Bro,si kwamba watu hawajaguswa.
Kuna mawili:
1. Yawezekana kukawa na kosa lako(kutokuwa nanripoti kamili au kufungua hiyo CD)
2. Yawezekana kukawa pia na kosa la mfumo wa kutoa huduma kwa hospitali husika(Mhimbili)
Yawezekana sasa labda ikawa hivi: daktali wa hospitali iliyokupa transfer,alisoma akaelewa lakini kwa msaada zaidi,akawa anawahitaji wanaomzidi uwezo. Hizo ghalama zikawa zimeishia huko.
Sasa unapoingia Mhimbili,wana utaratibu wao si kwamba gharama ulizotumia hospitali ya kwanza zina uhusiano. Unajua kuonana na doctor,hasa kama ni specialist,kuna gharama zake. Na hazikwepeki. Labda huduma au vipimo vingine.
Japo na mi bado hujaelezea vizuli. Kuna doctor mlionana akakupokea,akasoma ripoti na ndo akakwambia CD ipelekwe kitengo cha ICT?
Na mbona hata kama ni hivyo,madaktali wa levo hiyo,huwa na wasaidizi hapo wanaotumwa. Ilikuwaje ukatakiwa kupeleka mwenyewe wakati hao watu wapo?