Episode 2 - Sehemu ya 4
Daudi Khan anaendelea kueleza jinsi kaka yake anavyotakatisha fedha, kuna duka linalouza bidhaa za kidini ambalo ni moja ya kampuni ya Mo Dollars Johannesburg, ambayo inatumika katika kuonesha malipo ya awali yamefanyika. Kampuni hiyo inajulikana vizuri tu katika jiji hilo, inaendeshwa na baba pamoja na mtoto wake.
Invoice ya dola 167700 inaonyesha malipo ya awali yamefanyika katika kampuni ya china Changshu City China kwaajili ya kununua mavazi ya kiislamu, bidhaa ambazo zitapelekwa kwa tarehe ya mbele iliyopangwa, lakini hakuna pesa imetumwa kwenye kampuni hiyo. Malipo haya yanayofanyika yanakuwa makubwa sana kwa kununua mzigo, yaani kwa pesa hiyo unapata nguo nyingi mno kiasi utakosa pa kuziweka na hutakuwa na watu wa kutosha kuwauzia nguo hizo, hiki ni moja ya kiashiria kinachoonesha invoice hiyo ni fake (mkikutana na malipo kama haya sehemu mtaweza kutambua hapa kuna shida pahala😃).
Picha ya invoice
Invoice ikionesha malipo ya awali kufanyika kwaajili ya mavazi ya kiislamu
Invoice inayotumwa na msambazaji ili Mo Dollars alipie bidhaa kwa pesa zake chafu nayo ni feki, account zote mbili zinazotuma pesa pamoja na kupokea (duka la kuuza bidhaa za kiislamu na msambazaji) ni za Mo Dollars! Hakuna bidhaa zinazotoka China kwenda Johannesburg lakini pesa chafu za Mo Dollars zinakuwa zimesafishwa kupitia account hiyo ya nje. Huku kwenye benk kuu kila kitu kinaonekana kipo shwari, muamala halali umepita, hakuna magendo yoyote yanafanyika.
Kutuma pesa kama malipo ya awali ni mbinu inayotumiwa sana na watakatishaji pesa, hii ni kwasababu unaweza kuhamisha pesa kirahisi nje bila kupokea mzigo kama malipo ya awalai na unakuwa na muda wa kutengeza documents za muamala huo kufanyika baadae.
Katika mazunguzo (kutoka kwenye kikao kilichofanyika kwa njia ya mtandao) yaliyorekodiwa, Mo Dollars alisikika akimtahadharisha mshirika mwenzake asifanye biashara na hasimu wao katika utakatishaji pesa, akielezea mbinu yake ya utakatishaji pesa kama biashara, na inatakiwa kuendelea kujulikana hivyo, akisema kwamba uliahidi kufanya biashara hii na sisi tu, ukianza kufanya 'biashara' hiyo na watu wengine wawili, watatu inatoa ishara mbaya.
Daud Khan ndio alikuwa mwandishi wa invoice feki, akielezea ofisini kwao kuna 'strong room', chumba kinachotimiwa kuhifadhia vitu vyenye thamani, na chumba hiko kinakuwa na ulinzi mkubwa. Daud anaelezea kwenye chumba hiko walikuwa na maboksi mengi sana yaliyojaa stempu za benki, passport pamoja na nyaraka za vitambulisho. Daudi pia ndio alikuwa anatengeneza logo, kuweka kiasi cha pesa na kila kitu kwenye invoice hizo, ambapo kwa kukadiria 90% ya rekodi kwenye kitabu cha kampuni ya Salt Management hazikuwa za kweli (halisi).
Makala inaturudisha kwa bwana Pattni, ambaye nae anaujua mchezo huu vizuri. Pattni anasema; huwezi ukaweka mayai yako yote sehemu moja, inabidi utawanyishe kwenye mafungu madogo madogo, na yeye hutawanyisha kwenye makundi madogo madogo kama 20 hivi. Wakati akiwa anaendelea kuongea na bwana Stanley, Pattni anasema yuko na network kubwa. Kwa upande wa UK ana duka la kuiza vito, group ya hotel, kampuni za bidhaa mbalimbali, kwahivyo wana uthibitisho wa sababu pindi wakituma pesa chafu nje ya nchi kama malipo ya bidhaa.
Hela zinatumwa kutoka kwenye kampuni zake za Dubai kwenda kwenye biashara zake za London na wana vitabu vyote vya rekodi hizo, hivyo ni rahisi kuthibitisha sababu ya kufanya malipo kwenye account ya nje katika mchakato wa kutakatisha pesa.
Si unakumbuka bwana Pattni ana utambulisho mwingine kama mtu wa dini anaependa kusaidia masikini, ambapo kwenye upande huu anajulikana kama brother Paul? Timu ya Al-Jazeera inafanikiwa kumpata mhasibu wa zamani wa brother Paul, Bwana Raj. Raj anasema wakati anajiunga na bwana Pattni (brother Paul) alikuwa anamuona kama mtu mwema sana, anaefanya kazi ya Mungu, lakini kituo cha msaada cha Bwana Pattni kinachoitwa Land of Hope ndio kimekuwa kikitumika kama sehemu muhimu ya kutakatishia pesa.
Raj anasema Pattini akaanza kutoa misaada na kwa watu rasmi, akificha rushwa kwenye jina la msaada, Raj ana kitabu kinachoonesha rushwa zilizofanywa na Pattini, kinaonesha malipo ya ada kwenye chuo kwaajili ya watoto wa mtu muhimu kutoka katika tawi la Benki Kuu ya Zimbabwe. Baba mwenye Watoto hao anaitwa David Chirozvi.
David Chirozvi
David anafanya kazi kwenye duka la vito la Aurex Jewellery, ambako wanatengeneza vito, lakini pia duka hilo ni sehemu ya Benki Kuu, David hapo ni Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu. Kampuni ya Pattini ya Suzan ina leseni iliyotoka Aurex, ambayo inawapa kibali cha kusafirisha vito vya dhahabu na almasi, ambapo pia kibali hicho kinajumuisha malipo ya ziada ya 18% ya mauzo kwa kampuni Suzan kutoka serikalini (si unakumbuka kuhusu malipo ya serikali kwa akina Pattini kwa kuwasaidia upatikanaji wa dola na kuruka/kukwepa vikwazo walivyowekewa na mataifa ya nje?). Kampuni ya Pattini ina leseni pia inayowawezesha kununua dhahabu kutoka wachimbaji kwa niaba ya Fidelity Printers. Mhasibu Raj anasema, kila siku Pattni anaingiza 80kg – 100kg za dhahabu.
Lengo la Leseni hizo kutolewa kwa bwana Pattni ni kwaajili ya kuhakikisha uzalishaji na mauzo ya dhahabu yanaongezeka Zimbabwe, lakini uhalisia ni kwamba wananufaika akina Pattni na maafisa waliohusika kuthibitisha mauzo ya dhahabu hizo. Jamaa ambae anasimamia kitengo cha mauzo ya dhahabu, bwana Dube, anapokea kiasi cha Dola za Kimarekani 3000 kwa mwezi kutoka kwa Pattni. Mehluleli Dube alikuwa Mkuu wa Kitego kwenye masuala ya dhahabu kutoka Fidelity Printers, na yeye ndio alikuwa na mamlaka ya kusaini ili kupata leseni kwaajili ya kuuza na kununua dhahabu.
Mehluleli Dube
Jina jingine katika kitabu cha mahesabu alichonacho Raj kinaonesha nguvu ya Bwana Pattni dhidi ya Fidelity Printers, F.Kun. Bwana huyu anapokea Dola za Kimarekani 30,000 kila mwezi kutoka kwa Pattni.
F.Kun ni nani? Tukutane katika muendelezo
Muendelezo soma -
Episode 2 - Sehemu ya 5