo?