Mwamba umeendelea kung'ang'ana na msimamo wako. Binafsi sina uwezo wa kuvunjavunja hoja zako kwa hoja nzito zaidi lakini naamini Mungu yupo na naamini hoja zako kuna siku (au pengine tayari) zitajibiwa kwa kiwango cha kukuridhisha na mwishowe utajitokeza mwenyewe hadharani kukiri na kuomba msamaha!
Kuamini unaruhusiwa kuamini lolote unalotaka, hiyo ni haki yako ya kikatiba.
Lakini, kuamini kitu hakukifanyi kitu hicho kiwe kweli.
Kitu muhimu hapa si unaamini nini, kila mtu anaruhusiwa kuamini anachotaka.
Kitu muhimu hapa ni, ukweli ni upi?
Ukweli ni kwamba, dhana ya kuwepo Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, aliyeumba ulimwengu huu unaoruhusu mabaya kuwapo, inajipinga yenyewe (ina internal contradictions).
Kujipinga huko kunaonesha Mungu huyo hayupo.
Yani, ni sawa mtu akwambie kwamba, katika Euclidean geometry, kuna duara, lina nyuzi 360, halafu kuna pembetatu, ina nyuzi 180, vitu hivi viwili ni tofauti.
Halafu, hapo hapo, akwambie kwamba, kuna pembetatu-duara moja ya ajabu ipo, yani hiyo hapohapo ni pembetatu na pia ni duara, kwa wakati mmoja.
Utakubali habari hiyo kuwa ni ya ukweli?