DOKEZO Habari hii ikufikie Waziri wa Afya, ubabe wa Hospitali ya Muhimbili utaniua

DOKEZO Habari hii ikufikie Waziri wa Afya, ubabe wa Hospitali ya Muhimbili utaniua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kinachozungumziwa si watu ni kifaa, picha zinazopigwa Mwananyamala lazima ziaminike Muhimbili hili halina ubishi, vinginevyo ukipiga xray Mwananyamala asuhuhi na ukapelekwa Muhimbili mchana itabidi wakupige xray tena! Hapana.
X-ray unayopigwa Mwananyamala ni kwa ajili ya doctor wa Mwananyamala tuuu. Kitendo cha kupelekwa hospital ya ngazi ya juu,ni kwamba hiyo hospitali uliyopo haina uwezo wa kukupatia tiba. Kwa hiyo,kulipia hizo gharama huko Mwananyamala,hakuondoi gharama za ziada za Mhimbili.
 
Kinachozungumziwa si watu ni kifaa, picha zinazopigwa Mwananyamala lazima ziaminike Muhimbili hili halina ubishi, vinginevyo ukipiga xray Mwananyamala asuhuhi na ukapelekwa Muhimbili mchana itabidi wakupige xray tena! Hapana.
Ila mkuu kuhakika ni muhimu vipi kama wakawa wamekosea kupiga ,Vipi kama katika kupiga kuna some error zilitokea zikasababisha Hilitafu kwenye mfumo hivyo film plate ikasoma tofauti Vp kuhusu hiyo CT...
Kama DICOM files kwenye CT disc zimeonyesha picha with error au wakekupa ya mwingine kwa bahati mbaya?
Nani atakuwa Answerable kwenye hayo maswali kwa situation kama hzio unafikiri ni mwananyamala?
Vipi kama ukapima malaria Mwananyamala ,Ukienda Muhimbili watakupa Dawa?
In matter ya Uvimbe kwa wale wanatakiwa kufanyiwa op..
Vipi kama akapokea Picha au DICOM files kutoka kwingine bila kuhakika na akafanya incision na kwa bahati mbaya incision haikuwa sehemu husika na amekuwa misleaded na kipimo unafikiri akikwambia kwamba kipimo kime m-mislead utamuelewa?
 
Bro,si kwamba watu hawajaguswa.
Kuna mawili:
1. Yawezekana kukawa na kosa lako(kutokuwa nanripoti kamili au kufungua hiyo CD)
2. Yawezekana kukawa pia na kosa la mfumo wa kutoa huduma kwa hospitali husika(Mhimbili)
Yawezekana sasa labda ikawa hivi: daktali wa hospitali iliyokupa transfer,alisoma akaelewa lakini kwa msaada zaidi,akawa anawahitaji wanaomzidi uwezo. Hizo ghalama zikawa zimeishia huko.
Sasa unapoingia Mhimbili,wana utaratibu wao si kwamba gharama ulizotumia hospitali ya kwanza zina uhusiano. Unajua kuonana na doctor,hasa kama ni specialist,kuna gharama zake. Na hazikwepeki. Labda huduma au vipimo vingine.
Japo na mi bado hujaelezea vizuli. Kuna doctor mlionana akakupokea,akasoma ripoti na ndo akakwambia CD ipelekwe kitengo cha ICT?
Na mbona hata kama ni hivyo,madaktali wa levo hiyo,huwa na wasaidizi hapo wanaotumwa. Ilikuwaje ukatakiwa kupeleka mwenyewe wakati hao watu wapo?
Bila kuambiwa nipeleke nisingejua kuwa hupelekwa, ripoti kamili ya maandishi na DVD nimewasilisha na taratibu zote za malipo nimekidhi isipokuwa hilo la shs. 86,000/= sikuona uhalali wake kwani ni pesa nyingi sana kuliko nilikofanyia ct-scan.
 
Ila mkuu kuhakika ni muhimu vipi kama wakawa wamekosea kupiga ,Vipi kama katika kupiga kuna some error zilitokea zikasababisha Hilitafu kwenye mfumo hivyo film plate ikasoma tofauti Vp kuhusu hiyo CT...
Kama DICOM files kwenye CT disc zimeonyesha picha with error au wakekupa ya mwingine kwa bahati mbaya?
Nani atakuwa Answerable kwenye hayo maswali kwa situation kama hzio unafikiri ni mwananyamala?
Vipi kama ukapima malaria Mwananyamala ,Ukienda Muhimbili watakupa Dawa?
Kila kitu kilihakikiwa mara mbili na kuthibitishwa nami nilishuhudia kabla ya kukabidhiwa DVD na ripoti inayohusu muonekano wa picha.
 
Bila kuambiwa nipeleke nisingejua kuwa hupelekwa, ripoti kamili ya maandishi na DVD nimewasilisha na taratibu zote za malipo nimekidhi isipokuwa hilo la shs. 86,000/= sikuona uhalali wake kwani ni pesa nyingi sana kuliko nilikofanyia ct-scan.
Hapa naanza kukuelewa. Issue huenda sasa ikawa ni gharamankubwa si madaktari wababaifu au mfumo hafifu.
Iko hivi,hiyo ripoti na CD hazikuwa na umhimu sana kwa doctor,kwa sababu kwa maelezo ambayo ungempa au yaliyomo kwenye ripoti na CD, ulitakiwa tena ukachuguzwe kupitia hiyo machine,wapiga picha wake, na akapewa ripoti yake.
Yaani kikubwa ni kwamba ulivyofika Mhimbili,ulienda kuanza matibabu upya,si kwamba ungeendeleza matibabu. Hata kama ni dawa,ungeachishwa ulizoanza na kuendeleza ambazo ungeandikiwa. Hapo tatizo ni uelewa tu
 
Navyofahamu kuna Manager au Mkurugenzi wa ICT ambae ndio anatakiwa kuwasilisha WAZO au Ubunifu kwa Management au Bodi.

Sijakosea kuwaita wendawazimu, kuanzia Bosi mpk Maafisa.
Mawazo anaweza kuwasilisha, lakini yeye sio final sayer. Watoa maamuzi ya mwisho bado wata-prioritize mapato
 
tatizo letu wabongo hatupendi kuambiwa ukweli.! afuate utaratibu uliowekwa na mamlaka husika apate matibabu.

Leo unakuta mtu analalamika system mbovu wakati uchaguzi ukifika unamkuta na kikofia chake na litisheti likubwa la kile chama cha matapeli, useless [emoji717]
Wabongo wanafiki sana

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kila kitu kilihakikiwa mara mbili na kuthibitishwa nami nilishuhudia kabla ya kukabidhiwa DVD na ripoti inayohusu muonekano wa picha.
Kilihakikiwa na nani? Yaani unamaanisha majibu ya doctor wa hospitali hiyo,ndo hayo hayo doctor wa Mhimbili alitakiwa atumie kukutibu? Sahau. Na haitokaa itokee. Maana akikosea pia utasema alikuwa mzembe kukushughulikia akatumia ripoti ya doctor mwingine.
Hapa we lalamikia gharama,lakini vinginevyo,inaonekana hiyo 86,000 ni kianzio wala haina uhusiano na matibabu hapo
 
Kama wewe ni mtu wa ICT au utaalamu wa mifumo ya Hospitali inavyofanya kazi utagundua kuwa kila mtu amepewa acces ya Huduma kadhaa..

Kwamfano wote wanaweza kutumia mfumo huo huo mmoja ila ni vigumu Mhasibu Kuona taarifa za kitabibu kwa sababu hana acces nazo..

Na ni vigumu kwa Daktari kuona Taarifa za kihasibu kwa sababu hana acces nazo labda kama atapewa acces hiyo...

Kwahiyo daktari kumtuma aende kwa ICT anaweza akawa sahihi labda pengine Wenye uwezo wa ku-Upload taarifa hiyo ni ICT na Idara ya Mionzi (Radiology) ....lakini kumbuka Idara ya Mionzi hawawezi ku-Upload Taarifa ambayo hawakuifanyia kzi kwa hiyo inabki chance moja ambayo ni ICT pekee...
So from there nahisi wako sahihi .....

Ufinyu wa mtandao

Serkali kushirikiana na PS3 walianzisha mifumo ya Kiserkali ya Wagonjwa Na pilot yao.ilikuwa mifumo yote iwe Countrywide ...
Yaani mimi naweza kumtibu semini hapa nyanguruchiro hospitali halafu akaenda kesho Sujundu Hospitali Akakuta taarifa zake zote za alikotoka zipo..
Tatizo likawa kuna baadhi ya sehemu na maeneo kutokuwa n mtandao wa kutosha kuimili Mfumo wa internet kwa muda wote..
Kwahyo hospitali nyingi zinatumia Locahost (Offline Database) ya mfumo..Japo Kuna baadhi wana Tumia online lakini....ndo wale ukicika unaambiwa mtandao unasumbua ngoja ukae sawa tutakutibu 😅 ..
Cha msingi.. wafanye juu chini mifumo isomane. Swala la Mtandao kukosekana ni hoja yenye mashiko ila kwa ulimwengu wa sasa hakuna cha kujitetea hapo. Kuna matumizi ya Satellite Dish kuvuta mawimbi ya internet ktk maeno ya ndani ndani kabisa ni swala la investment tu.
 
Hapo kwenye kuna mjadala mrefu.
Kuwezesha mifumo kuonana ndiyo Jambo rahisi na salama.
Inatakiwa mfumo uwe na API ya kuwezesha baadhi ya data kuonekana au kusomwa kwenye mifumo mingine iliyopo remote place.

Kuruhusu kila storage device kama flash disk na CD/DVD kuingizwa ovyo inaweza kusababisha mfumo kushambuliwa na virus au hackers. Kunaweza kuwa kuna embedded malicious code ndani ya hivyo vifaa.

Jasusi uchwara tu anaweza kwenda hospital kama Muhimbili na CD yake ina Trojan horse akadukua taarifa za afya ya kiongozi nyeti aliye pata matibabu hapo.tu anaweza disrupt system yao akaomba pesa kama blackmail.
Yeah, upo sahihi kabisa.

Pia kuingiza CD mara kwa mara kunachosha ule mlango wa CD, pia kunapoteza muda na mbaya zaidi ndio hiyo ishu ya kiusalama kwa kuingiza virusi hatarishi...
 
Kila kitu kilihakikiwa mara mbili na kuthibitishwa nami nilishuhudia kabla ya kukabidhiwa DVD na ripoti inayohusu muonekano wa picha.
Mkuu nakuelewa na nimekuelewa kabisa ila Taaluma ya Udaktari haifanyi hivyo kazi....

Ntakupa mfano mmoja mdogo tu (Japo upo nje ya hapa)
Angalia: Mgonjwa amekuja akapima HIV katika kitengo cha upimaji na nasaha hospitali ya Bushungwa akapewa rufaa kwenda kitengo CTC (huduma ya Matunzo na matibabu) hapo hapo Hospitali ya Bushungwa..
Unafikiri ni kwanini kabla ya kuwa registered Lazma apimwe tena,,,,Tena n mtu mwingine tofauti na wa mwanzo..?
Unafikiri kwakuwa ni hospitali moja kwanini kupima mara mbili ?
Jibu ni dogo Refferal System hutumia majibu ya zehemu aliyotoka mgonjwa kama rejea tu na sio implementation hata kama unamjua aliyefanya na ni bora kuliko wewe...
 
Issue ya mifumo kusomana, nimeona Prof Jay, ameizungumzia sana! amegundua wekness hiyo baada ya kukaa Muhimbili mwaka na siku kadhaa.

Halii hiyo inapelekea Madaktari kukosa historia sahihi ya mgonjwa kwa tatizo linalomsumbua.
Na kuna watu wana graduate kila siku wataalam wa health systems alafu hakuna wanalofanya malofa kabisa.
 
Hahah 😅😅
Kwa tanznia Mkuu bado sana utakuta watu Wametoa taarifa nyingi za uongo humo 😅😅
Na ndo maana Daktari yupo kwa ajili ya kuverify taarifa zake za ugonjwa yeye ndo anajua kuwa ukisem dalili fulan huendaan na kitu fulani kwahyi nikikosa dalili fulin huyu sio fulan...

Unajua nilipoanza kazi niliwahi kujicheka sana kuna kipindi nilikusa najifanya kuumwa Sana nikiwa advance maana tulikuwa tunabanwa sana halafu msosi hafifu kila nikipelekwa hospitali dakktari alikuwa anacheka ananiambia dogo kachukue dawa ananipa amoxyxiline na Panadol sasa japo nilikuwa naiigiza kwelikweli nilipokuja kuingia kwenye mfumo huu nikajicheka kuona kumbe jamaa alikuwa ananichora tu anacheka anaona dogo hna anachoumwa 🤣🤣
😅 but taarifa hizo hujazi ww anayejaza ni Daktari pekee ambaye nae yupo registered humo ktk mfumo. Na huyo daktari anakuw na privileges za kuona nyuma ulitibiwa vipi yaani faili lako linazunguka ktk mifumo.
 
Sasa hapo shida ni ya hao wanaowapa malengo ya kukusanya mapato, na sio wanaopewa malengo.

Kuna watu wako kwenye upande wa management ndio wanaleta huu uozo. Na hata huwa hawaoni kabisa hizi shida wanazopata wagonjwa.
Yeye anatibiwa bure ukoo wake wote ataonaje shida? Wizara ndiyo inawapa target kulingana na population ya eneo husika including vifaa walivyo navyo.
 
😅 but taarifa hizo hujazi ww anayejaza ni Daktari pekee ambaye nae yupo registered humo ktk mfumo. Na huyo daktari anakuw na privileges za kuona nyuma ulitibiwa vipi yaani faili lako linazunguka ktk mifumo.
Sasa huo mfumo si ndo uliopo sasa Sema anayejaza ni Daktari na sio mteja
 
Kilihakikiwa na nani? Yaani unamaanisha majibu ya doctor wa hospitali hiyo,ndo hayo hayo doctor wa Mhimbili alitakiwa atumie kukutibu? Sahau. Na haitokaa itokee. Maana akikosea pia utasema alikuwa mzembe kukushughulikia akatumia ripoti ya doctor mwingine.
Hapa we lalamikia gharama,lakini vinginevyo,inaonekana hiyo 86,000 ni kianzio wala haina uhusiano na matibabu hapo
Uhakiki huu unahusu nilichopeleka kilikuwa kinanihusu mimi na picha iliyokuwemo kwenye DVD ilinihusu mimi, na hiyo gharama si ya matibabu ni ya ICT tu. Unapofanya CT-scan picha nayo inakuwa inachomwa na ukimaliza unakabidhiwa kila kitu hapo hapo kabla ya kumuanza mtu mwingine.
 
Cha msingi.. wafanye juu chini mifumo isomane. Swala la Mtandao kukosekana ni hoja yenye mashiko ila kwa ulimwengu wa sasa hakuna cha kujitetea hapo. Kuna matumizi ya Satellite Dish kuvuta mawimbi ya internet ktk maeno ya ndani ndani kabisa ni swala la investment tu.
Si walimfukuza Elon musk 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom