Haji Manara afungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa Miaka 2. Atakiwa pia kulipa faini Tsh milioni 20

Haji Manara afungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa Miaka 2. Atakiwa pia kulipa faini Tsh milioni 20

Bongo kila kitu sahivi ni mipasho mipasho.....taaluma,fani etc zinaendeshwa kimipashomipasho
Ndomana Internationaly huwa tuna
Angukia pua

Ova
 
Msemaji wa Yanga, Haji Manara amefungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa muda wa miaka 2 na kupigwa faini ya Tsh milioni 20

Manara amekumbwa na adhabu hiyo kutokana na sakata lake na Mwenyekiti wa TFF
View attachment 2298517
====

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemfungia Msemaji Klabu ya Yanga, Haji Manara kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa muda wa miaka 2 na kupigwa faini ya Tsh. milioni 20

Amekutwa na hati kwa makosa ya kumvunjia heshima Rais wa TFF, Wallace Karia kwenye fainali ya ASFC kati ya Yanga na Coastal Jijini Arusha
View attachment 2298509
Akome
 
Ogopa sana yani hadi wana Yanga wamefurahishwa na hii taarifa
Hakuna mwana yanga kaunga mkono huo upuuzi nafikiri nyuzi zetu za mpira Kule wanayanga unawatambua

Hao unao waona wanajisemesha mimi ni yanga kawatafute kule utagundua ni makolo wenzio
 
Sema hivi ameingiziwa mchanga kwenye kitumbua Kwa wivu wa ubingwa wa kihistoria [emoji124]
Manara Hana professionalism kwenye matamshi yake.

MDA mwingi Anaongea Kama mshabiki layman wa mpira na sio msemaji official wa club kubwa na kongwe Kama yanga.

Hizi tabia za kuropoka ropoka alitakiwa awaachie mashabiki Kama kina Ally yanga, maana wao mkono wa sheria uko mbali nao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ko mlidhani yule msomali angemwacha[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]yule mzee anakulaga mirungi asingemwacha
 
Duh faini million 20 tff wanajenga barabara za mtaa wapi hivi wajumbe wote wamepitisha hili .Hapa ilitakiwa faini mil 5 na ban ya miezi 6 tu biashara inaisha kwa sababu hii ni soka.
 
Duh faini million 20 tff wanajenga barabara za mtaa wapi hivi wajumbe wote wamepitisha hili .Hapa ilitakiwa faini mil 5 na ban ya miezi 6 tu biashara inaisha kwa sababu hii ni soka.
Yule 'msemaji' hakupaswa kuaminiwa na taasisi kubwa, ana matatizo!
 
Karia ni mpita njia tu. Muda wake ukifika atafurumushwa pale TFF hata kwa mateke.

Enzi za Leodgar Tenga, hakukuwepo na mambo ya hovyo hovyo ya baadhi ya watu kutaka kuonekana kama miungu watu kwenye mpira wa Tanzania.
 
Bumbuli huko aliko, anakunywa kahawa na kashataa, yaan ana furaha mnooo.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hata mzee wa "wape salaaam" atakuwa anacheka sana huko aliko.

Jamaa alianza kumfanyia figisu ionekane kama hakuna haja sana ya Bumbuli kuwepo kwenye kitengo hicho ilihali yeye yupo, kila sehemu akajiweka kimbembele ikafikia hatu yeye ndo akaonekana ni msemaji na Bumbuli awe mhamasishaji, kumbe ni kinyume.

Halafu akajikuta anauchungu sana na Yanga Sc kuliko aliowakuta[emoji23].
 
Back
Top Bottom