Haji Manara afungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa Miaka 2. Atakiwa pia kulipa faini Tsh milioni 20

Haji Manara afungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa Miaka 2. Atakiwa pia kulipa faini Tsh milioni 20

Nikiwa mpenzi wa mpira na mpenzi wa klabu bingwa Tanzania, Dar Young African!nimefurahishwa sana na hii adhabu!sikuwahi kumkubali tangu akiwa makolo FC na sasa Yanga!!mimi ni muumini wa soka/utani wa kistaarabu na uungwana!!haiwezekani mtu anatukana wenzie,akiguswa tu anakimbilia anaonewa!!mtu hataki watu waikosoe club anayoifanyia kazi na matokeo yake wachambuzi wengi wanaogopa kuikokosoa Yanga kwa kuogopa manara atawararua katika ukurasa wake!!mambo ya ovyo sana haya!!ngoja akae benchi ajifunze weledi kazini!
Alituambia pale Yanga mtu mwenye akili ni Baba yake na Mzee Kikwete tu.
Huyu jamaa alijua kutukera ni haki yake akatangaze Rimoti za Azam Tv kwa sasa.
 
duh pole zake m20 sio hela ndogo saa nyingine bora kuwa kimya tu
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha

Kicheko cha Bumbuli chooni, polenii sana wanajangwani, kwa hiyo hatatambulisha wachezaji siku ya mwananchi?
ile ni sherehe,atapewa kazi kama mamc wengine, Zembwela, Mpoki etc.
 
Safi sana wangemfungia maisha kabisa, huyu kijana ulemavu wake ndo amefanya kinga ya kuwakosea watu adabu. Mi naonaga hata kinyaa kumsikia akajifunze ustaarabu.
dah usiseme hivyo ni yeye na akili yake tu ulemavu sio kigezo bhana
 
Duuu, yule Msomali ni hatari kweli kweli, kwa kweli haji alikanyaga pabaya, RIP Haji!
Hatari kwelikweli wapi kwa kosa lile alitakiwa kufungiwa maisha, walianza kwa kupunguza adhabu ya wale maafisa wa Mbeya Kwanza ili Haji akipewa adhabu ndogo watu wasihoji na hapo watamwambia akate rufaa ili upunguzwe zaidi.
 
Msemaji wa Yanga, Haji Manara amefungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa muda wa miaka 2 na kupigwa faini ya Tsh milioni 20

Manara amekumbwa na adhabu hiyo kutokana na sakata lake na Mwenyekiti wa TFF
View attachment 2298517
====

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemfungia Msemaji Klabu ya Yanga, Haji Manara kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi kwa muda wa miaka 2 na kupigwa faini ya Tsh. milioni 20

Amekutwa na hati kwa makosa ya kumvunjia heshima Rais wa TFF, Wallace Karia kwenye fainali ya ASFC kati ya Yanga na Coastal Jijini Arusha
View attachment 2298509
Yanga tushahujumiwa tayari
 
Za ndaaani kabisa Bumbuli ndiye alimroga ili afanye kosa lile kwani Haji Manara mwenyewe anasema hata hajui nini kilitokea siku ile. Hassan Bumbuli Mungu anakuona.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] dah nimecheka sana asee kwahyo bumbuli mganga wake wa kweli[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huyu jamaa ana backup kubwa sna nyuma yake..hii ni danganya toto kama hamuamin muda ni mwalimu mzuri...vipi akibaki kama shabiki wa yanga??
Ushabiki wake uwe wa moyoni,marufuku kwenda uwanjani,kama ni mechi aangalizie nyumbani Kwake!Yaani hata Yanga ikishinda,basi afurahie huko huko nyumbani Kwake!
Wana Yanga wanaomfuata kwenye mitandao ya kijamii wataishia kukutana na matangazo ya ASAS!
 
Karia alimbeba alipokuwa simba sasa kahamia mtaa wa7 ndo hayo
 
Atakata rufaa ,atafunguliwa,maisha yataendelea ......hii ndiyo tanzania bwana

Ova
 
Alishazoea kuwa tukana MO na Barbara ila sasa ameingia sehemu mbaya
 
Back
Top Bottom