DOKEZO Habari hii ikufikie Waziri wa Afya, ubabe wa Hospitali ya Muhimbili utaniua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sure. Ila wabongo kinachotuhsribia ni njaa mingi. Kwa ushauri wako watu wa ICT watakufa njaa.
 
iko hivi wewe wapigie kule hospitali ulikopewa rufaa wambie unaomba report ya ile CD , watakutumia pdf yake afu uwape muhimbili mchezo umeisha
Ila usipofanya hivo lazima ulipie hiyo hela hapo muhimbili ya kutafsiri hiyo CD
 
Mkuu Kufanya Upload ya Data ni muhimu sana Vinginevyo kama asipokubali itabidi wamcharge Pesa nyingine ya kufanya Kipimo kingine cha CT-scan...
Kwanini kwa sababu kapewa Rufaa Kwenda muhimbili na bahati nzuri kaenda akiwa na CD (Hajaiacha Nyumbani)..

Ili Daktari aweze kufanya Uchunguzi na kufanya Maamuzi kwenye mfumo wa Tiba ni lazma Data ziingie kwenye mfumo endapo Tatzo litakuwa kubwa au linahusu kitengo kingine aweze Kupass Kwenda kitengo husika ndani ya mfumo wa matibabu ..Hivyo kufanya Registration ya Matibabu ikiwemo kuandika historia yake,Vipimo na uchunguzi uliofnywa kwa Taarifa za kidaktari ni muhimu kuliko chochote kile..
Cha msingi kama ataweza aongee na ICT hapo waiupload chap au afanye njia yoyote...

Mifumo kwa sasa ya utibuji Afya haisomani....
Hilo swala lipo kwenye mchakato Though Kuna pilot kama Tatu zilishafeli kutokana na ufinyu wa mtandao na vitendea kazi
 
Wewe ni mgonjwa ujiwezi wala hujui kama kuna vifungashio vingine vinatakiwa viambatanishwe unapofanyiwa transfer...au umesahau wengine wanafanyiwa transfer wakiwa hawajiwezi na wanaoshughulikia wanakuwa hawana uelewa wowote wa hizo nyaraka, je huko Mhimbili hawana uwezo wa kuwasiliana na Hospitali iliyotoa transfer ili missing documents zitumwe? Mbona taasisi zingine wanafanya mawasiliano?
Yaani kwa akili yako timamu unadiriki kumlaumu mgonjwa kuwa amesahau nyaraka ya hospitali kwenda hospitali nyingine!!! Badala ya kutoa lawama kuwa amesahau kutumia dawa kwa wakati.

Acha kutetea upumbavu
 
iko hivi wewe wapigie kule hospitali ulikopewa rufaa wambie unaomba report ya ile CD , watakutumia pdf yake afu uwape muhimbili mchezo umeisha
Ila usipofanya hivo lazima ulipie hiyo hela hapo muhimbili ya kutafsiri hiyo CD
Hiyo niliwaomba wakanipa nayo nikauwasilisha kwa dakitari cha ajabu bado wanataka iingizwe kwenye mfumo wa Muhimbili! Na uzuri hiyo CD iko kwenye mfumo wa DVD na ni rahisi kufunguka kwenye DVD yoyote.
 
Hili tatizo si la dakitari, ni kanuni ya Muhimbili kujipatia pesa za bure.
Na kwa nini wizara haitoi mwangozo? Kwa nini seikari haifanyi unified system ya nchi nzima kwa maswala haya? Basi wazibinafsishe hospitali zote ili tujue na kufanya maamuzi magumu.
 
Naomba wote mnielewe, nilichopeleka Muhimbili ni hiyo CD iliyo kwenye mfumo wa DVD na ripoti iliyochapishwa ikionesha kinachoonekana kwenye hiyo picha ya DVD, hapa nimekamilisha kila kitu pasipo na shaka, tuanzie hapo.
 
Ni DVD na inasomeka hata nikikupa wewe utaifungua, na ripoti iliyochapishwa nimewapa.
 
Kwahili nashindwa kuitetea serikali yangu chini ya chama pendwa CCM, hao ICT walipaswa mpaka muda huu wawe majobles
 
Naomba wote mnielewe, nilichopeleka Muhimbili ni hiyo CD iliyo kwenye mfumo wa DVD na ripoti iliyochapishwa ikionesha kinachoonekana kwenye hiyo picha ya DVD, hapa nimekamilisha kila kitu pasipo na shaka, tuanzie hapo.
Mkuu mimi nimekuelewa Vizuri sana na nafikir nakuelewa pia...
Ila nina Maswali kadhaa kwako!
Ulijisajili Kam mgonjwa?
Ulipeleka rufaa ili usajiliwe kwenye mfumo?
Ulilipa Pesa ya Consultation?
Ulitoa tena maelezo juu ya ugonjwa wako?

Ukinijibu maswali haya Nitaweza kukuuliza follow up Qns na baasae nitakupa mrejesho wapi ulikuwa sawa na wapi ulikosea
 
Ni DVD na inasomeka hata nikikupa wewe utaifungua, na ripoti iliyochapishwa nimewapa.
DvD mkuu nazifahamu Na najua kuzungusha Position na pia hata kuzoom na kuzoom out..
Tatizo sio kusomeka mkuu Tatizo ni utaratibu!
Ndo maana nimeuliza maswali kadhaa ili ukiyajibu nikupe jibu
 
Kuongea na wafanyakazi wa ICT ni hujuma dhidi ya serikali, maadam nimewasilisha CD na ripoti ya kinachoonekana ndani ya DVD sioni sababu ya mimi kulipa Sh 86,000/= kwa kitu ambacho tayari nimekwisha lipia, hatutengenezi Bongo muvi.
 
Ndo nimeuliza maswali mkuu..
Ulijisajili ulipofika Hospitali nyingine?
Ulilipia pesa ya Consultation?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…