Gwajimanized na Samialization ya Siasa Zetu: Serikali Imelikuza la Gwajima

Kwa maoni yako ukiwa kiongozi wa dini hutakiwi kukosoa na kukemea maovu yanayoonekana kushamiri kwenye jamii unayoiongoza kiroho?

Kuna shehe mmoja maarufu wa msikiti wa Temeke aliyewahi kuwa shehe wa mkoa wa Dar es salaam Al Hadi kama sikosei Kila mara alikuwa anatoa matamko ya kisiasa hukuwahi kutoa kauli hizi au kwa kuwa anasifia watawala?

Siasa ni mahusiano ya jamii na uchumi ( social economy relation) unamtengaje raia na masuala yanayohusu maisha yake kwa mfano?

Gwajima hana kosa, kama Raia ametumia haki yake kutoa maoni ambayo wengi ikiwemo wewe tumekosa ujasiri wa kukemea na kuyasema. Hana kosa labda kama hupendezwi na haki ya kuishi ya watanzania
 
You nailed it, lakini mtoa Uzi ana majibu yake maana kwanza anajaribu kudowanplay impact ya utekaji nchini.

Kauli kwamba Kuna wengine waliishia sema ni kijinga, serikali ilitakiwa kuja na majibu siyo kiongozi mkuu kuja na vijembe na michambo wakati wananchi wanaona hali halisi.
 
Kwani siasa ni nini hadi Gwajima na viongozi wengine wa siasa hawaruhusiwi?

Askofu Bagonza amejibu swali hili mara nyingi tu, mbona hamuwasemi TEC na barua zao nyingi tu za kukemea? Au wanaogopwa? Maana imebaki kuwashambuloa akina father Kitima
 
Mpuuzi huyu wa kupuuzwa na wengine wanaomuunga tena wako humu jukwaani ambao maisha ya wanayetofautiana mtazamo siyo muhimu
 
M.M long-time !

1. Serikali haijalikuza . Ni tatizo linaloisumbua jamii kwa sasa .Wasiojulikana wana nguvu zaidi ya vyombo vya dola, nani yu salama! Mjadala wa Wananchi kupitia Bunge umezuiliwa na Spika Tulia. Gwajima tofuati na wengine ameongea kwa uwazi ''ya moyoni' kama msemaji wa Wananchi.

2. Serikali haijalikuza, bali imekosa Watu wanaofahamu ku deal na situation wakidhani hoja inaweza kutekwa, pigwa rungu, risasi na maji ya washawasha. Hawafahamu hoja inajibiwa kwa hoja na hubaki hewani na mioyoni bila shurti na daima.

3. Wasio na ufahamu ndani ya serikali ni Short sighted, hawajui wa deal vipi na situation iliyopo.
Pili ni long sighted hawajui madhara ya siku za mbeleni. Mfano, wamefungia Kanisa , je Sheikh X akisema ya Gwajima watafungia misikiti? Viongozi wana set bad precedent bila kujijua.

4. Kwamba ajiuzulu , hapana! Ni vema 'revolt' ikianzia ndani ya CCM. Angesema CHADEMA au ACT ingeonekana ni wale wanaotumiwa na mbeberu. Kutoka ndani ya CCM inaeleza jamii jambo fulani halipo sawa. Inaeleza ''resentment'' katika jamii
 
Naona hapa ni level ya juu ya upumbavu, kama alikuwa anaropoka na wewe kwa akili yako ukaona anaropoka, kuwa hakuna utekaji, upoteaji na mauaji ya watu basi mahali salama kwako ni Mirembe.
 
Gwajima mbona hajaituhumiu serikali?
Yenye mamlaka ya kuchunguza na kubaini wauaji yako kwa nani kama siyo serikali?

Anayeteua viongozi wa vyombo vya ulinzi wa usalama ni nani? Huwezi kusoma between the lines au una agenda maalum?
 
Wakati mwingine inabidi tuwe na kipimo cha kupima afya ya akili, Gwajima ametoa hoja ambazo inabidi zijibiwe, badala ya kumjibu mnamshambulia binafsi.

Hapa umetuonyesha mapungufu yake?
Great minds discuss ideas
Simple minds discuss events
And foolish minds discuss people.

Kama mna akili hata ya kuazima jibuni hoja zake
 
Ni tapeli kweli tunakubali, jibuni hoja zake nyie watekaji na wauaji.

Au mmejiunga na Idi Amin Mama kujibu mipasho na michambo badala ya hoja?

Tuanzie hapa: Kuna utekaji au hakuna?
 
Hili Jambo alizingatie Sana.Na wale WA mfano WA the late mama lwakatare wasikimbilie vitu maalum Tu ya kaisari yabaki kuwa ya kaisari na ya MUNGU yabaki kuwa ya MUNGU..Watumishi wabaki na kofia moja Tu inawatosha.
Kwa nini umzibe mdomoni asitumie haki yake ya kikatiba? Akina Bagonza, TEC, sheikh Ponda, Al Hadi, father Kitima. Unamkumbuka Mtikila?

Two wrongs don't make a right, mfumo wa uovu ulimpa ubunge that's right. Wote kwenye mfumo hawatakiwi kurepent wabaki huko huko?

Jaribuni basi kutumia akili hata za kuazima basi mtumie kujibu hoja zake
 
Kwani akina Bagonza, TEC wanafanyia kwenye mikutano ya kisiasa?

Ukiwa CCM lazima ujichatue uwe chizy
Hilo wanajifanya hawajaliona...

Gwajima moja kwa moja kaituhumu serikali na kuihusisha na utekaji.

Mbaya zaidi mashambulizi hayo anayafanyia kanisani,anaachwa VIPI?
Wewe juha wa CCM alifanya press conference, hiyo ni Moja. Kanisani aliweka sawa maana ya GWAJINIZATION

Pili mbona nyie wote machawa wa CCM hakuna hata mmoja anayejibu hoja zake? Je hakuna utekaji upoteaji na mauaji ya Raia?

Ukisema kweli unaachwaje? Mnatakiwa kupimwa afya ya akili
 
Naona hapa ni level ya juu ya upumbavu, kama alikuwa anaropoka na wewe kwa akili yako ukaona anaropoka, kuwa hakuna utekaji, upoteaji na mauaji ya watu basi mahali salama kwako ni Mirembe.
Kwahiyo, Gwajima katibu tatizo?
 
Kwahiyo, Gwajima katibu tatizo?
Kaliweka wazi tatizo, na hapo tumewajua wasiojulikana, wanaoteka watu, kuwavunja miguu, kuwapoteza na kuwaua watanzania.

Maana wamekasirika kuwekwa wazi wanataka wamdhibiti, na wewe umewajua ila dhamira yako ndio inakusaliti unaogopa kupoteza ajira yako ya buku 7
 
Kaliweka wazi sawa. Kwahiyo, way forward ni nini?
 
Kaliweka wazi sawa. Kwahiyo, way forward ni nini?
Serikali ya wauaji iwajibike siyo kutaka kuzima sauti zinazopinga mauaji yao.

Na nyinyi CHAWA wa buku 7 muanze kupaza sauti kukemea leo ni CHADEMA kesho itakuwa ndugu yako
 
Hiyo ni level ya akili yako na Gwaji boy, usituweke kwenye level zenu ambazo ni imbecelic
 
Serikali ya wauaji iwajibike siyo kutaka kuzima sauti zinazopinga mauaji yao.

Na nyinyi CHAWA wa buku 7 muanze kupaza sauti kukemea leo ni CHADEMA kesho itakuwa ndugu yako
Wenyewe mbona wanuana???
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…