Hai: Waliorusha mawe kwenye mkutano wa Lissu mkoani Kilimanjaro wakamatwa

Hai: Waliorusha mawe kwenye mkutano wa Lissu mkoani Kilimanjaro wakamatwa

Yawezekana "kukamatwa" kwa waliofanya fujo kwenye msafara wa Lissu ni propaganda ya kujisafisha tu lakini sio kwa nia ya halisi ya kulinda usalama. Kwa sasa dunia nzima inatuangalia kwahiyo sitoshangazwa kama walikuwa wanatuhadaa tu na kutufanya sisi na jumuiya za kimataifa ni mazuzu. Kesho na keshokutwa wakienda kuomba misaada watasema hao watu walichukuliwa hatua kumbe ni maigizo tu.

Mpaka hao waliofanya fujo wakifungwa ndio nitaamini kweli haki inatendeka.
 
Umeambiwa walikimblia Arusha ambako Godbless Lema ni Mbunge na Kwao Ni Hai Gari ya Lisu ilikotupiwa mawe

Ikumbukwe Arusha kwa Lema ndiko ofisi ya Chadema ilichomwa Moto.

Connect dots Ni Nani alikuwa nyuma ya hao wachoma ofisi na kutupia mawe magari ya Lisu ili wapate kura za huruma na huruma ya kimataifa
Kwahiyo makada wa ccm ndiyo tunatakiwa kuunganisha dot kwao...! Mbona mnatufanya tunakwazika kwa kutufanya hatuna akili.
 
Inawezekana ikawa maigizo tu, tungeona hata majina yao yakitajwa ndipo tungeanza kuaamini. Lakini kinachofanyika ni porojo tu.
 
Wawekwe hadharani kama watuhumiwa wengine kisha washtakiwe na kuhukumiwa haraka ikiwezekana chini ya hati ya dharura na kupewa vufungo vigumu ili iwe MFANO NA FUNDISHO kwa wengine wenye tabia kama hizo kipindi hiki cha uchaguzi mkuu

Kwa kufanya hivyo tutaiona NIA YA DHATI ya mamlaka katika kupambana na wahuni
 
Kakamate na we we unaowafahamu. Sijui nyie mnashidaaa ganiiii. Polisi wakifanya kazi hamuwaaminii wakikaaa kimyaaa mnalalamikaaa, sasa mnataka iwejeee? Basi jitokeze uisaidie polisi kukamata wewe unaowajua.
 
Siro ...ICC utaikwepaje awamu hii? Mikono yenu michafu hata ukiomba kupumzika too late mikono kunuka damu tayari .....!! Hizi sinema za kitoto!
 
Uko sahihi kabisa, huyu Sabai amewafanyia wapinzani maafa/mauaji/ukatili mkubwa bila kukemewa, the implication of which is that the higher authority is behind him! Ana kibali cha Mfalme kufanya haya anayoyafanya. Hii ya kujitia kuwakamata hawa vijana ni gheresha tu kujikosha mbele ya macho ya dunia!
 
Wawekwe hadharani kama watuhumiwa wengine kisha washtakiwe na kuhukumiwa haraka ikiwezekana chini ya hati ya dharura na kupewa vufungo vigumu ili iwe MFANO NA FUNDISHO kwa wengine wenye tabia kama hizo kipindi hiki cha uchaguzi mkuu
Kwa kufanya hivyo tutaiona NIA YA DHATI ya mamlaka katika kupambana na wahuni

Nashangaa sana TL hajalizungumzia hili hadharani. Wanafanya hizi porojo ili hasa kuwadanganya wafadhili wa nchi.
 
Wawekwe hadharani kama watuhumiwa wengine kisha washtakiwe na kuhukumiwa haraka ikiwezekana chini ya hati ya dharura na kupewa vufungo vigumu ili iwe MFANO NA FUNDISHO kwa wengine wenye tabia kama hizo kipindi hiki cha uchaguzi mkuu
Kwa kufanya hivyo tutaiona NIA YA DHATI ya mamlaka katika kupambana na wahuni
Hatuwez kuwahukumu kwa sababu baadhi yao ni watu wa kitengo na walokuwa ktk special task siku hiyo
 
Uko sahihi kabisa, huyu Sabai amewafanyia wapinzani maafa/mauaji/ukatili mkubwa bila kukemewa, the implication of which is that the higher authority is behind him! Ana kibali cha Mfalme kufanya haya anayoyafanya. Hii ya kujitia kuwakamata hawa vijana ni gheresha tu kujikosha mbele ya macho ya dunia!
Bila kumkamata Sabai, ni maigizo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kakamate na we we unaowafahamu. Sijui nyie mnashidaaa ganiiii. Polisi wakifanya kazi hamuwaaminii wakikaaa kimyaaa mnalalamikaaa, sasa mnataka iwejeee? Basi jitokeze uisaidie polisi kukamata wewe unaowajua.

Hawajataja hata majina yao kama wahalifu wengine. Wanawadanganya wafadhili tu ili kupata misaada.
 
Bado haijulikani mnataka nini?

Wasiwapeleke mahakamani kwanza.

Mpaka mume wenu atakapotii mahakama na kushtakiwa ashindwe au ASHINDE.

Ndipo hivi vidagaa vishtakiwe.
 
Wakati mwingine mnatia huruma, serikali isipochukua hatua ni kelele tu wakichukua hatua ni kelele pia, nyie kwenu baya ni lipi na jema ni lipi? Kama huwezi kujitanabaisha kwa wananchi hasa munataka na mnasimamia nn, kamwe hamwezi kuongoza nchi.
 
Hatuwez kuwahukumu kwa sababu baadhi yao ni watu wa kitengo na walokuwa ktk special task siku hiyo

Sheria ni msumeno tunategemea kesi zote kuendeshwa kwa usawa bila kujali kazi ya mtu.

Lakini cha kushangaza huyo DC bado yupo kazini. Hii ni ishara tosha kuwa hii ni geresha tu.
 
Wasipokamatwa mnalalamika, wakikamatwa bado mnalalamika na mmeanza hadi kuingilia uhuru wa mahakama sasa kwa kutoa hukumu..

Ndio maana serikali huwa haishughuliki na matukio yenu
 
Sasa wewe si uisadie polisi kutaja hayo majina? Viacheni vyombo vya dola vifanye kazi zakee

Yaani kutaja majina ni kazi ya kuisaidia polisi wakati wao wanasema watuhumiwa wamekatwa?! Halafu huyo DC bado anaendelea na kazi.

Hebu acha kujaza watu ujinga hapa.
 
Yawezekana "kukamatwa" kwa waliofanya fujo kwenye msafara wa Lissu ni propaganda ya kujisafisha tu lakini sio kwa nia ya halisi ya kulinda usalama. Kwa sasa dunia nzima inatuangalia kwahiyo sitoshangazwa kama walikuwa wanatuhadaa tu na kutufanya sisi na jumuiya za kimataifa ni mazuzu. Kesho na keshokutwa wakienda kuomba misaada watasema hao watu walichukuliwa hatua kumbe ni maigizo tu.

Mpaka hao waliofanya fujo wakifungwa ndio nitaamini kweli haki inatendeka.
nyie hata mfanyiwe vipi hamuishi kulalamika sasa ulitaka wasikamatwe? bado ungesema serikali haijali yaaninyie ni kama watoto wa kambo yaani ni walalamishi balaa hawaishi kuona wanaonewa wao tu da nyie aliyewaloga hayupo duniani angewasaidia
 
Kwanza nimpongeze IGP kwa agizo alilo litoa kwa RPC Kilimanjaro,pia RC wa Kilimanjaro. Matatizo ya Polisi na wananchi yanaanzia pale RC au DC anapojivika cheo cha chama wakati yeye ni mtumishi wa umma ambaye analipwa na serikali kwa pesa za walipa kodi wote wa Tanzania.

RC akijivika ukada wa chama au DC maelekezo yake yanakua ya kiitikadi , mifano ipo Mbeya,Iringa,Dsm wakati ule, Songwe (Tunduma), na ma RC wengi ambao kutwa wanafanya kazi za chama badala ya kufanya kazi za umma wa watanzania. Chama cha mapinduzi kina viongozi wake wa mkoa na wilaya, kwahiyo RC na DC hawapaswi kujifanya kuwa viongozi wa chama mkoani au wilayani, wanapaswa kuwa walezi wa vyama vyote katika maeneo yao ya kazi.

Tunaendelea kufuatilia, kwa sasa hivi kumezuka mtindo wa warudisha fomu za udiwani na ubunge kutekwa na wananchi wenginekukamatwa na Polisi.

Morogoro ametekwa mgombea udiwani ACT azalendo. Tunduma wagombea udiwani chadema wamekamatwa kwamba si raia,lengo wasiweze kurejesha fomu na huko.Mtwara/Lindi mgombea bunge ACT wazalendo ambaye alikatwana vikao vya ccm amekamatwa na Polisi.

Kwanini Polisi wanataka kuwachagulia wananchi viongozi ? waacheni watu wachukue fomu na kurejesha fomu wagombee nafac za uongozi, wananchi wanajua wanamtaka nani!

Huyo mnaye mzuia asigombee leo ndiye anaweza kutoa wazo la kubadilisha maslahi yenu ambayo yatakunufaisha wewe unaye mzuia njia.
CCM isiwatumie vibaya mkajisahau.
 
Back
Top Bottom