1
Isipokuwa kuna Ukweli mchungu Sana kwamba Watu/Raia wengi wa DRC wa kutoka kwenye maeneo hayo ya pembezoni mwa nchi hiyo ikiwamo na Majimbo ya Kivu na Katanga huwa wanahesabika Kama Raia wa Daraja Pili au raia wa Daraja la mwisho kabisa kwenye nchi hiyo.
Hapa ndipo tunataka kujua, wanakosa haki gani?
Kuna tatizo la Siasa za Ubaguzi kwa Watu wa maeneo hayo ya Mashariki mwa nchi hiyo ya DRC na kuwapendelea zaidi Watu wengine wa kutoka katika maeneo mengine ya nchi hiyo. Watu wengi wa Mashariki mwa DRC kwa kiasi kikubwa Sana wanahesabika Kama siyo WaCongoman, hiki ndio chanzo kikubwa Sana Cha kuwepo kwa huo Mgogoro usiokoma, ukiachana na vyanzo vingine kama vile kuwepo kwa rasilimali nyingi sana za madini ya vito, udhaifu wa Jeshi la DRC, Udhaifu wa Utawala wa nchi hiyo ya DRC, n.k..
Wanojitambulisha kama Watutsi ni wao wenyewe . Hatakujua jina la Banyamulenge!
Tanzania tuna makabila 120 wakiwemo Watusi, Wahutu n.k. Jambo moja zuri, ukijitambulisha kwa Kabila hutakuwa utaonekana kituko, at least kabla ya kuja kwa JPM.
Watu wa mashriki DRC wanajitambulisha kwa makabila ya Banyamulenge na si Wacongoman
Pili, udhaifu wa jeshi nimeueleza chanzo chake bandiko kabla ya hili
Tatu, kuhusu rasilimali hicho ndicho chanzo cha Rwanda kuitamani Kivu na Goma !
2. Siyo rahisi hata kidogo kulipiga na kulifurusha Jeshi la M23 kwa sababu nyingi sana. Mathalani, Watu/Wananchi wengi Sana waishio kwenye maeneo hayo ya Kivu wanawaunga mkono Wapinzani wa Utawala wa nchi hiyo ya DRC, M23 wanaungwa mkono na Wananchi.
Hii ni '' deja vu'' . Tumeishi na kuona mengi sana. Tuliambiwa UNITA wanapendwa sana kule Kabinda.
Tena UNITA walikuwa na msaada wa Mataifa makubwa ya magharibi kuzuia influence ya Russia na China kupitia MPLA. Nchi za SADC zilipoamua Savimbi aliondoka. Unajua mipango ilipangwa wapi! Tz
Tuliambiwa RENAMO wanapendwa sana, mwisho wa siku waliamua kuweka silaha chini.
Nguvu likuwa ya SADC
Bad enough, hata Jeshi la nchi hiyo nalo pia ni dhaifu Sana, na pia kuna Mawakala wengi Sana wa M23 ndani ya Serikali na ndani ya Jeshi la Serikali ya DRC.
I agree
3. Kwa bahati mbaya sana, hata hapa nchini Tanzania, Watu wengi wa kutoka katika mikoa ya pembezoni mwa nchi kama vile Mkoa wa Kigoma, pia wamekuwa wakichukuliwa kama ni 'Wakimbizi.' Tatizo hili lipo sana katika nchi hii, Mimi binafsi nimewahi kushuhudia mara nyingi sana mambo ya namna hii. Kuna ' bad sentiment' miongoni mwa Watu kuwaona Watu wa kutoka Kigoma kuwa ni Wakimbizi kutoka katika nchi za jirani, tatizo hili lipo katika Jamii zetu za Tanzania.
Huwezi kuilamu Tanzania kwasababu ilipokea watu zaidi ya milioni 2 kutoka maeneo ya Vita.
Kuna watu wanaingia na kujifanya ni Watanzania wakikingiwa vifua na wenzao waliotangulia.
Serikali iliamua kuwatawanya Wakimbizi waliopewa Uraia kuzuia hali hiyo
Tuna makabila ya mikoa ya Mara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga yenye mbadala Kenya.
Hatujasikia malalamiko! sababu kubwa ni ''stability' katika mipaka kama wa Kenya na TZ
Tuna Wawemba wa Zambia na Wangoni wa Malawi, hatujasikia tatizo! sababu ni stability
Upande wa magharibi lazima tuwe waangalifu, ya M23 yanaweza kutusumbua siku zijazo.
Usidhani M23 wataishia DRC, wakimalizana na DRC watahamia Tanzania!
Hii ni expansion ya Himaya!