HAJI MANARA NI KIELELEZO CHA MAPINDUZI YA MPIRA WA TANZANIA :
Vilabu vyetu vya Mpira ni Taasisi kama zilivyo Taasisi zingine Duniani. Taasisi zote Duniani zimekua zikipambana kuhakikisha zinapata wafanyakazi Bora ambao wataifikisha Taasisi husika kwenye kilele cha Mafanikio. Bahati mbaya mpira wa Tanzania Kwasababu Kwa miaka mingi umekua ukiendeshwa kitamaduni. Soka letu Kwa miaka mingi limekua likiongozwa na mashabiki Wa vilabu badala ya watu Wenye Weledi, Taaluma na uzoefu wa kuhudumu Kwenye Idara mbalimbali za vilabu vyetu.
Mapinduzi makubwa ya kibiashara Kwenye soka la Tanzania yaliyochipua Kwa miaka ya Karibuni yanapelekea Mabadiliko makubwa ya kiutendaji na kimfumo Kwenye Taasisi hizi. Kidogo Kidogo utaratibu wa mashabiki kuviongoza vilabu Bila kujali ubora,uzoefu na Taaluma zao unaenda kutoweka. Alianza Senzo kutoka SA mpaka Simba Akiwa sio mwanachama, Baadae akaibukia Jangwani. Tumeona aliekua Katibu Mkuu wa Yanga Dkt. Jonas Tiboraha akitambulishwa Azam FC, na hatimaye Leo Haji Manara amerejea "Umamani". Yanga Ni klabu yenye historia kubwa zaidi Nchini kuliko yeyote, inafanya mazuri lakini walikosa mtu wa kuyakweza na kuyasemea wanamwachaje mtoto wao anazagaa wakati ana mdomo wa Dhahabu???
Mwisho watu wanatakiwa kutambua Kwamba Yanga ni Zaidi ya klabu, Yanga ni utamaduni na utamaduni Una tabia ya kurithiwa. Haji Manara ni Nani asiwe sehemu ya mirathi ya Baba yake, wazazi wake na familia yake?. Karibu Jangwani HAJI, Hadithi za klabu kubwa Afrika Mashariki sasa inaenda kusimuliwa Kwa Sanaa na Ubunifu Wa kisasa. Haya Ni unblock Basi Tuungane kuipeleka mbele Yanga yetu tuliyoirithi.