The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Kama wanavyosema watu kwamba ujinga ni mtaji mkubwa sana wa Wanasiasa hasa wa Africa na zaidi Tanzania. Ukizingatia kwamba ujinga bado ni tatizo kubwa sana kwa Tanzania, wanasiasa wanachofanya ni ku'capitalize' kwenye ujinga wa Watanzania.
Mtu akishakujua wewe ni mjinga maana yake hata akiamua kukudanganya bado atafanikiwa kwa sababu wewe ni mjinga. Ujinga ni hali ya kutokujua jambo fulani, ila ukishajua unakua sio mjinga tena kwenye hilo jambo. Tatizo la Tanzania watu wengi ni wajinga karibu kwenye kila kitu hata vile vitu vya msingi ambavyo unatarajia kua mtu lazima awe anavijua kwa Tanzania bado ni tatizo.
Ujinga uliopo sasa ni wa takwimu, serikali na wanasiasa kupika takwimu ili kutetea filamu ya royal tour. Juzi nimemsikia kiongozi mmoja akisema Watalii Tanzania wamejaa hadi mwezi wa 9, yaani hoteli za Tanzania zimejaa kwa miezi 3 ijayo ziko full booked kutokana na mafanikio ya Royal Tour.
Kuna kiongozi mwingine leo kaenda mbali zaidi akasema Tanzania kwa sasa inaongoza kwa kua na watalii wengi Afrika nzima kutokana na Royal Tour.
Kwa wasiofahamu, Kabla ya Covid, Nchi iliyokua inaongoza kwa idadi ya Watalii Afrika ilikua ni South Afrika ambayo ilikua inapokea watalii milioni 16 kwa mwaka ikifuatiwa na Tunisia milioni 12 kwa mwaka. Ila baada ya Covid, South Afrika mwaka jana imepata watalii 9.5m huku ikizidiwa na Tunisia iliyopata watalii 10m. Tanzania kwa miaka yote imekua ikiambulia watalii kati ya milioni moja hadi milioni 1.8 kwa mwaka.
Turudi kwenye hoja yangu ya uongo ulipo. Kama watanzania wangekua wanajua facts chache tu ambazo ziko wazi wala wasingehangaika na maneno ya wanasiasa.
Ili ujue kama Watalii wanaongezeka Tanzania ama lah angalia thamani ya shilingi dhidi ya Dollar ya Marekani kwa kipindi cha miezi 5 iliyopita hadi leo hii June 2022.
Thamani ya shilingi imezidi kuporomoka siku hadi siku kutokana na kwamba hakuna vyanzo vya kuingiza Dollar nchini. Kwa Tanzania vyanzo pekee vya kuingiza pesa za kigeni ni utalii na mauzo ya mazao ghafi kama Korosho, Kahawa ama Pamba.
Ukiangalia takwimu za Shilingi dhidi ya Dollar, shilingi ilipanda mwezi Septemba mwaka jana hadi December kutokana na mauzo ya Korosho, msimu wa korosho ulipoisha tu Dollar imekua ikipanda kwa fujo na labda itashuka tena kuanzia Septemba mwaka huu.
Iwapo kungekua na inflow kubwa hivyo ya watalii kama inavyosemwa na wanasiasa, inflow ya Dollar ingeonyesha matokeo yake kwenye thamani ya shilingi dhidi ya Dollar. Kwa tunaojua soko la Dollar shilingi tunajua ni maneno tu ya wanasiasa maana dollar haipo kabisa sokoni.
Watanzania wengi wangekua wanajua hata hizi naked facts wanasiasa wasingekua wanathubutu kusema uongo ila kwa kua wanajua watanzania wengi ni wajinga, watasema wanachotaka kusema.
Ahsante sana.