Haji Manara afungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa Miaka 2. Atakiwa pia kulipa faini Tsh milioni 20

Ila "makolo" alilowabatiza Simba unaliimba kikasuku! Acha kujichanganya.
 
Hatari kwelikweli wapi kwa kosa lile alitakiwa kufungiwa maisha, walianza kwa kupunguza adhabu ya wale maafisa wa Mbeya Kwanza ili Haji akipewa adhabu ndogo watu wasihoji na hapo watamwambia akate rufaa ili upunguzwe zaidi.
Kweli kabisa. Ile ilikuwa "calculated move" kuwaandaa wadau wa soka kwa hiki kilichotokea.
 
Hiyo ni kazi ya Maulid Kitenge na Zembwela, huyo Manara wamchukuwe GSM akasimamie maroli yao.
Yanga walikosea kumpa huyo mtu nafasi na ametoka nje ya Yanga,wakati wazalendo kama kina kitenge hawapewi hiyo nafasi.
 
Katika utetezi wake kwenye hilo shauri alisikika akisema mbele ya kamati kua haikua akili yake alitumia cannabis iliyosindikwa
 
Adhabu ni kali sqna .imekaa kukomoana .Sijui wachezaji wanaopiga mwamuzi watafungiwa muda gani
.Je adhabu iliyotolewa ipi kwenye taratibu za TFA?
 
Wapi ulionyeshwa kuchukiza kuja kwake? Mbona hujaonekana kujitenga na mihemko na kauli zake?

Labda shabiki ambaye alionyesha dhahiri kuwa hamkubali Manara ni Matola kwa hali zote..!
Mkuu kwanza ungeonesha sehemu yoyote niliyomuunga mkono ili kudhirisha kauli yako.
 
Yanga imehujumiwa kipi? Mafanikio ya Yanga ni pesa za GSM na si vinginevyo, ukiona mtu anachukiwa na wengi ujuwe ana tatizo.
Kuna wajinga wanajisahaulisha hii fact.
 
.... Katibu mkuu wa zamani wa (TFF) !

"Kuna mambo mengi sana katika hii commettee, huwa ninaonekana mimi ndio huwa na tatizo nayo au na TFF, lakini kanuni ziko very Clear, anayehusika pale ni secretariet ya ethics Committee na si ya TFF"

"Haiwezekani Secretariet ya (TFF) ika-file Case, halafu ikahusika na adminstrative work ambazo kamati itahitaji kama kuandika minutes, kutunza nyaraka na nyingine"

"Kuna kuwa na conflict of interest,, Pale kulikuwa kuna kurushiana maneno na KARIA anaonekana anamnyooshea kidole HAJI, kwa hiyo Secretariet haiwezi kumshitaki KARIA kwa kuwa ndiye Boss wao"

"Maana yake, Mwenyekiti wa kamati angeitisha suala hilo mezani kwake kwa kuwa aliona kuna uvunjifu wa maadili, Secretariet ya kamati ingelifikisha suala hilo mbele ya kamati na baadae KARIA na HAJI wangeitwa kujitetea"

"Ndio neutrality inavyoelezewa kwenye ethics Code, wenzetu wameenda mbali zaidi kwa kuunda chamber mbili katika kamati ya maadili....."

".... (1) Investigation chamber, ambayo hufanya uchunguzi wa tatizo na (2) Adjudicator chamber ambayo huendesha shitaka. Hapo hakuwezi kuwa na conflict of interest"

[emoji368] Angetile Osiah
 
Keshaanza kutuma message za kutafuta kuonewa huruma. Muda huu ndio atazumgumziwa kama m2 anaehitaji huruma kutokana na maumbile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…