Haika Lawere: Wanawake ficheni Mali Zenu, Wanaume Ni Matapeli!


Sikutegemea kusikia haya kwa mtu kama Haika Lawere. Niliona smart na strong. Na vile ambavyo anapenda sisi walimwengu tujue mambo yake yamenyooka kupitia post zake za mitandaoni.

Ex Husband kuoa, tena mtoto wa mujini kama yeye, inaonekana imekuwa ngumi ya chembe kwake. anaanza kuwadanganya wenzake.

Binafsi sijui sababu hasa ya kuachana na mumewe...siwezi kumuhukumu. Sijui lolote. Ila alichosema sio sawa kabisa.

Experience yake sio universal...kila mtu anachangamoto zake na hazijawahi kuwa unique. wakati mwingine anagombania mali, mwingine anapambana watoto wasomeshwe.

mwingine anapambana mumewe an mke wake arudi warudiane. Kila mtu anapimwa kivyake.

Yeye anatumiaje mali kama kigezo? Namuonea huruma...maana najua pia, hatujakamilika. Ila mjuaji kama yeye ajipange na kupigwa matukio kama hayo 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Aione ephen_
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…