DOKEZO Habari hii ikufikie Waziri wa Afya, ubabe wa Hospitali ya Muhimbili utaniua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tatizo watu huwa hawaelewi wanafikiri Taaluma ya udaktari ni simple hivyo kwamba nimepokea majibu kutoka hospitali x ameandikiwa ana uvimbe kichwani bhasi na mimi bila kujiridhisha naandika Aende for Emmegency craniotomy...
Vipi ukapasua ukakuta sio Uvimbe?
 
Ct-scan na x-ray nililipia bila tatizo kwani hivyo mimi pia nilivihitaji, na Xray na CT- scan siyo sh. 86,000/= ni hela ndefu zaidi.
 
Swala la gharama za matibabu zinaanzia kwa dakitari, hizo hazikuwa tatizo kwangu kwani ukipokelewa tu unaanza kulipa. Nataka kujua uhalali wa hiyo sh 86,000/= bila jasho ni pesa nyingi sana kwa kukopi tu!
Hapa hamjaelewana. Kwanza alikopi aziweke wapi? Sasa,kama huna tatizo la kulipia, na uliambiwa watakopi CD,huo ni wizi wa wazi wazi. Tema mtupu
DR Mambo AMP , tueleweshe. Inaruhusiwa kukopi nankuhifsdhi data za mgonjwa kutoka kwenye mfumo mwingine? Na unavyojua hizo machine,hiki kitu kiko fare?
 
Ukiambiwa uvirudie tena na tena utapiga! Haujipendi na unahela za mchezo.
Kwa X-Ray kwakuwa ina low dose ya Radiation unapiga hata mara 6 kwa siku ila kaa CT scan unaweza kupiga mara mbili kwa siku hiyo ni kwa mujibu wa sheria za ALARA (as low as reasonably achievable)
 
Umeeleza vizuri

Ila huyu mgonjwa mleta mada binafsi namuona ni Mgonjwa aliyechangamka
 
Kama aliambiwa ku-Upload kwwnye mfumo ili iwe accesible kwwnye mfumo wa taarif zake za kitabibu wako sawa...
Ila kama aliambiwa wakopi CD ili wawe na copy yao kwa 86k sio sawa (japo nahisi haikuwa hivyo)
 
Tatizo siyo kutibiwa tatizo kwanini dakitari asiisome hiyo CD na kisha anitibu bila ya kutaka picha yangu iingizwe kwenye seva za Muhimbili, ili iweje.
 
Ndo kitu nilichosema mimi kwamba Watamzungusha sana kwa sababi yeye mwwnyewe anaonekana ni mbishi..
Bila kupinga ni kwamba huyu jamaa kwanza kabishana nao na kuna uwezekano kaiweka CD kwenye computer hata kabla hajaenda hospitalini aone kumewekwa nini 🤣🤣
Inaonekana pia alikuwa janja janja kujifanya anajua na ndo maana wamempa hiyo njia ndefu🤣🤣
 
Kwa X-Ray kwakuwa ina low dose ya Radiation unapiga hata mara 6 kwa siku ila kaa CT scan unaweza kupiga mara mbili kwa siku hiyo ni kwa mujibu wa sheria za ALARA (as low as reasonably achievable)
Nadhani gharama zake unazijua na kama hauzijui ulizia.
 
Na hicho ndo nilichokiona mimi Tangu mwanzo kabisa 🤣🤣
Kuna kitu kwa huyu jamaa hakipo sawa its either ana majibu mabaya kwa Watumishi au Alikuwa anajaribu kumfundisha daktari au kubisana naye kuhusu nini cha kufanya...
Maana kwa hali ya kawaida haingii akilini kabisa Kutumwa kwa IT 😅😅
Its either alitaka abaki na CD au chochote kitakuwa kilitojea angetoa muhtasari wote akasaidika
 
Kamati ya roho mbaya mpo vizuri sana

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Walioitengeneza CD ndio walionionesha ili nihakikishe iko sawa na kisha wakaifunga na kunikabidhi na taarifa zake wakaambatanisha, huo ndio utaratibu wao kwani hauwezi kuingia bila ruhusa.
 
Walioitengeneza CD ndio walionionesha ili nihakikishe iko sawa na kisha wakaifunga na kunikabidhi na taarifa zake wakaambatanisha, huo ndio utaratibu wao kwani hauwezi kuingia bila ruhusa.
Mkuu Kama ungesema ukweli kuhusu Ukivyofika muhimbili kulitokea nini?
Ulijibizana au kujaribu kumwelekeza Daktari ulimwonyesha kama unaijua CT scan au umeisoma na unajua shida yako?
 
Dadeki.

Hii picha hapa, ya mtu mmoja.
Aliugua mda mrefu,akavimba tumbo. Alienda kwa doctor,tena private,akampima akasema ana tatizo la uvimbe kwenye milija ya uzazi,na alitakiwa afanyie upasuaji kwamba kalipia uvimbe unapasuka. Na ukipasuka anakufa.

Kwa kuwa operation ilikuwa ya haraka,walitumia ripoti hiyo wakaenda hospitali kubwa na wakamuona daktari bingwa wa wanawake.
Kuna vichekesho. Akatumia ile ripoti,akaangalia kwenye X-Ray,akamlaza na kesho yake akampasua kweli.
Alipopasuliwa, doctor huyo huyo aliyepokea ripoti na kuisoma na kupiga picha tena, eti alikuta siyo uvimbe kama alivyokuwa anaona,kumbe ni kiuvimbe kimelalia tu mirija ya uzazi.
Hapo alitakiwa ahusike doctor mwingine. Akawa yupo likizo. Wagonjwa wengi wana appointment yake. Huyu,tayali wameshampasua. Walifunga na kushona,akakaa na kidonda wiki nzima.
Baada ya wiki yule doctor kaja,nae kaongeza tundu,kufika ndani,eti kitu kilichopo hajawahi kukiona. Kumbuka nae kama daktari bingwa,amecheck picha za wenzie na kupiga zake.
Nchi nzima hakukuwa na doctor wa kumtibu,ilibidi ripoti itilewe wizara ya afya akasafilishwe kwenda India.
Bahati nzuli walikuwa na doctor mgeni,akaitwa kama mtaalam kwenye kikao,kabla ya kupitisha kupelekwa,kikao kilisitishwa kwa mda,akapiga picha zake, akaona anaweza kumtibu. Kikao kiliitishwa tena, ikapangwa siku akapasuliwa kwa mara ya tatu, kikatolewa.

Sasa,haya ni badhi ya makosa madaktari wanayoyafanya,ikiwemo kuaminiana na kutofanya uchunguzi wa kina,kisa daktari furani aliona hali fulani. Huyu angekuwa simple simple,alikuwa anaondoka kwa makosa ya watu. Japo huwezi jua kikao kimeamua nini,lakini kwa vyovyote wanasutwa na kupotezewa imani.
Kwa hiyo,ni mara chache taarifa za mgonjwa kuaminiwa na doctor mwingine
 

Attachments

  • Screenshot_20231114-162755.jpg
    56.9 KB · Views: 1
Mkuu Kama ungesema ukweli kuhusu Ukivyofika muhimbili kulitokea nini?
Ulijibizana au kujaribu kumwelekeza Daktari ulimwonyesha kama unaijua CT scan au umeisoma na unajua shida yako?
Nimeshauli mimi akiacha kiburi akaomba msamaha,hata humu atapata msaada. Lakini akiendelea kuwa mbishi,ndo hivyo. Huenda alifika akatibuana na watu,sasa haemi ukweli
 
ulipofika hospitali ulipokelewa na kusajiliwa kama mgonjwa wa rufaa au ulitafuta daktari koridoni?
Nina imani hapo muhimbili kuna ofisi za kupokea malalamiko ni vyema ungieanzia hapo kabla ya kufika kwa Waziri
 
Watanzania tafuteni hela mjue huduma za afya ni gharama sana, la sivyo mtaendelea kulalamika kila siku. Matibabu siku hizi sio bure ni hela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…