Habari za Kiuchunguzi kuhusu Maelfu ya Askari wa Rwanda waliouawa katika mapigano ya DRC

Habari za Kiuchunguzi kuhusu Maelfu ya Askari wa Rwanda waliouawa katika mapigano ya DRC

Walisha infiltrate sana katika mifumo ya DRC kiasi kwamba ni ngumu kuwajua
Katika jeshi, wana siri zote za ulinzi na hapo ndipo tatizo lilipo.

Watu kama Kabarebe walishirikishwa serikali kwasababu waliaminiwa wanatoka mashariki ya DRC ili kuondoa hisia za kwamba eneo hilo linatengwa. Hawa akina Kabarebe ni Wazaliwa wa DRC au Raia kwa miaka mingi. Ghafla tunawaona ni viongozi wa serikali ya PK!

Banyamulenge ambao ni Wanyarwanda hata aliyezaliwa DRC mwaka 1920 bado ana link na Rwanda

CDF General J.J. Nkunda aliposema '' kuna watu wasio Rais wamepewa nafasi za maamuzi'' hayo ni kwasababu kama hizi, kwamba, utawaona ni Watanzania lakini wana link na nchi yao!

Majaluo wa Tz ni Mzawa halisi. Mmakonde ni Mzawa halisi, Mngon ini mzawa halisi. Hawana link
Si kila kabila ni hivyo hasa ya Wahamiaji wa magharibi!

Miaka michache iliyopita kuna Afisa wa Jeshi alikimbia baada ya kuhisiwa, unajua alikwenda wapi! Rwanda
Sio kwamba wanalink na nchi Yao hapana wanatumika na wanaaminishwa Kwa maslahi ya kagame na kusambaziwa propaganda kuwa wao ni watu Bora sana
 
Mkuu Historia haijawahi kuwa nzuri kwa Rwanda na Burundi. Haikuanza miaka ya 60 na 70, ilianza nyuma ya 1957. Ugomvi wa Watutsi na Wahutu una mizizi ingawa siku hizi wanasema ni ''social class'' kwamba Mhutu anaweza kuwa Mtutsi au vice versa kutokana na Utajiri, sikubaliani na dhana hii

Tatizo lilianza na Belgium, lakini pia likakuzwa baada ya Uhuru mwaka 1962 ambapo Wahutu waliwatimua Watutsi. Kuna Theories nyingi lakini moja kubwa ni kwamba Hutu ni Bantu ndio asilia na Tutsi ni Nilotic wanatoka Horn of Afrika. Ugomvi wa '' Watawala na Wageni'' ndicho chanzo
Suala la Hutu na Tutsi ni suala fulani la kihisia zaidi kuliko uhalisia na hizo hisia zote zimehengeka katika misingi siku ukisikia wanaojinasibu kuwa ni waTutsi na WaHutu wanavyoongea ndo utajiuliza tofauti zenu ni nini? Mfano Mhutu anajejiita anasalimia Amakulu, Mtutsi anasalimia Amakulu yaani ni kwamba wanakamusi moja hakuna kamusi ya Wahutu au Watutsi ila kunakamusi ya Kinyarwanda na Kirundi sasa unapoongelea habari za Ubantu mara Unilotic unakuwa umeenda nje sana hata hivyo Rwanda na Burundi kamusi zao zinaelekeana kwa asilimia 80% lakini kote kuna Watutsi na Wahutu ambao sio makabila ila ni makundi ya kujinasibu pia kuna kundi dogo sehemu zote wanaitwa Watwa.
Vita ya M23 ina lundo la habari nyuma yake na inakuwa ngumu kuikabili moja kwa moja kwa kuwa ina maslahi ya wenye nguvu ya uchumi wa Dunia nyuma yake ndo maana nchi nyingi kujiingiza moja kwa moja zinasita hasa nchi jirani
 
Kundi la wanga huwa wanajaribiana kujua je na wewe mwanga kweli au unazuga tu?

Afrika bara la ajabu sana, Angalia AU/OAU wako kimya hawahusiki, EAC-SADC wanahangaika hata sijui wananguvu kiasi gani.

Kuna majeshi ya SADC mashariki mwa Kongo, lakini M23 na DRC wanaendelea kupigana na wao wanapigwa vikumbo hadi kuuwawa, wapo wapo tu.

Hiyo AMANI wanailindaje?

Au wanamlinda nani DRC au M23?
EAC na AU ni vijiwe vya wahuni Africa Ina laana Angalia Aiti
 
Hapa ndipo tunataka kujua, wanakosa haki gani?

Wanojitambulisha kama Watutsi ni wao wenyewe . Hatakujua jina la Banyamulenge!

Tanzania tuna makabila 120 wakiwemo Watusi, Wahutu n.k. Jambo moja zuri, ukijitambulisha kwa Kabila hutakuwa utaonekana kituko, at least kabla ya kuja kwa JPM.

Watu wa mashriki DRC wanajitambulisha kwa makabila ya Banyamulenge na si Wacongoman

Pili, udhaifu wa jeshi nimeueleza chanzo chake bandiko kabla ya hili
Tatu, kuhusu rasilimali hicho ndicho chanzo cha Rwanda kuitamani Kivu na Goma !

Hii ni '' deja vu'' . Tumeishi na kuona mengi sana. Tuliambiwa UNITA wanapendwa sana kule Kabinda.
Tena UNITA walikuwa na msaada wa Mataifa makubwa ya magharibi kuzuia influence ya Russia na China kupitia MPLA. Nchi za SADC zilipoamua Savimbi aliondoka. Unajua mipango ilipangwa wapi! Tz

Tuliambiwa RENAMO wanapendwa sana, mwisho wa siku waliamua kuweka silaha chini.
Nguvu likuwa ya SADC

I agree

Huwezi kuilamu Tanzania kwasababu ilipokea watu zaidi ya milioni 2 kutoka maeneo ya Vita.

Kuna watu wanaingia na kujifanya ni Watanzania wakikingiwa vifua na wenzao waliotangulia.
Serikali iliamua kuwatawanya Wakimbizi waliopewa Uraia kuzuia hali hiyo

Tuna makabila ya mikoa ya Mara, Arusha, Kilimanjaro, Tanga yenye mbadala Kenya.
Hatujasikia malalamiko! sababu kubwa ni ''stability' katika mipaka kama wa Kenya na TZ

Tuna Wawemba wa Zambia na Wangoni wa Malawi, hatujasikia tatizo! sababu ni stability

Upande wa magharibi lazima tuwe waangalifu, ya M23 yanaweza kutusumbua siku zijazo.
Usidhani M23 wataishia DRC, wakimalizana na DRC watahamia Tanzania!

Hii ni expansion ya Himaya!
Baada ya Burundi ni Kigoma M23 wako mitano Tena subiri Pengo la Mkapa ni Kubwa
 
Sio kwamba wanalink na nchi Yao hapana wanatumika na wanaaminishwa Kwa maslahi ya kagame na kusambaziwa propaganda kuwa wao ni watu Bora sana
Hii sio kweli na ndio sababu hii vita inatokea, haki za uraia na usalama wao ndio issue sio hizi conspiracies mnazodanganyana humu, Kagame alikuwa mkimbizi for almost 30 years na walipojaribu kurudi waliambiwa nchi imejaa and you don’t belong here na wengine kuuliwa, Banyamurenge going through the same thing, acha waitafute haki yao and they don’t need your help pigeni mdomo tuu
 
Kama kagame alikuwa mkimbizi na kurudi Rwanda hao wengine wanajiona wakimbizi SI warudi Rwanda?
 
..

..maiti wamekuwa wengi mno, askari wa vyeo vya chini wanazikwa katika mass graves huko DRC.

..miili ya maofisa inayorudishwa Rwanda ina hali mbaya ya kutisha, familia zinalazimishwa kuzika bila kuonyeshwa wapendwa wao.

..Mzee Kagame amekiri "kiaina" katika moja ya hotuba zake alipogusia kwamba mchango wa askari waliopoteza maisha hautasahaulika.

..kupata taarifa nzima soma hapa chini.

Kama Rwnda wanakufa hivyo. Je, DRC itakuwaje!?
 
Suala la Hutu na Tutsi ni suala fulani la kihisia zaidi kuliko uhalisia na hizo hisia zote zimehengeka katika misingi siku ukisikia wanaojinasibu kuwa ni waTutsi na WaHutu wanavyoongea ndo utajiuliza tofauti zenu ni nini?
Hapa unacHanganya mambo. Wahutu na Watusi wamekaa pamoja kwa karne siyo siku moja. Zaidi ya hapo nchi zao ni ndogo na jamii zao zinaishi kwa ukaribu sana. Lugha zao zinafanana kwasababu ya mwingiliano. Kule Musoma kuna Waruli, Wakwaya na Wajita. Wanaongelea lugha zinazoingiliana kwa asilimia 90! lakini hawa ni makabila tofauti
Mfano Mhutu anajejiita anasalimia Amakulu, Mtutsi anasalimia Amakulu yaani ni kwamba wanakamusi moja hakuna kamusi ya Wahutu au Watutsi ila kunakamusi ya Kinyarwanda na Kirundi sasa unapoongelea habari za Ubantu mara Unilotic unakuwa umeenda nje sana hata hivyo Rwanda na Burundi kamusi zao zinaelekeana kwa asilimia 80% lakini kote kuna Watutsi na Wahutu ambao sio makabila ila ni makundi ya kujinasibu pia kuna kundi dogo sehemu zote wanaitwa Watwa.
Matumizi ya neno Banyarwanda limekuzwa sana baada ya mauaji ya Kimbari. Anayehimiza ni PK kwa kuangalia mfano wa Tanzania. Kwamba ukiwa Tanzania wewe ni Mtanzania lakini haiondoi ukweli kwamba katika Tanzania kuna Wabantu, Nilotics n.k.

Kamusi ya Tanzania ni moja, Kiswahili. Mmakonde, Mngoni, Mkurya, Muha, Mchaga, Msukuma, Mmasai, Mbarabaigi, Mrangi wote wakiongea utaulizwa swali lako, tofauti ya hawa watu ni nini? Jibu lake ni kwamba wanaunganishwa na lugha lakini haindoi ukweli kwamba kuna Wabantu, Nilotic n.k.

Rwanda kuna Wahutu na Watusi, wana kamusi moja, lakini haiondoi ukweli kwamba Watusi walikuja.
Historia inasema hivyo! Bila kukubali historia hawa watu wataendelea kuuana kama ilivyotokea miaka ya 90

JokaKuu
 
Suala la Hutu na Tutsi ni suala fulani la kihisia zaidi kuliko uhalisia na hizo hisia zote zimehengeka katika misingi siku ukisikia wanaojinasibu kuwa ni waTutsi na WaHutu wanavyoongea ndo utajiuliza tofauti zenu ni nini? Mfano Mhutu anajejiita anasalimia Amakulu, Mtutsi anasalimia Amakulu yaani ni kwamba wanakamusi moja hakuna kamusi ya Wahutu au Watutsi ila kunakamusi ya Kinyarwanda na Kirundi sasa unapoongelea habari za Ubantu mara Unilotic unakuwa umeenda nje sana hata hivyo Rwanda na Burundi kamusi zao zinaelekeana kwa asilimia 80% lakini kote kuna Watutsi na Wahutu ambao sio makabila ila ni makundi ya kujinasibu pia kuna kundi dogo sehemu zote wanaitwa Watwa.
Vita ya M23 ina lundo la habari nyuma yake na inakuwa ngumu kuikabili moja kwa moja kwa kuwa ina maslahi ya wenye nguvu ya uchumi wa Dunia nyuma yake ndo maana nchi nyingi kujiingiza moja kwa moja zinasita hasa nchi jirani
Usifananishe lugha na kabila. Lugha ni kitu unachoweza kujifunza ila kabila lina chimbuko la asili ya mtu. Hata wewe kama unaifahamu lugha yao unaweza kusalimia na kuitikia hivyo. Ila hutu na tutsi ni kabila mbili tofauti. Kwenye mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 unadhani wahutu na watutsi hawakujua nani ni mhutu na nani mtutsi?
 
Rwanda kuna Wahutu na Watusi, wana kamusi moja, lakini haiondoi ukweli kwamba Watusi walikuja.
Historia inasema hivyo! Bila kukubali historia hawa watu wataendelea kuuana kama ilivyotokea miaka ya 90
Rwanda pale hakuna amani. Kuna utulivu wa muda tu na sababu ni hiyo ya kutoshughulikia tofauti zao za kikabila. Wahutu wakishika madaraka kama walivyoshika Burundi watutsi nao hawatakubali kutawaliwa na ndio utakuwa muendelezo wa mapigano ya kikabila kati yao.
 
..

..maiti wamekuwa wengi mno, askari wa vyeo vya chini wanazikwa katika mass graves huko DRC.

..miili ya maofisa inayorudishwa Rwanda ina hali mbaya ya kutisha, familia zinalazimishwa kuzika bila kuonyeshwa wapendwa wao.

..Mzee Kagame amekiri "kiaina" katika moja ya hotuba zake alipogusia kwamba mchango wa askari waliopoteza maisha hautasahaulika.

..kupata taarifa nzima soma hapa chini.

Si mlisema wale wanyarwanda waliopo Congo ni wakaazi wa Congo ambao ni raia wa Congo ila tu wanabaguliwa kwa unyarwanda wao! Sasa inakuwaje wanapelekwa kuzikwa Rwanda? So ni ushahidi kwamba Rwanda anasapoti m23?
 
Rwanda pale hakuna amani. Kuna utulivu wa muda tu na sababu ni hiyo ya kutoshughulikia tofauti zao za kikabila. Wahutu wakishika madaraka kama walivyoshika Burundi watutsi nao hawatakubali kutawaliwa na ndio utakuwa muendelezo wa mapigano ya kikabila kati yao.
Tatizo ni Watusi wana '' superiority complex'' na Wahutu wana ''inferiority complex'' . Tazama sakata la DRC, ni Watusi wanaoleta mapigano kwamba wananyimwa haki. Ukiuliza haki gani, wanasema ya kushirikishwa serikalini!!! Wana haki zote lakini moja tu wanaitaka, kuwemo serikalini tena wakitaka asilimia

Niambie wapi ambapo Watusi wamewahi kuishi pakawa salama. Unakumbuka ya Uganda?

Mkapa aliwarudisha baada ya vita. JK naye akawarudisha katika sakata lake na PK.
Mkapa na Kikwete walifahamu wakipewa kata ipo siku watadai Wilaya n.k.

Watu wasikatae kwamba hakuna Utusi na Uhutu! lazima watu wakubali historia ili wajifunze kupitia kwalo
 
Hapa unacHanganya mambo. Wahutu na Watusi wamekaa pamoja kwa karne siyo siku moja. Zaidi ya hapo nchi zao ni ndogo na jamii zao zinaishi kwa ukaribu sana. Lugha zao zinafanana kwasababu ya mwingiliano. Kule Musoma kuna Waruli, Wakwaya na Wajita. Wanaongelea lugha zinazoingiliana kwa asilimia 90! lakini hawa ni makabila tofauti

Matumizi ya neno Banyarwanda limekuzwa sana baada ya mauaji ya Kimbari. Anayehimiza ni PK kwa kuangalia mfano wa Tanzania. Kwamba ukiwa Tanzania wewe ni Mtanzania lakini haiondoi ukweli kwamba katika Tanzania kuna Wabantu, Nilotics n.k.

Kamusi ya Tanzania ni moja, Kiswahili. Mmakonde, Mngoni, Mkurya, Muha, Mchaga, Msukuma, Mmasai, Mbarabaigi, Mrangi wote wakiongea utaulizwa swali lako, tofauti ya hawa watu ni nini? Jibu lake ni kwamba wanaunganishwa na lugha lakini haindoi ukweli kwamba kuna Wabantu, Nilotic n.k.

Rwanda kuna Wahutu na Watusi, wana kamusi moja, lakini haiondoi ukweli kwamba Watusi walikuja.
Historia inasema hivyo! Bila kukubali historia hawa watu wataendelea kuuana kama ilivyotokea miaka ya 90

JokaKuu
Eti watusi walikuja, kwa akili hii ya kipumbavu ndio maana vita haviishi then mnaishia kulaumu kina PK, una same thinking ya Tshesekedi Uber driver from Brussels, anawaambia Banyamurenge ambao wako Congo kabla ya mkoloni sio raia warudi kwao , wtf acha zipigwe tuu kitaeleweka
 
Historia ndiyo imeandika hivyo na Watusi hawajakanusha. Ikiwa ni upumbuvu basi ni wa Historia si Wasomaji
Pili, PK analaumiwa kwa kuunga mkono M23 kwa silaha na askari. Soma mada ya Uzi huu utaelewa.
Tatu, Banyamurenge walikuwepo wakati wa Mobutu, mbona hawakuwahi kubeba silaha!
Nne, Tshesekedi kuwa dereva Uber haondoi ukweli kwamba ni Rais wa DRC. Udereva wake si hoja
Tano, ikiwa Banyumulenge ni Raia haki gani wanayodai na kupelekea wabebe silaha!
 
Back
Top Bottom