Haji Manara abubujikwa machozi akimuelezea aliyemtweza sababu ya rangi ya ngozi yake,asema anamuachia Mungu

Kwanza huyo Takadini anakutana na watu wenye ustaarabu, kwa zile hulka zake akutane na mtu km mie, nampa mijineno mipya mipya mbna anakufa kwa kihoro.

Nashangaa watu kumuogopa mzungu pori, mbna hata hasitui kabisa. Lol
Mh mkuu basi na wewe ni fundi.

Unajua kupigana vita vya maneno ni ujuzi kama wa sanaa.

Ni utaalamu unaotakiwa kuwa na karama ya ujuzi wa kutunga na kufyatua albamu za papo kwa hapo.
 
Ahaa na wabaya wake wakilijya hilo watapiga hapo hapo
 
Ahaa na wabaya wake wakilijya hilo watapiga hapo hapo
Ni kama jina la utani vile!
Ukiitwa ukavimba, ndiyo watu wanakazia hapo hapo na jina linazagaa linakuwa la kwako kweli😁😁😜
Sasa na yeye kama analizwa kwa kuitwa zeru zeru, tena ambao uzeru zeru wake ni ukweli, basi kaisha.
 
Nimesima nae mnazi mmoja mkoja primary school alinitangulia madarasa,namfahamu kitambo sana
 
Waswahili tuna matatizo, hata matako hawataki uyataje na ndio jina la kiungo.
 
Yeye kuvunjia watu heshima yuko comfortable sana ila yeye kuambiwa mdomo unanuka tumbaku analia huku anasema watu wamekosoa uumbaji wa Mungu sasa mdomo kunuka tumbaku ni uumbaji au ni wewe mwenyewe kuvuta masigara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…