Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Hapo kwenye kuna mjadala mrefu.Kitengo cha ICT naona wana watu wendawazimu.
Kufanya Uploading ya data za kwenye CD kuziingiza kwenye mfumo ni kuijaza DATABASE bila sababu ya msingi. Kwanini Daktari asiwe na files zake yeye mwenyewe bila kuwa redirected na watu wengine? Kingine faragha ya Mgonjwa ipo wapi hapo? Maana IT anaona kila kitu.
Kwa upande wa pili, kwanini hizo Hospital za rufaa zisiwe na portal ya kutuma hizo data moja kwa moja kwa daktari wa Muhimbili? Dunia inatoka ktk physical devices hasa hzi storage devices kama vile CD.
Inatakiwa Ubunifu wa hali ya juu ktk hii ishu mifumo isomane.
Kuwezesha mifumo kuonana ndiyo Jambo rahisi na salama.
Inatakiwa mfumo uwe na API ya kuwezesha baadhi ya data kuonekana au kusomwa kwenye mifumo mingine iliyopo remote place.
Kuruhusu kila storage device kama flash disk na CD/DVD kuingizwa ovyo inaweza kusababisha mfumo kushambuliwa na virus au hackers. Kunaweza kuwa kuna embedded malicious code ndani ya hivyo vifaa.
Jasusi uchwara tu anaweza kwenda hospital kama Muhimbili na CD yake ina Trojan horse akadukua taarifa za afya ya kiongozi nyeti aliye pata matibabu hapo.tu anaweza disrupt system yao akaomba pesa kama blackmail.