Habari za uongo kuhusu mafanikio ya Royal Tour

U
Kama wanavyosema watu kwamba ujinga ni mtaji mkubwa sana wa Wanasiasa hasa wa Africa na zaidi Tanzania. Ukizingatia kwamba ujinga bado ni tatizo kubwa sana kwa Tanzania, wanasiasa wanachofanya ni ku'capitalize' kwenye ujinga wa Watanzania.

Mtu akishakujua wewe ni mjinga maana yake hata akiamua kukudanganya bado atafanikiwa kwa sababu wewe ni mjinga. Ujinga ni hali ya kutokujua jambo fulani, ila ukishajua unakua sio mjinga tena kwenye hilo jambo. Tatizo la Tanzania watu wengi ni wajinga karibu kwenye kila kitu hata vile vitu vya msingi ambavyo unatarajia kua mtu lazima awe anavijua kwa Tanzania bado ni tatizo.

Ujinga uliopo sasa ni wa takwimu, serikali na wanasiasa kupika takwimu ili kutetea filamu ya royal tour. Juzi nimemsikia kiongozi mmoja akisema Watalii Tanzania wamejaa hadi mwezi wa 9, yaani hoteli za Tanzania zimejaa kwa miezi 3 ijayo ziko full booked kutokana na mafanikio ya Royal Tour.

Kuna kiongozi mwingine leo kaenda mbali zaidi akasema Tanzania kwa sasa inaongoza kwa kua na watalii wengi Afrika nzima kutokana na Royal Tour.

Kwa wasiofahamu, Kabla ya Covid, Nchi iliyokua inaongoza kwa idadi ya Watalii Afrika ilikua ni South Afrika ambayo ilikua inapokea watalii milioni 16 kwa mwaka ikifuatiwa na Tunisia milioni 12 kwa mwaka. Ila baada ya Covid, South Afrika mwaka jana imepata watalii 9.5m huku ikizidiwa na Tunisia iliyopata watalii 10m. Tanzania kwa miaka yote imekua ikiambulia watalii kati ya milioni moja hadi milioni 1.8 kwa mwaka.

Turudi kwenye hoja yangu ya uongo ulipo. Kama watanzania wangekua wanajua facts chache tu ambazo ziko wazi wala wasingehangaika na maneno ya wanasiasa.

Ili ujue kama Watalii wanaongezeka Tanzania ama lah angalia thamani ya shilingi dhidi ya Dollar ya Marekani kwa kipindi cha miezi 5 iliyopita hadi leo hii June 2022.

Thamani ya shilingi imezidi kuporomoka siku hadi siku kutokana na kwamba hakuna vyanzo vya kuingiza Dollar nchini. Kwa Tanzania vyanzo pekee vya kuingiza pesa za kigeni ni utalii na mauzo ya mazao ghafi kama Korosho, Kahawa ama Pamba.

Ukiangalia takwimu za Shilingi dhidi ya Dollar, shilingi ilipanda mwezi Septemba mwaka jana hadi December kutokana na mauzo ya Korosho, msimu wa korosho ulipoisha tu Dollar imekua ikipanda kwa fujo na labda itashuka tena kuanzia Septemba mwaka huu.

Iwapo kungekua na inflow kubwa hivyo ya watalii kama inavyosemwa na wanasiasa, inflow ya Dollar ingeonyesha matokeo yake kwenye thamani ya shilingi dhidi ya Dollar. Kwa tunaojua soko la Dollar shilingi tunajua ni maneno tu ya wanasiasa maana dollar haipo kabisa sokoni.

Watanzania wengi wangekua wanajua hata hizi naked facts wanasiasa wasingekua wanathubutu kusema uongo ila kwa kua wanajua watanzania wengi ni wajinga, watasema wanachotaka kusema.

Ahsante sana.
Ukiitaka kujua Ie billion 100 italeta unafuu kiadi gani kwenye bei ya mafuta kwa waTanzania ambao tuko million 60 ni simple.: 100b/60m=1,667.
Jiulize kama wewe ukipewa sh. 1,667 /= zitakupa unafuu kiasi gani?
 
Haters hawaamini basi wamebaki kujaribu kuharibu kila kitu cha mama......kila dakika ni kujaribu, bila mafanikio, kurusha thread ya kuipondea Royal tour lakini wapi!!!!
Mi nawaangalia na kujisemea, HIIIIIIIIIIÌÌIIIIIIIIII
Kila mtu mwenye mawazo tofauti na nyinyi mnambatiza kuwa ni HATER!! Acheni upumbavu huo watu wote hatuwezi kuwa tunafikiri sawa sawa.!
 
Ni mjinga pekee ndiye huamini bila kuhoji[emoji16][emoji23][emoji23][emoji23].

Hii nchi ili kuendelea ni lazima raia wabadiri mindset zao kutoshobokea uongo wa wanasiasa ili tuone huo upumbavu wao watampa nan.

Huyu maza pamoja na genge lake wameshindwa kupika data mpaka wanasanukiwa mapema hivi?

Huyu mvaa majuba akivuka 2025 bila kung'olewa ama kujing'oa mwenyewe basi mjuwe the karma is wrong na waTz tutakuwa tumeshindikana ktk level ya uvumilivu wa Upumbavu&Ujinga.
20220603_173327.jpg
 
Upo sahihi, royal tour haijatimiza hata nusu mwaka toka itoke, hivyo ni vigumu kusema imeleta tija.
Mkuu kinachoendelea si unakisia kama sio kukiona? Maana wafuta viatu wanasema rolaytour ishaanza kuleta wageni, ilo ndilo ninalopinga Mimi sio vinginevyo na ñdiyo maana nikasema kama kuna kampuni yoyote iliyopata mafuliko ya wageni kinyume na booking za kawaida itupe ushuhuda. Tufauti wanavyotuaminisha akina mwijaku kama impact ya rolaytour imeanza kuonekana .
 
Ningeona Ana Akili sana , awe sponsor kwenye movies zinazojulikana kama Fast & Furios , Avengers kwa hiyo hela , wamtengenezee scene yenye vivutio vya Tanzania katikati ya stori ya movie

Au angefanya Digital Marketing, nchi ya Marekani Ni namba moja katika matumizi ya intaneti , So kila anayeingia mtandaoni anakutana na matangazo ya Utalii Tanzania.
Kwa hiyo Tanzania imepigwa na watanzania wenyewe? 😂
 
Wanaongea chochote kwasababu wanajua hakuna watakapoulizwa.Huyo anayesema hiyo filamu imeleta impact mapema hivi yeye ndiye kilaza kwasababu swala la utalii sio sawa na kwenda sokoni kununua nyanya.High season ndo imeanza ngoja tuone hadi decembar tutakua na wagen kiasi gani ila kwasasa ni mapema sana kuanza kuzungumzia mafanikio ya hiyo filamu.vinginevyo wanaongea kumpamba malkia ili walambe asali.
 
Kama wanavyosema watu kwamba ujinga ni mtaji mkubwa sana wa Wanasiasa hasa wa Africa na zaidi Tanzania. Ukizingatia kwamba ujinga bado ni tatizo kubwa sana kwa Tanzania, wanasiasa wanachofanya ni ku'capitalize' kwenye ujinga wa Watanzania.

Mtu akishakujua wewe ni mjinga maana yake hata akiamua kukudanganya bado atafanikiwa kwa sababu wewe ni mjinga. Ujinga ni hali ya kutokujua jambo fulani, ila ukishajua unakua sio mjinga tena kwenye hilo jambo. Tatizo la Tanzania watu wengi ni wajinga karibu kwenye kila kitu hata vile vitu vya msingi ambavyo unatarajia kua mtu lazima awe anavijua kwa Tanzania bado ni tatizo.

Ujinga uliopo sasa ni wa takwimu, serikali na wanasiasa kupika takwimu ili kutetea filamu ya royal tour. Juzi nimemsikia kiongozi mmoja akisema Watalii Tanzania wamejaa hadi mwezi wa 9, yaani hoteli za Tanzania zimejaa kwa miezi 3 ijayo ziko full booked kutokana na mafanikio ya Royal Tour.

Kuna kiongozi mwingine leo kaenda mbali zaidi akasema Tanzania kwa sasa inaongoza kwa kua na watalii wengi Afrika nzima kutokana na Royal Tour.

Kwa wasiofahamu, Kabla ya Covid, Nchi iliyokua inaongoza kwa idadi ya Watalii Afrika ilikua ni South Afrika ambayo ilikua inapokea watalii milioni 16 kwa mwaka ikifuatiwa na Tunisia milioni 12 kwa mwaka. Ila baada ya Covid, South Afrika mwaka jana imepata watalii 9.5m huku ikizidiwa na Tunisia iliyopata watalii 10m. Tanzania kwa miaka yote imekua ikiambulia watalii kati ya milioni moja hadi milioni 1.8 kwa mwaka.

Turudi kwenye hoja yangu ya uongo ulipo. Kama watanzania wangekua wanajua facts chache tu ambazo ziko wazi wala wasingehangaika na maneno ya wanasiasa.

Ili ujue kama Watalii wanaongezeka Tanzania ama lah angalia thamani ya shilingi dhidi ya Dollar ya Marekani kwa kipindi cha miezi 5 iliyopita hadi leo hii June 2022.

Thamani ya shilingi imezidi kuporomoka siku hadi siku kutokana na kwamba hakuna vyanzo vya kuingiza Dollar nchini. Kwa Tanzania vyanzo pekee vya kuingiza pesa za kigeni ni utalii na mauzo ya mazao ghafi kama Korosho, Kahawa ama Pamba.

Ukiangalia takwimu za Shilingi dhidi ya Dollar, shilingi ilipanda mwezi Septemba mwaka jana hadi December kutokana na mauzo ya Korosho, msimu wa korosho ulipoisha tu Dollar imekua ikipanda kwa fujo na labda itashuka tena kuanzia Septemba mwaka huu.

Iwapo kungekua na inflow kubwa hivyo ya watalii kama inavyosemwa na wanasiasa, inflow ya Dollar ingeonyesha matokeo yake kwenye thamani ya shilingi dhidi ya Dollar. Kwa tunaojua soko la Dollar shilingi tunajua ni maneno tu ya wanasiasa maana dollar haipo kabisa sokoni.

Watanzania wengi wangekua wanajua hata hizi naked facts wanasiasa wasingekua wanathubutu kusema uongo ila kwa kua wanajua watanzania wengi ni wajinga, watasema wanachotaka kusema.

Ahsante sana.
hivi kuna Mtanzania anaamini huo uongo wa viongozi ?
 
Mkuu kinachoendelea si unakisia kama sio kukiona? Maana wafuta viatu wanasema rolaytour ishaanza kuleta wageni, ilo ndilo ninalopinga Mimi sio vinginevyo na ñdiyo maana nikasema kama kuna kampuni yoyote iliyopata mafuliko ya wageni kinyume na booking za kawaida itupe ushuhuda. Tufauti wanavyotuaminisha akina mwijaku kama impact ya rolaytour imeanza kuonekana .
Hao ni walevi
 
Back
Top Bottom