1. Suala hili la Mgogoro wa huko DRC (Zaire) ni Complex sana. Lina historia ndefu Sana.
Isipokuwa kuna Ukweli mchungu Sana kwamba Watu/Raia wengi wa DRC wa kutoka kwenye maeneo hayo ya pembezoni mwa nchi hiyo ikiwamo na Majimbo ya Kivu na Katanga huwa wanahesabika Kama Raia wa Daraja Pili au raia wa Daraja la mwisho kabisa kwenye nchi hiyo. Hii ni kutokana na Mfumo au Sera ya Siasa mbaya sana za Kuwagawa Watu ili Watawala wa nchi hiyo ya DRC waweze kutawala kiurahisi. Kuna tatizo la Siasa za Ubaguzi kwa Watu wa maeneo hayo ya Mashariki mwa nchi hiyo ya DRC na kuwapendelea zaidi Watu wengine wa kutoka katika maeneo mengine ya nchi hiyo. Watu wengi wa Mashariki mwa DRC kwa kiasi kikubwa Sana wanahesabika Kama siyo WaCongoman, hiki ndio chanzo kikubwa Sana Cha kuwepo kwa huo Mgogoro usiokoma, ukiachana na vyanzo vingine kama vile kuwepo kwa rasilimali nyingi sana za madini ya vito, udhaifu wa Jeshi la DRC, Udhaifu wa Utawala wa nchi hiyo ya DRC, n.k..
2. Siyo rahisi hata kidogo kulipiga na kulifurusha Jeshi la M23 kwa sababu nyingi sana. Mathalani, Watu/Wananchi wengi Sana waishio kwenye maeneo hayo ya Kivu wanawaunga mkono Wapinzani wa Utawala wa nchi hiyo ya DRC, M23 wanaungwa mkono na Wananchi. Aidha, Utawala wa nchi hiyo ya DRC ni dhaifu Sana kupita kiasi. Bad enough, hata Jeshi la nchi hiyo nalo pia ni dhaifu Sana, na pia kuna Mawakala wengi Sana wa M23 ndani ya Serikali na ndani ya Jeshi la Serikali ya DRC. Kuna vitendo vingi Sana vya Uasi wa chini chini ndani ya Jeshi la Serikali ya DRC.
3. Kwa bahati mbaya sana, hata hapa nchini Tanzania, Watu wengi wa kutoka katika mikoa ya pembezoni mwa nchi kama vile Mkoa wa Kigoma, pia wamekuwa wakichukuliwa kama ni 'Wakimbizi.' Tatizo hili lipo sana katika nchi hii, Mimi binafsi nimewahi kushuhudia mara nyingi sana mambo ya namna hii. Kuna ' bad sentiment' miongoni mwa Watu kuwaona Watu wa kutoka Kigoma kuwa ni Wakimbizi kutoka katika nchi za jirani, tatizo hili lipo katika Jamii zetu za Tanzania.