Hapa unacHanganya mambo. Wahutu na Watusi wamekaa pamoja kwa karne siyo siku moja. Zaidi ya hapo nchi zao ni ndogo na jamii zao zinaishi kwa ukaribu sana. Lugha zao zinafanana kwasababu ya mwingiliano. Kule Musoma kuna Waruli, Wakwaya na Wajita. Wanaongelea lugha zinazoingiliana kwa asilimia 90! lakini hawa ni makabila tofauti
Matumizi ya neno Banyarwanda limekuzwa sana baada ya mauaji ya Kimbari. Anayehimiza ni PK kwa kuangalia mfano wa Tanzania. Kwamba ukiwa Tanzania wewe ni Mtanzania lakini haiondoi ukweli kwamba katika Tanzania kuna Wabantu, Nilotics n.k.
Kamusi ya Tanzania ni moja, Kiswahili. Mmakonde, Mngoni, Mkurya, Muha, Mchaga, Msukuma, Mmasai, Mbarabaigi, Mrangi wote wakiongea utaulizwa swali lako, tofauti ya hawa watu ni nini? Jibu lake ni kwamba wanaunganishwa na lugha lakini haindoi ukweli kwamba kuna Wabantu, Nilotic n.k.
Rwanda kuna Wahutu na Watusi, wana kamusi moja, lakini haiondoi ukweli kwamba Watusi walikuja.
Historia inasema hivyo! Bila kukubali historia hawa watu wataendelea kuuana kama ilivyotokea miaka ya 90
JokaKuu