Naipendatz
JF-Expert Member
- Jul 27, 2011
- 5,096
- 8,234
Kuna wahuni bado wanamlaumu Mama, hasa hawa wa CHADEMAMama Samia atakuwa na sisi mpaka mwaka 2030 Mungu akijalia.
KIpindi cha JPM kuna mambo yalikuwa hayako sawa ila tulikuwa hatuthubutu kuropoka coz aliweza kuvibana vizuri vyombo vya habari. Kina Azory Gwanda,Ngurumo etc.
Bungeni pia aliweza kuzuia na kuna mpaka wabunge walifungwa (Sugu) na wengine kupigwa Risasi ( TL).
HAPA JF tu jukwaa la siasa tulikuwa tukipost za kumkosoa JPM na serikali yake @mods wanazifuta.
Tuliona Maxence Melo wakimuweka ndani kisa privacy.
JPM 2019 alibaka uchaguzi wa serikali za mitaa bila aibu akawaengua wapinzani nchi nzima.
2020 akaunda bunge la chama kimoja. Moja mzigo mkubwa sana aliotuachia na utatutesa mpaka 2025.
Hili bunge limekuwa nuksi imagine wanapelekewa muswaada wenye mapungufu kisheria wao hata hawausomi wanaupitisha tu. Cc sheria ya tozo katika miamala ilivyowaathiri service providers kwa kukosa mapato.
Tulimtukanaga sana KIKWETE akawa anatabasamu tu. JPM alivyokuja tu ule mwaka wa kwanza tu kila mtu akachoka kuanzia wafanyabishara mpaka wafanyakazi.
Mimi nitaanza mlaumu huyu mama 2031 baada ya kutoka madarakani aise.