Habari za uongo kuhusu mafanikio ya Royal Tour

Habari za uongo kuhusu mafanikio ya Royal Tour

Unavyopenda kutumia neno" mjinga," inaonyeshwa kuwa wewe utakuwa ni mtu mjinga sana, tena wa kutupwa. Nimeanza kuona ujinga wako kwa kushindwa kuelewa maana ya habari kuhusu utalii, wewe unaona habari ni shirika la utalii lililoltea watu. Hata hujui kuwa aShirrika hupelekea watu kule wanakotaka kwenda, lenyewe nlina facilitate tu. Kama kilwa mwaka huwa wanakuja lakini mwaka huu shirika sulani likafaciliatate safari zao kwa unafcuu wewe unaona hiyo ndiyo roya tua. Huo ni upumbavu es hsli ya juu sana; wapumbavu wa aina yako ndio mikipewa perememde tu basi mnaingia chumbani kwa kujisifia.
Huyo ni chawa pro Max
 
Kwa tunaojua soko la Dollar shilingi tunajua ni maneno tu ya wanasiasa maana dollar haipo kabisa sokoni.
Kwenye ishu ya inflow ya dola nakupinga ama Nina mtizamo tofauti na wewe.
Hebu type data za USD vs na sarafu zote za dunia ili tujidhirishe.
Yaani Kama benjas Ina power huwa unafaki karensi karibia zote duniani mkuu Kama hujajua.
Na ukiwa weak huwa Ni weak kwa sarafu zote.
Mnaweza mkawa mnazipata dola halafu mnazitumia nyingi sana. Ile net inakuwa zero or even minus sijui Kama unanipata.
Mfano saivi dola vs gbp Ina range 1.25++
Na hapo fiber imegain power kidogo mana Kuna muda ilikuwa 1fiber =1.214++ huyo miezi unayosema nadhani one fiber aka £ ilikuwa Ni around 1.37++USD ili uipate.
Nadhani na huo muda yen ya Japan ilifika 114.+++ Ila cheki saivi ikoje kwa rate.

In short there's are like six Fiat currencies za dunia nzima. Sasa tatu zikiwa weak tatu zingine zinakuwa strongest. And vice versa just to balance world economy
 
Utaitwa sukuma gang!

Uzuri ni kwamba hii awamu ina machawa kutoka pande zote 2. Kuna yale machawa kutoka ccm na yale ya kutoka chadema
Wa ACT tusiwataje blaza, au ndo tutakuwa wadini?
 
Utaitwa sukuma gang!

Uzuri ni kwamba hii awamu ina machawa kutoka pande zote 2. Kuna yale machawa kutoka ccm na yale ya kutoka chadema
Sukuma gang unatapatapa sana. Upigaji ulikuwepo hata wakati wa lile chizi LENU la kisukuma msituchoshe.
Ndege kununuliwa bila sheria manunuzi haikuwa wizi?
Kujenga uwanja wa ndege kwa kampuni yake bila kupitishwq na bunge haikuwa upigaji?
Tenda ta bwqwq la mwl nyerere haikuwa na upigaji?
Brigedia mbung'o alirudi toka kusini na makapu ya pesa nyumbani kwake yule mbung'o aliteuliwa na SSH?
 
Haters hawaamini basi wamebaki kujaribu kuharibu kila kitu cha mama......kila dakika ni kujaribu, bila mafanikio, kurusha thread ya kuipondea Royal tour lakini wapi!!!!
Mi nawaangalia na kujisemea, HIIIIIIIIIIÌÌIIIIIIIIII
Kwa hiyo uongo unaoendelea huuoni? Basi wakikuita mjinga usishangae!
 
Kama wanavyosema watu kwamba ujinga ni mtaji mkubwa sana wa Wanasiasa hasa wa Africa na zaidi Tanzania. Ukizingatia kwamba ujinga bado ni tatizo kubwa sana kwa Tanzania, wanasiasa wanachofanya ni ku'capitalize' kwenye ujinga wa Watanzania.

Mtu akishakujua wewe ni mjinga maana yake hata akiamua kukudanganya bado atafanikiwa kwa sababu wewe ni mjinga. Ujinga ni hali ya kutokujua jambo fulani, ila ukishajua unakua sio mjinga tena kwenye hilo jambo. Tatizo la Tanzania watu wengi ni wajinga karibu kwenye kila kitu hata vile vitu vya msingi ambavyo unatarajia kua mtu lazima awe anavijua kwa Tanzania bado ni tatizo.

Ujinga uliopo sasa ni wa takwimu, serikali na wanasiasa kupika takwimu ili kutetea filamu ya royal tour. Juzi nimemsikia kiongozi mmoja akisema Watalii Tanzania wamejaa hadi mwezi wa 9, yaani hoteli za Tanzania zimejaa kwa miezi 3 ijayo ziko full booked kutokana na mafanikio ya Royal Tour.

Kuna kiongozi mwingine leo kaenda mbali zaidi akasema Tanzania kwa sasa inaongoza kwa kua na watalii wengi Afrika nzima kutokana na Royal Tour.

Kwa wasiofahamu, Kabla ya Covid, Nchi iliyokua inaongoza kwa idadi ya Watalii Afrika ilikua ni South Afrika ambayo ilikua inapokea watalii milioni 16 kwa mwaka ikifuatiwa na Tunisia milioni 12 kwa mwaka. Ila baada ya Covid, South Afrika mwaka jana imepata watalii 9.5m huku ikizidiwa na Tunisia iliyopata watalii 10m. Tanzania kwa miaka yote imekua ikiambulia watalii kati ya milioni moja hadi milioni 1.8 kwa mwaka.

Turudi kwenye hoja yangu ya uongo ulipo. Kama watanzania wangekua wanajua facts chache tu ambazo ziko wazi wala wasingehangaika na maneno ya wanasiasa.

Ili ujue kama Watalii wanaongezeka Tanzania ama lah angalia thamani ya shilingi dhidi ya Dollar ya Marekani kwa kipindi cha miezi 5 iliyopita hadi leo hii June 2022.

Thamani ya shilingi imezidi kuporomoka siku hadi siku kutokana na kwamba hakuna vyanzo vya kuingiza Dollar nchini. Kwa Tanzania vyanzo pekee vya kuingiza pesa za kigeni ni utalii na mauzo ya mazao ghafi kama Korosho, Kahawa ama Pamba.

Ukiangalia takwimu za Shilingi dhidi ya Dollar, shilingi ilipanda mwezi Septemba mwaka jana hadi December kutokana na mauzo ya Korosho, msimu wa korosho ulipoisha tu Dollar imekua ikipanda kwa fujo na labda itashuka tena kuanzia Septemba mwaka huu.

Iwapo kungekua na inflow kubwa hivyo ya watalii kama inavyosemwa na wanasiasa, inflow ya Dollar ingeonyesha matokeo yake kwenye thamani ya shilingi dhidi ya Dollar. Kwa tunaojua soko la Dollar shilingi tunajua ni maneno tu ya wanasiasa maana dollar haipo kabisa sokoni.

Watanzania wengi wangekua wanajua hata hizi naked facts wanasiasa wasingekua wanathubutu kusema uongo ila kwa kua wanajua watanzania wengi ni wajinga, watasema wanachotaka kusema.

Ahsante sana.
Hilo nalo NENO! In fwakti WAJINGA NI WANASIASA WENYEWE SIO RAIA! Maana kama mtu mwenyewe kaamua kuuzunguka ukweli ulio wazi kabisa kisha akaupindisha kwa sababu moja au nyingine si basi! Mjinga ni yeye mwenyewe tu! Kwani ni watanzania wangapi wanaofaidika na biashara ya Utalii nchini?! Kidogo sana; kwa hiyo utalii ukipanda au kudumaa kunawasaidia kitu gani? Wanasiasa wanajichua na kukojoa wenyewe; wananchi wanawaangalia wanavyodemka basi; na maisha yataendelea tu![emoji91][emoji91]
 
lakini wale wazanzibari waliowamwagia tindikali watalii kule zanzibar nadhani wametuhalibia sana swala la watalii kujazana Tanzania. sijui waliakamtwa au bado wapo mafichoni mpaka leo.
 
Timing mbovu, unaanzaje kushawishi watu ambao janga la covid limewavurugia uchumi tayari. Watu wako kwenye recovery time wewe unaleta royal tour yakishamba.

Inflation ilioletwa na crisis ya Covid 19 ulimwenguni imewafelisha vibaya.
 
Unavyopenda kutumia neno" mjinga," inaonyeshwa kuwa wewe utakuwa ni mtu mjinga sana, tena wa kutupwa. Nimeanza kuona ujinga wako kwa kushindwa kuelewa maana ya habari kuhusu utalii, wewe unaona habari ni shirika la utalii lililoltea watu. Hata hujui kuwa aShirrika hupelekea watu kule wanakotaka kwenda, lenyewe nlina facilitate tu. Kama kilwa mwaka huwa wanakuja lakini mwaka huu shirika sulani likafaciliatate safari zao kwa unafcuu wewe unaona hiyo ndiyo roya tua. Huo ni upumbavu es hsli ya juu sana; wapumbavu wa aina yako ndio mikipewa perememde tu basi mnaingia chumbani kwa kujisifia
Huyo jamaa ni chawa mwandamizi, atasifia jambo lolote linalo connect na bi tozo. Hata liwe la hovyo kiasi gani ila atalipamba tu😂 ndio shuguli inayompeleka yeye na familia yake maliwatoni.
 
Haters hawaamini basi wamebaki kujaribu kuharibu kila kitu cha mama......kila dakika ni kujaribu, bila mafanikio, kurusha thread ya kuipondea Royal tour lakini wapi!!!!
Mi nawaangalia na kujisemea, HIIIIIIIIIIÌÌIIIIIIIIII
Weka facts mzee mbona mtoa mada kaweka
 
Watanzania wengi wangekua wanajua hata hizi naked facts wanasiasa wasingekua wanathubutu kusema uongo ila kwa kua wanajua watanzania wengi ni wajinga, watasema wanachotaka kusema.
'The Evil Genius', inatisha!

Mkuu, ni mara yangu ya kwanza kukusoma, na niko 'impressed' na andiko lako.

Kuna mambo kadhaa umeyaandika, moja likiwa hilo la "ujinga" wa waTanzania. Umeelezea maana ya hilo neno, 'ujinga', kuwa ni kutofahamu juu ya jambo fulani.

Kwa hiyo hapa ni kama inaonekana kuwa waTanzania ni 'perpetual' wajinga, yaani ni wajinga wa kudumu, siyo katika jambo hili pekee, bali katika mambo mengi tu yanayokusudiwa na serikali kuwapotosha (kuwajaza ujinga) juu yake!

Mbaya zaidi ni kama taasisi zinazotakiwa kuondoa huu ujinga kwa wananchi, nazo ni kama zinashiriki katika kuwajaza ujinga waTanzania.
Hapa ningependa kutumia mfano wako wa utalii kuelezea ujinga wanaopata waTanzania, na hawatakiwi kuondokana na ujinga huo.

Tuna taasisi yetu ya takwimu. Hivi kazi ya hawa watu ni ipi hasa, maana binafsi sioni au kusikia wakitoa taarifa za takwimu mbalimbali kwa wananchi, kama za hao watalii wanaoingia nchini mwetu.
Kutofanya hivyo, ni sawa na kusema wao ndio wanaoruhusu wanasiasa wawajaze ujinga waTanzania kwa kutoa taarifa za uongo

Kwa hiyo, washirika muhimu wanaotakiwa kulaumiwa mwanzo kabisa ni hawa watu tunaowalipa watufanyie kazi, na badala yake wanaruhusu tujazwe ujinga.

Pili, ujinga walionao waTanzania kusema kweli ni 'upumbavu', na siyo ujinga tena. Mtu mjinga huweza kujielimisha kwa kila njia anayoweza kuitumia na kuondoa ujinga. Hawa waTanzania wetu wameridhika kabisa kuambiwa uongo, na hawajishughulishi kabisa na kutafuta ukweli. Huu ni upumbavu na wanasiasa(?) wanapenda sana watu wa aina hii

Tatu, Tanzania tumeingia kwenye hali ambayo tunaweza kuendelea kuwatambua hawa watu wanaosema uongo kuwa ni wanasiasa. Hawa ni matapeli, na mbaya zaidi ni kuwa waTanzania hawastuki kwamba wanatapeliwa
Ni siasa gani zinazoruhusu hadi mkuu wa nchi akiwa ni maiti, halafu viongozi wenzake wanasema ni mzima anachapa kazi!
Na waTanzania walivyo, wanashangilia kupata taarifa kama hiyo. Kama si upumbavu huo, tuuite kitu gani?
 
Niletee EuroWings kutoka ujerumani kwa miaka ya nyuma sio kuropoka kama kasuku
Eurowings ni ndege iliyokodishwa na kampuni la utalii kuwaleta Tanzania mwaka huu, miaka mingine huwa wanakodi ndege nyingine. Kwa mfano miaka miwili iliyopita (kabla ya Covid) waliletwa na ndege zisizopungua tatu KLM, Ethiopian, na Turkish. Watalii huwa wanaplani safari hizo kwa muda mrefu, siyo kama safari za daladala kuwa umesikia roya tua majuzi tu, basi leo unaondoka. Usidhani kuwa wana dimbwi la pesa la kuchota na kuondoka kwenda kutumia bali huwa wanasevu kwa muda mrefu, normally miezi kama nane au tisa hivi.
 
Eurowings ni ndege iliyokodishwa na kampuni la utalii kuwaleta Tanzania mwaka huu, miaka mingine huwa wanakodi ndege nyingine. Kwa mfano miaka miwili iliyopita (kabla ya Covid) waliletwa na ndege zisizopungua tatu KLM, Ethiopian, na Turkish. Watalii huwa wanaplani safari hizo kwa muda mrefu, siyo kama safari za daladala kuwa umesikia roya tua majuzi tu, basi leo unaondoka. Usidhani kuwa wana dimbwi la pesa la kuchota na kuondoka kwenda kutumia bali huwa wanasevu kwa muda mrefu, normally miezi kama nane au tisa hivi.
Umejaa funza kichwani.
 
Jiangalie vyema unakurupuka na matusi huna hoja chawa papasi
Wewe Pinga Pinga utakuwa na hoja kweli?

Haya ropoka na kupinga na hapa 👇
 

Attachments

  • Screenshot_20220701-162839.png
    Screenshot_20220701-162839.png
    99 KB · Views: 3
  • Screenshot_20220628-090709.png
    Screenshot_20220628-090709.png
    239.5 KB · Views: 3
  • Screenshot_20220628-090518.png
    Screenshot_20220628-090518.png
    174.2 KB · Views: 4
Back
Top Bottom