John Wickzer Mulholland
JF-Expert Member
- Apr 13, 2023
- 6,656
- 14,403
Sidhani kama upo sahihi kuhusiana na Hoja yako hii...Mobutu pamoja na mabaya yake yote hakumwaga damu ya Wacongo kwa kiwango ambacho Kagame, Museveni, na vibaraka wao, wamefanya.
..Wacongo waliopoteza maisha tangu 1998 Kagame, Museveni,na vibaraka wao, walipovamia DRC, ni wengi kupita kiasi, na inaleta ugumu mkubwa kuitetea Rwanda, au Uganda, katika madai yao dhidi ya DRC.
Dikteta Mobutu Sese Seko aliua Watu wengi Sana nchini Zaire, hili lipo wazi kabisa.
Enzi za Utawala wake nchini Zaire, kumkosoa Mobutu Sese Seko ilikuwa ni kujikatia tiketi ya kifo.
Wakosoaji wengi sana wa Utawala wa Kidikteta wa Mobutu Sese Seko walikuwa wanatekwa hadharani na Wanajeshi wa Vikosi kazi (Abduction Squads) kutoka kwa Kikosi Maalumu Cha Kumlinda Rais na kisha unapelekwa nyumbani kwa Rais Mobutu Sese Seko kijijini kwake Gbadolite ili ukateswe na kisha kuuawa. Ndege za Jeshi na Helicopter zilikuwa hazikauki angani kwa Safari za kuwasomba Mateka kutoka katika miji mbambali iliyopo kwenye nchi hiyo ya Zaire na kuwapeleka katika Kijiji Cha Gbadolite nyumbani kwa Mobutu Sese Seko.
Hadi leo hii Watu wengi wa Nchi hiyo hawataki kwenda kuishi katika Kijiji hicho Cha Gbadolite kwa Madai kwamba ni eneo lenye laana kubwa kutokana na damu nyingi sana za Watu kumwagika hapo chini ya Utawala wa Mobutu.