Habari Njema; Nimeidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Kutoa Elimu ya Fedha

Kongole sana na Mungu akubariki.
Hili swala la usimamizi wa fedha linatakiwa kuwa somo la lazima toka shule ya msingi mpaka chuo kikuu.
 
Id nyingi zimekuja kumsapoti mleta uzi. Ni kitu kimoja kua na nadharia na ni kitu kingine nadharia kua practically doable.

Binafsi nimempongeza Kwa kutunukiwa cheti, hata kwenye maisha tunawapiongeza wanaohitimu wakati tunajua wana kazi kubwa ya kwenda kuitumia hiyo Elimu kwenye maisha Yao, hiyo ni kipengere tofauti kabisa.

Anaweza akapata hiki cheti na bado asiweze kutekeleza adhimio lake.

Kupata lesseni ya udereva jambo moja, kuwa dereva mzuri jambo lingine.

Hua naliona tatizo kidogo kwenye baadhi ya majibu yake, vinginevyo anajitahidi na yuko na bidii.

Shida nyingine ni kuamini kile anachokiamini yeye ndio suluhu ya kumfaa Kila mtu. Ukitofautiana na nadharia zake, inatokea mikwaruzano.

Kuna wapemba, wakinga na wachaga hautawaona kwenye semina yoyote ya personal finance lakini wanapesa chafu.
 
Hongera mkuu .

Kumaliza shule ndo kuanza masomo . Mitihani halisi huwa inaanza baada ya kumaliza shule. Shuleni kuna mitihani feki .
 
😄

Ova
 
Tunapiga kote kote mkuu.
Asante kwa maoni.
 
Mkuu,
Maelezo yako ni mazuri lakini umechanganya mada nyingi kwa wakati mmoja.
Kufanya kwa vitendo hakukwepeki, lakini maarifa sahihi lazima yawepo.
Wengi wanafanya sana lakini kwa kukosa maarifa sahihi wanaishia tu kukosea.
Hivyo usibeze maarifa hata kidogo.
Asante sana kwa mchango wako na karibu upate maarifa mazuri ya kifedha na kuyaweka kwenye matendo.
 
Kwa kusoma reply zako unaonekana mtu mwenye kiburi fulani
Mkuu,
Nakujibu kama unavyokuja, hivyo ukihukumu nilo ni juu yako.
Njoo sawa, nitakujibu sawa. Njoo kwa majibu ya kejeli nakujibu kwa majibu ya kejeli.
Hiyo ndiyo maana halisi ya UKIJA BILA GADI, NAGAWA WASTANI KWA IDADI.
Karibu sana mkuu.
 
Yaani anajiita coach akijibiwa asivyopenda anasema huo ni ugoro! Kwa style hiyo atamcoach mtu kweli😃
Siwezi kucoach ugoro mkuu,
Nacoach mtu anayejielewa.
Majibu yenu mnajaa kejeli halafu mkijibiwa sawa mnakuja kutafuta sympathy.
Sina hiyo mkuu, unataka matokeo njoo tufanye kazi, unataka kejeli kaa mbali.
Huwezi kuleta kejeli kwenye kitu sahihi halafu nikuchekee ili unione mnyenyekevu.
Hayo ndiyo yamefanya hili taifa kuwa masikini.
Tunapaswa kuwa straight, bullshit you name it bullshit and I don't entertain bullshiters.
 
S

Sawa sawa lakini kazi ipo ndugu kuwa tajiri au kupatq elimu juu ya jinsi ya matumizi ya pesa haitoshi hata kiduchu hata kuwa na uwezo wa kununua anyway safari njema
Kwaio tufanyeje ili tuwe matajiri mkuu?
Tupe ushauri basi, maana umesema ambayo hayawezekani hata kiduchu, tusaidie kile kinachowezekana ni kipi ili tukifanyie kazi.
Asante.
 
Asante mkuu,
Tatizo wengi hata vitabu hawajawahi kusoma ila utawasikia wanakandia vitabu.
Ni shida kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…