DOKEZO Habari hii ikufikie Waziri wa Afya, ubabe wa Hospitali ya Muhimbili utaniua

DOKEZO Habari hii ikufikie Waziri wa Afya, ubabe wa Hospitali ya Muhimbili utaniua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu una matatizo. Mbona unataka kufanya presumptions na kuzitumia hizo presumptions kutoa hukumu? Acha kumzungusha mgonjwa; mpe tiba stahiki apone akalitumikie taifa. Cha kushangaza, watu wenye roho mbaya kama wewe huwa mnakuwa na maisha marefu sana.
Komaaaa. Tiba unayotaka apewe tofauti na kuelekezwa anachotakiwa kufanya ni nini? Short and clear. Mgonjwa anaeletwa na ambulance,huyo anakuwa amezidiwa na anapewa kipaumbele. Mgonjwa anaetembea, bado ana uwezo wa kusubiria au kuwatumia waliomsindikiza kufata taratibu. Sasa niache na roho mbaya yangu ila ukweli ndo huo. Hata nikifa leo,ukweli utabaki pale pale. Kuliko kutokwa na pavu humu,si ungeongozana nae ukamsaidie kadai haki yake?
 
Waziri wa Afya ninaandika hili kwa uchungu mkubwa na majuto ya kujitawala, mimi ninaumwa nilikwenda hosipitali ya mkoa nikafanya X-Ray na Ct-Scan, kisha nikapewa rufaa kwenda Muhimbili.

Nimeenda Muhimbili tarehe 9/11/2023 nikiwa na CD ya Ct-Scan ili daktari aicheze kuona tatizo langu, daktari hawezi kuicheza mpaka niipeleke ICT eti waikopi waiweke kwenye mfumo wa Muhimbili!

Na ili waikopi ninatakiwa nilipe sh 86,000/=? Bila hivyo nikae na CD yangu nikafilie mbali, sina hela hiyo na pia sioni uhalali wa malipo hayo kwani hiyo CD ukiweka kwenye kompyuta inafunguka haihitaji uchawi wowote ule.

Mhe. Waziri walionipa CD hiyo ni hospitali ya Serikali na niligharamia hiyo Ct- Scan kwa ajili ya madaktari wajue tatizo langu na si kwa ajili yangu binafsi ya kutengeneza Bongo muvi, hiyo CD kwangu mimi ni nyangarakasha kwani sina utaalamu wa kuisoma na nimeingia hasara ya kufanya Ct- Scan.

Kwaheri kuonana ni majaliwa.
 
Kitengo cha ICT naona wana watu wendawazimu.
Hao wa kitengo cha ICT unawaonea tu. Wao wanafuata utaratibu uliowekwa na management, ambapo wao sio sehemu ya management. Wao ni sehemu ya implementation, kama ilivyo kwa madaktari.

Wa kulaumiwa hapa ni uongozi wa hospital unaoweka hizi taratibu, na sio doctors au ICT officers.
 
Hapo kwenye kuna mjadala mrefu.
Kuwezesha mifumo kuonana ndiyo Jambo rahisi na salama.
Inatakiwa mfumo uwe na API ya kuwezesha baadhi ya data kuonekana au kusomwa kwenye mifumo mingine iliyopo remote place.

Kuruhusu kila storage device kama flash disk na CD/DVD kuingizwa ovyo inaweza kusababisha mfumo kushambuliwa na virus au hackers. Kunaweza kuwa kuna embedded malicious code ndani ya hivyo vifaa.

Jasusi uchwara tu anaweza kwenda hospital kama Muhimbili na CD yake ina Trojan horse akadukua taarifa za afya ya kiongozi nyeti aliye pata matibabu hapo.tu anaweza disrupt system yao akaomba pesa kama blackmail.
Kama hosipitali ya rufaa ya mkoa haiiaminiki na hosipitali ya rufaa ya taifa? Yaani wa mkoa waweke virusi kuishambulia ya taifa! Ili iweje, haitatokea maishani.
 
Mkuuu hata wakiona hakuna watakachofanya
Wataona aibu kwenye mioyo yao lakini wataigeuza fursa kwa kuombea maokoto kwenye bajeti ya mwakani.
Halafu wanampa Sa1:00 anairemba kuwa anataka mifumo ya hospitali isomane kuanzia zahanati ya kijiji cha kizimkazi hadi Muhimbili National Hospital
 
Shida wanapewa target ya makusanyo utadhani nao ni TRA, ni mambo ya kijinga sn
Sasa hapo shida ni ya hao wanaowapa malengo ya kukusanya mapato, na sio wanaopewa malengo.

Kuna watu wako kwenye upande wa management ndio wanaleta huu uozo. Na hata huwa hawaoni kabisa hizi shida wanazopata wagonjwa.
 
Hao wa kitengo cha ICT unawaonea tu. Wao wanafuata utaratibu uliowekwa na management, ambapo wao sio sehemu ya management. Wao ni sehemu ya implementation, kama ilivyo kwa madaktari.

Wa kulaumiwa hapa ni uongozi wa hospital unaoweka hizi taratibu, na sio doctors au ICT officers.
Navyofahamu kuna Manager au Mkurugenzi wa ICT ambae ndio anatakiwa kuwasilisha WAZO au Ubunifu kwa Management au Bodi.

Sijakosea kuwaita wendawazimu, kuanzia Bosi mpk Maafisa.
 
Mpaka sasa sijaona mtu akiguswa na hiyo gharama ya shs. 86,000/= kukopi.
 
Kama hosipitali ya rufaa ya mkoa haiiaminiki na hosipitali ya rufaa ya taifa? Yaani wa mkoa waweke virusi kuishambulia ya taifa! Ili iweje, haitatokea maishani.
Mkuu ndiyo kabisa Refferal system yoyote hutakiwi kumwamini Wa chini yako hata kama Anafanya vizuri kiasi gani kwa sababu kumbuka Hatudeal na magari kwamba Unaweza ukakosea Then umakirekebisha..kwa ni vyema kuwa care na kuanza Upya
 
KIZIMKAZI hana muda na Watanganyika zaidi y kuuza Mali zao TU. Na pia anacho weza YY kuteua na kutengua tu
 
Kitengo cha ICT naona wana watu wendawazimu.

Kufanya Uploading ya data za kwenye CD kuziingiza kwenye mfumo ni kuijaza DATABASE bila sababu ya msingi. Kwanini Daktari asiwe na files zake yeye mwenyewe bila kuwa redirected na watu wengine? Kingine faragha ya Mgonjwa ipo wapi hapo? Maana IT anaona kila kitu.

Kwa upande wa pili, kwanini hizo Hospital za rufaa zisiwe na portal ya kutuma hizo data moja kwa moja kwa daktari wa Muhimbili? Dunia inatoka ktk physical devices hasa hzi storage devices kama vile CD.

Inatakiwa Ubunifu wa hali ya juu ktk hii ishu mifumo isomane.
Issue ya mifumo kusomana, nimeona Prof Jay, ameizungumzia sana! amegundua wekness hiyo baada ya kukaa Muhimbili mwaka na siku kadhaa.

Halii hiyo inapelekea Madaktari kukosa historia sahihi ya mgonjwa kwa tatizo linalomsumbua.
 
Ni mambo ya ajabu sana kwa kweli.. au kwanini kusiwe na User portal ya Mgonjwa? Anaingia anaweka taarifa zake na kila kitu kumhusu kinabaki humo. Akienda ktk hosp nyingine wanalogin na kutrack historia ya matibabu yake.? Kuna mambo mengi ya kimfumo yanatakiwa yawe implemented
Hahah 😅😅
Kwa tanznia Mkuu bado sana utakuta watu Wametoa taarifa nyingi za uongo humo 😅😅
Na ndo maana Daktari yupo kwa ajili ya kuverify taarifa zake za ugonjwa yeye ndo anajua kuwa ukisem dalili fulan huendaan na kitu fulani kwahyi nikikosa dalili fulin huyu sio fulan...

Unajua nilipoanza kazi niliwahi kujicheka sana kuna kipindi nilikusa najifanya kuumwa Sana nikiwa advance maana tulikuwa tunabanwa sana halafu msosi hafifu kila nikipelekwa hospitali dakktari alikuwa anacheka ananiambia dogo kachukue dawa ananipa amoxyxiline na Panadol sasa japo nilikuwa naiigiza kwelikweli nilipokuja kuingia kwenye mfumo huu nikajicheka kuona kumbe jamaa alikuwa ananichora tu anacheka anaona dogo hna anachoumwa 🤣🤣
 
Shida sana hii madaktari jitahidi I kufata miiko mloapw na muwe na huruma na utu kwa wagonjwa sio fair kabisa kumsumbua mgonjwa kiasi hiki
 
Mpaka sasa sijaona mtu akiguswa na hiyo gharama ya shs. 86,000/= kukopi.
Bro, si kwamba watu hawajaguswa.

Kuna mawili:
1. Yawezekana kukawa na kosa lako(kutokuwa nanripoti kamili au kufungua hiyo CD)
2. Yawezekana kukawa pia na kosa la mfumo wa kutoa huduma kwa hospitali husika(Mhimbili)

Yawezekana sasa labda ikawa hivi: daktali wa hospitali iliyokupa transfer,alisoma akaelewa lakini kwa msaada zaidi,akawa anawahitaji wanaomzidi uwezo. Hizo ghalama zikawa zimeishia huko.

Sasa unapoingia Mhimbili, wana utaratibu wao si kwamba gharama ulizotumia hospitali ya kwanza zina uhusiano. Unajua kuonana na doctor, hasa kama ni specialist, kuna gharama zake. Na hazikwepeki. Labda huduma au vipimo vingine.

Japo na mi bado hujaelezea vizuli. Kuna doctor mlionana akakupokea,akasoma ripoti na ndo akakwambia CD ipelekwe kitengo cha ICT?

Na mbona hata kama ni hivyo, madaktali wa levo hiyo, huwa na wasaidizi hapo wanaotumwa. Ilikuwaje ukatakiwa kupeleka mwenyewe wakati hao watu wapo?
 
Mkuu ndiyo kabisa Refferal system yoyote hutakiwi kumwamini Wa chini yako hata kama Anafanya vizuri kiasi gani kwa sababu kumbuka Hatudeal na magari kwamba Unaweza ukakosea Then umakirekebisha..kwa ni vyema kuwa care na kuanza Upya
Kinachozungumziwa si watu ni kifaa, picha zinazopigwa Mwananyamala lazima ziaminike Muhimbili hili halina ubishi, vinginevyo ukipiga xray Mwananyamala asuhuhi na ukapelekwa Muhimbili mchana itabidi wakupige xray tena! Hapana.
 
Mkuu ndiyo kabisa Refferal system yoyote hutakiwi kumwamini Wa chini yako hata kama Anafanya vizuri kiasi gani kwa sababu kumbuka Hatudeal na magari kwamba Unaweza ukakosea Then umakirekebisha..kwa ni vyema kuwa care na kuanza Upya
Safi sana. Refferal ni tiketi ya kukuwezesha kuanza matibabu kwenye ngazi ya juu,si ya kufanya uendeleze matibabu kupitia kilichoonekana ulikoanzia.
 
Back
Top Bottom