Haiwezekani Mungu asimuue Shetani halafu aamuru Watu waue wanaofanya mambo ya kishetani; Haiingii akilini

Sio kukubali Miungu wako wengi ilo liko wazi kama huangaiki na biblia tutajie huyo Mungu unayesema ni sawa na shetan
 
Kwa hiyo biblia unayosema imeborongwa alafu unaitumia tena kwa kumtuhumu Yahweh ni sawa na shetani samahan unakupaji wa unafki

Wewe ndio umeileta Biblia humu, sasa ninatumia silaha anayoitumia ninayejadiliana naye.
Hujui hata mijadala inavyofanyika au unadhani upo Kanisani hapa?
 
Kama unaamin shetani anahusika kweny maovu kwann serikali hutoa hukum ya kunyongwa kwa muuaji why shetani asihukumiwe?


uongeza. Someni dini ndo mje kureason.
Serikali haimtambui Mungu wala shetani. Haina dini
 
Sio kukubali Miungu wako wengi ilo liko wazi kama huangaiki na biblia tutajie huyo Mungu unayesema ni sawa na shetan

Mungu wa kwenye Vitabu vyenu ambaye hasimu wake ni Shetani kama mada isemavyo. Soma mada vizuri.
Kama Mungu unayemuabudu hasimu wake anaitwa shetani basi ndiye ninayemzungumzia hapa
 
Quran

Al-Hijr 15:26-44

"Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto.Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura.Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia.
Basi Malaika wote pamoja walimsujudia,Isipo kuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na walio sujudu.
(Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na walio sujudu?

Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yenye sura.

(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni! (Waliolaaniwa)

Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo.

Akasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watapo fufuliwa.

(Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika walio pewa muhula

Mpaka siku ya wakati maalumu.

Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote,ila waja wako waliosafika.

Akasema: hii njia ya kujia kwangu iliyonyooka

Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata.

Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote.

Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa."





 
Mungu yupo na bila shetani dunia ingekuwa inabore, shetani analeta vybez , uwepo wa shetani mitihani wa necta ya mbingu
 
Maisha bila dini inawezekana

Ukikaa ukafikiria, dini ni kitu kilichitengenezwa na binadamu pale ambapo alishindwa kujibu maswali magumu mfano, chanzo cha ulimwengu....

Umeanza kulitambua hilo, big up
Huwa unaandika makala zisizo kichwa wala miguu za kikristo, sasa nimethibitisha kumbe bado huna uelewa wa Mungu. Hoja zako ni za kiwango cha kawaida tu, unahitaji kuelekezwa uelewe, wala hazina ugumu kama unavyodhani. Tutakujibu ili uwe na ufahamu.
 
KISSENDI anaamini Mungu yupo, sio dini, na huyo Mungu ni upendo na matendo mema.
Kissendi Nyanda Ntalima Mpandagoya a.k.a Mkushi, yeye ndio muasisi wa makundi sogozi yanayojulikana kwa jina la Waafrika Tujitambue, ambapo amekuwa akifundisha mambo mbalimbali juu ya historia ya mtu mweusi, namna alivyokuwa kinara wa Mapinduzi ya ustaarabu na teknolojia duniani.

Lakini kutokana na husda na fitna za husda za NYAHUNI au mtu mweupe, akautweza utu wa mtu mweusi na kumsahaulisha kabisa asili yake kwa kutumia dini za Ukristo na Uislam.

NYAHUNI waliwakata mikono watu wote waliotokea kwenye koo za wahunzi.

Hizi harakati zina nia njema sana, lakini sidhani kama zitawafurahisha mabeberu
 

Malizia Ile Aya isemayo, aliyemnyoosha Mungu Shetani hawezi mpindisha, na aliyempindisha hawezi kunyooshwa
 
Ajiangalie asijiaminishe sana katika mawa
 
Twende taratibu huwezi ukaruka ruka tu mada ikiwa kweli unataka mjadala.

Sawasawa.

Embu tuambie Kabla Ibilisi hajaasi Mungu hakujua Ibilisi ataasi?
Kama alijua, ni Nani aliyeweka Uasi ndani ya Ibilisi maana Ibilisi ni kiumbe tuu, ameumbwa.
Ni kama Mimi na wewe
 
Jibu tunalipata kuwa kwanini MUNGU hakumuua ibilis palepale baada ya kumuasi? Ni kuwa Mungu hana desturi ya kuangamiza viumbe tu kwa kuvionea, huwa ana kawaida ya kuvipa muda kwanza ili kuona kama huenda vikarejea katika njia. Iblis nae amepewa muda mara baada ya kuona kuwa amehukumiwa upotovu...hakuona Toba kama adam alivyokuja kukosea na kula tunda la mti aliokatazwa...IBLIS aliomba apewe uhai mrefu tu ili aje kutimiza lengo lake la kuvipoteza vizazi vya adam.

Mungu alilijua hili na alimtaarifu mapema Adam na mkewe Hawa, kuwa Iblis ni adui yenu basi nanyi mfanyeni kuwa ni adui.

Hivyo Iblis bado ana muda mrefu wa kuishi ulimwenguni, sisi tutakufa tutamuacha mpaka wakati wake nae utakapofika wa kufa
 
Acha makufuru

wewe ni binadamu tu unayekunya na kuharisha limited with time, you are not worthy of questioning an eternal God's wisdom.
 
Mwambie mara ngapi Watu wameambiwa wamlete Shetani au Mungu Mahakamani na wakashindwa,
Kumaanisha wakosaji ni wao wenyewe Ila wanasingizia wengine wasiohusika.
Naomba kujua kwanza

Je unaamini katika uislamu au ukristo

Maana huwezi jadili habari za Mungu na Sheteni ilihali wewe huamini kama kuna Mungu na Shetani!

Na kama unaamini je hujui mipaka ya kuhoji habari za Mungu na Shetani katika dini yako?
 
Sawasawa.

Embu tuambie Kabla Ibilisi hajaasi Mungu hakujua Ibilisi ataasi?
Kama alijua, ni Nani aliyeweka Uasi ndani ya Ibilisi maana Ibilisi ni kiumbe tuu, ameumbwa.
Ni kama Mimi na wewe
Mungu ni mjuzi wa yaliyopita na yajayo. Anajua matendo watakayotenda viumbe wake kabla hata ya kuwaumba.

Wanaadamu na majini wameumbwa ndani yao wakiwa na Roho na Nafsi. Nafsi ndio mimi na wewe....hii nafsi imepewa uchaguzi wa kutenda iwe mema au mabaya, kuamini au kukufuru.

Mungu alichofanya ni kuibainishia nafsi matendo mabaya na mazuri kisha akaipa uhuru wa kuchagua inataka kufata kipi ila akaionya kuwa katika kila chaguzi mwisho wake itakutana na pepo ama moto.

So mwanadamu na jini wana haki ya kutenda wanalolitaka ila mwisho watalipwa kwa yale waliyoyachagua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…