Hai: Waliorusha mawe kwenye mkutano wa Lissu mkoani Kilimanjaro wakamatwa

Hai: Waliorusha mawe kwenye mkutano wa Lissu mkoani Kilimanjaro wakamatwa

Umeambiwa walikimblia Arusha ambako Godblrss Lema ni Mbunge na Kwao Ni Hai Gari ya Lisu ilikotupiwa mawe

Ikumbukwe Arusha kwa Lema ndiko ofisi ya Chadema ilichomwa Moto.

Connect dots Ni Nani alikuwa nyuma ya hao wachoma ofisi na kutupia mawe magari ya Lisu ili wapate kura za huruma na huruma ya kimataifa

Hahahahaha nimekuelewa Sana. Sema sisi Wana CCM kuna muda tunajigeuza mazuzu
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👍🏽

Wale polisi walio act kama spectators badala ya kutimiza wajibu wao wa kulinda usalama wamechukuliwa hatua zipi?

Mkuu wa wilaya ambaye ni mwenyekiti kamati ya ulinzi na usalama je?
Lile halikuwa tukio dogo.
 
Chadema wanaigiza kuchoma ofisi moto na kutupia magari Yaao wenyewe mawe kutafuta kura za huruma
Polisi wanafanyia uchunguzi tukio hilo na wamekamata hao 12 na wengine kukimbia. Sasa kwa vile wewe unawajua hao watu wa Chadema waliochona moto, itabidi Polisi wakutafute au Uende kituoni ukatoe hizo taarifa za hao watu ili wakamatwe. Naamini kama una akili zote kichwani huwezi ropoka usichokijua.

YEHODAYA
 
Yule mwenye ubini wa Jabir mbona yuko pale kwao? Halafu nyau YULE.... mijitu ile na wewe wapi na wapi?
 
Kawaida Polisi ikiwakamata watu kama hao wanatajwa majina,umri na kabila mbele ya press conference,je hilo limefanyika?

Polisi wanawaogopa ccm kuliko unavyofikiri.
 
Safari hii kitawakaa hatutaki mchezo na wezi wa kijani. Kuonewa sasa baathi. Umeshindwa kufanya siasa za ushindani rudi kwenu chatle kachunge ng'ombe ukisubiria kukabidhiwa ICC.
Hakitawaka chochote. Hakuna Mtanzania mwenye nia au uwezo wa kufanya lolote. Tumeizoea amani
 
Hakitawaka chochote.Hakuna Mtanzania mwenye nia au uwezo wa kufanya lolote.Tumeizoea amani
Vyombo vya dola na tume wana nia ovu. Ona wapinzani wana kamatwa ati wamesababisha maandamano lakini wagombea wa Ccm wana sindikizwa na gari za polisi.

Wasimamizi wa uchaguzi wana toa fomu za wagombea wa Upinzani kwa mamluki wa Ccm. Huu wote ni mwanzo wa machafuko
 
NEWS: WALIOMSHAMBULIA LISSU KWA MAWE WAKAMATWA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ACP Emmanuel Lukula amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 12 wanaodaiwa kufanya vurugu za kushambulia kwa mawe, mkutano wa mgombea Urais wa chama cha upinzani Chadema Tundu Lissu Wilayani Hai siku za hivi karibuni.


"Tumetumia sana intelejensia ya Polisi ili kuwabaini hao watu waliofanya kitendo hicho cha aibu kubwa tumefanikiwa kuwapata 12, wengine tumewakamatia Arusha wanasema baada ya hilo tukio waliona kama wangerudi majumbani mwao wangekamatwa, tumewafuatilia kwa muda mrefu lakini tumeona tuwafuate walipo, mbaya zaidi wanatueleza kuwa kuna mtu aliyekuwepo nyuma yao na amekimbia" amesema Kamanda Lukula leo Agosti 23, 2020

Agosti 14 mwaka huu Lissu alikwenda Mkoani Arusha kusaka wadhamini ili kukidhi masharti ya Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Sheria za Uchaguzi zinavyotaka, kuwa lazima upate wadhamini 200 kutoka mikoa 10 ya Tanzania.

Wakati Lissu na Msafara wake wanakaribia kufika kwenye Ofisi za Chama chake cha Chadema wilayani hai, alishambuliwa kwa mawe na genge la watu walioibuka ndani ya msafara huo.

Aliyekuwa Mbunge Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Twitter alitoa taarifa punde baada ya tukio hilo kuwa msafara wa Tundu Lissu umevamiwa katika Ofisi za Chama hicho Wilayani Hai

"Msafara wa mgombea Urais Mh Tundu Lissu umevamiwa na kushambuliwa vibaya katika ofisi ya CHADEMA HAI,magari yame haribiwa. Mgombea Uraisi na Team yake wako salama. Polisi wako lakini wana shuhudia, mkutano umevunjika. Alisema Lema
 
Polisi wamemkamata bosi wao wa kamati ya ulinzi wilaya Mhe. DC. Yeye ndiye tatizo.
 
Polisi wamemkamata bosi wao wa kamati ya ulinzi wilaya Mhe. DC. Yeye ndiye tatizo.
Kweli? Hapo watakuwa wamelitendea haki jeshi la polisi kama Sabaya yuko selo
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Kama ni kweli hao waliokamatwa ndo wahusika, basi ni jambo jema, maana yawezekana ni watu wengine wametolewa kafara tu.

Huyo aliyekuwa nyuma yao akakimbia inaelekea ana speed sana kuliko vyombo vya dola, na ndiyo maana hawataki hata kutaja jina lake. Nafikiri ni DC SABAYA

Hakuna mtu yoyote aliyekamatwa, bali ni utapeli kama utapeli mwingine. Kama DC na polisi waliosimamia huo uhuni bado wako ofisini basi huo ni usanii tu.
 
Bado kamanda hajaeleweka, amesema baada ya kuwakamata vijana hao waliofanya vurugi, waliwaoji na vijana hao wakasema kuna mtu nyuma yao ila amekimbia sasa ina maana chombo cha dola kimeshindwa kuwabana hao vijana ili wamtaje uyo aliyewatuma?
 
Umeambiwa walikimblia Arusha ambako Godblrss Lema ni Mbunge na Kwao Ni Hai Gari ya Lisu ilikotupiwa mawe

Ikumbukwe Arusha kwa Lema ndiko ofisi ya Chadema ilichomwa Moto.

Connect dots Ni Nani alikuwa nyuma ya hao wachoma ofisi na kutupia mawe magari ya Lisu ili wapate kura za huruma na huruma ya kimataifa
Ugoro mtupu
 
Back
Top Bottom