Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Vipaji vinaweza kuwepo. lakini msisahau pia kuna wakati mazingira yanaweza kuidanganya jamii kuwa fulani ana kipaji na fulani hana. Kumbe fursa ya mazingira tu yamemfanya mwingine kuonekana ana kipaji na mwingine hana. Mfano mzuri kwa Tanzania kidogo ni ngumu sana kujua vipaji vya watoto. Kuna shule zinaitwa za vipaji maalum lakini kimsingi ni shule za wachache wenye vipaji maalum na walio wengine waliopata fursa ya mazingira mazuri na wao wakaonekana wana vipaji maalum kumbe hawana. Ndo maana utaona vijana wanaenda shule form one kwa kigezo cha ufaulu wa marks lakini kidacho cha nne ufaulu huo wanapitwa na waliokuwa shule za kawaida.

Lakini pia hizi shule zetu zinazoitwa za vijapi hazijaweza kutusaidia kama Taifa kuwa hata na Ubunifu ili kuikwamua nchi. Hapa kuna mawili, ni ama tunaowapeleka kule siyo watu sahihi au sisi wenyewe kama nchi hatujatoa fursa ya kimazingira kuweza kutambua vipaji vya vijana wetu hawa au hatujaweka mazingira wezeshi hivi vipaji kuonekana na kuwa msaada kwa nchi.
 
Mkuu kwako wewe unatafsiri kipaji ni nini?

Kimsingi hakuna mtu anayezaliwa na kipaji moja kwa moja...... kila mtu anaweza kujifunza jambo na akaweza kulifanya kwa uzuri tu.
Kipaji ni pale namna mtu anavyoweza kuwa na uwezo wa kulifanya hilo jambo baada ya kulijua kulifanya

Mara nyingi watu wenye vipaji huwa wanajipambanua kwa upekee na ubora wao wa kufanya jambo husika

Kuna mambo mengi yana weza kufanya kipaji kikajidhirisha
Wapo ambao maumbo yao, au viungo vyao, au hormoni zao, mazingira/eneo unaloishi au hata JUHUDI zao zinaweza kuwa favor vipaji vyao

Kiufupi kabisa KIPAJI ni uwezo wa KIPEKEE wa ziada wa kufanya jambo dhidi ya wengine

Hayo maswali ulio uliza...... yes kuna watu wana(upekee wa ziada kufanya)

Kuhusu Messi na Bolt..... wangeweza kuwa na kazi zingine tu kama mamilioni ya Wabrazil na wajamaica wengine wanafanya nje ya Riadha na soka

Mwisho Walokole kukariri Bibilia sio VIPAJI mkuu
 

Mkuu nakosa maneno ya kukuaminisha kuwa hakuna kipaji lakini naamini utakaa, utatahmini kwa kina juu ya kuwepo au kitokuwepo kwa kipaji kisha ikikupendeza utakuja na majibu ya kuwa 'hakuna kipaji'.

Karibu sana mkuu.
 
Hapo kwenye kuangalia mara Moja kuanatokana na kizoesha kukariri position ambayo kitu fulani kipo na uwezo huu wa kukariri Kila mtu anao shida ni kwamba hatuutumii.

Ili uwe na uwezo wa kukariri/ku improve memory yako fanya mazoezi yanayoitwa Chunking
 
Jibu ni kwamba hakuna kipaji.
Acheni kwanza kutumia hilo neno maana ni zaidi ya tusi.
 
Mkuu Mimi ninachokipinga ni hii dhana ya kusema "kipaji ni uwezo wa asili ambao mtu anazaliwa nao kwa mfano Messi alizaliwa na uwezo wa kucheza mpira na Ronaldo hajazaliwa na uwezo wa kucheza mpira bali analazimisha kucheza kwa kutumia nguvu nyingi kufanya mazoezi".

Siamini kama mtu anatoka tumboni mwa mama yake akiwa anajua kufanya jambo fulani.

Ni hayo tu mkuu 😎
 
Nakubaliana na wewe kwamba mtu hazaliwi na kipaji....... ila vipaji vipo

Kipaji ni jambo linakuja kujidhihirisha baada ya kuwa na interest nalo na kuanza kulifanya...... na hii ITATOKANA na mambo mbali mbali kama nilivyo eleza hapo juu.
Kama huta lifanya wala kuwa na interest nalo nothing will happen

Messi angezaliwa na Yahya Sinwar pale Palestine saa hii kama angekuwa hajapigwa mabomu ya Israel angekuwa kwenye mahandaki huko chini huku kashikilia shotgun kavaa tasbii na quran mkononi na angekua anaona soka ni haraaam

Sawa na genius wa darasani Mzumbe au inter schools kama angezaliwa na Wahadzabe wasiosoma saa hii angekuwa maporini huko anawinda digi digi hata tebo ya pili haijui

Na mtu anayesema Ronald hana kipaji atakua hajui maana ya kipaji
 
Mkuu nilichokuwa nabishia ni kuaminishana kuwa tunazaliwa na uwezo wa kufanya jambo fulani (kipaji).

Basi tubadili definition ya neno kipaji.
 
You will be fine.. you will be fine. Unaumwa ugonjwa wa waafrika wengi kuamini matatizo yao yote yamesababishwa na mzungu... but you will be fine.
Haya nakuuliza, je, mtu anazaliwa na uwezo wa kufanya jambo fulani(kipaji)?
 
Definition yako ya 'Kipaji' ndiyo inasababisha unaona hakuna mtu anayezaliwa na kipaji.
Hakuna kipaji cha kuchora, kukimbia, kucheza mpira n.k ila, mtu anaweza kuzaliwa na uwezo unaofanya kufanya kitu fulani kuwa easy kwake. Huo uwezo hutokana na formation ya ubongo au misuli, mifupa na sehemu zingine za mwili.

Mifano:
Mtoto mwenye mikono mirefu na myepesi anaweza kujifunza kuchora kwa urahisi, lakini pia anaweza kufanikiwa katika upigaji wa vyombo vya muziki au ubunifu wa mavazi – yote haya yakitegemea ufanisi wa mikono.
Vilevile, kijana mwenye misuli yenye nguvu anaweza kuwa mwanariadha mzuri, mchezaji wa mpira, au hata askari, kutokana na uwezo wake wa kimwili.

Kwa hivyo, "kipaji" ni mwelekeo wa kiasili unaowezesha kujifunza kwa urahisi, lakini mafanikio hutegemea mazoezi, mwongozo, na mazingira bora ya kukuza uwezo huo.
 
Mtu anazaliwa na kipaji. Acheni siasa kwenye mambo yaliyoko wazi kabisa. Hata kama Messi angezaliwa Palestina na kutocheza mpira isingeondoa ukweli kuwa ana kipaji cha mpira. Tuliosoma zamani tunakumbuka ikifika UMITASHUMTA kuna jamaa mtoro alikuwa anaenda kutafutwa aje kuidakia timu ya shule kwa sababu ya kipaji chake... kuna mwingine alikuwa na akili ila shule hataki hadi mgambo wakamkamate... alifaulu kwenda Ilboru na akasonga mbele hadi UDSM. Acheni siasa.
 
Mkuu nilichokuwa nabishia ni kuaminishana kuwa tunazaliwa na uwezo wa kufanya jambo fulani (kipaji).

Basi tubadili definition ya neno kipaji.
Kwahiyo wewe unaamini kama Messi angekuwa ana interest na kufanya mchezo Gymnast au riadha au kuogelea au kulenga shabaha nk nk kwa namna alivyo kwenye soka basi angekuwa na uwezo wa hali ya juu kwenye michezo hiyo kama alionao kwenye soka kwasababu unaamini ni JUHUDI tu imemfikisha hapo?

Kwamba Michael Jackson angezingatia kwa bidii na kuwa Boxer angekuwa na uwezo wa juu kama alivyofanya kwenye muziki?

Kama majibu hapo juu ndio basi utakua SAHIHI
Kama majibu ni hapana basi kila mtu anauwezo wake wa ndani(kipaji) amezaliwa hivyo...... kinachotafutwa ni trigger tu

Mimi naamini kipaji kinadhihirika pale mtu anapo kuja kufanya jambo sahihi kulinga na mazingira yanayo favor uwezo wake wa juu(kipaji)

Unaweza ukawa ni mchoraji mzuri lakini kumbe (ulivyozaliwa)body morphology and other factors zingeweza kukufanya uje kuwa mcheza tenesi mwenye uwezo mkubwa sana lakini mazingira hayakukupa nafasi ya kuujua wala kuucheza mchezo huo

Sioni tatizo la tafsiri
 
Nenda google tafuta definition ya kipaji kwanza mkuu.

Ukamaliza rudi huku.
 
MamaSamia2025
Mkuu kila mtu duniani anakipaji

Ili kipaji kijidhihirishe ni lazima ufanye hilo jambo ambalo unakipaji nacho.... Usipolifanya itabaki HUNA KIPAJI

Sio kama Messi alizaliwa anajua kucheza mpira...... alijifunza na kuupenda mchezo wenyewe na luckily enough ilikua ndio kipaji chake

Kuna zaidi ya mambo milioni moja mtu anaweza kuwa na kipaji nayo...... issue ni kwamba huwezi jua kipaji chako kipo wapi katika hayo labda mazingira yaku favor kuujua hilo jambo

Kwasababu inawezekana wewe hapo unakipaji kikubwa sana cha jambo fulani lakini Bongo unapoishi hilo jambo halipo
Ukiulizwa unakipaji gani utajua?

Same to Messi, angekua Gaza angekua anaona Soka ni haramu
 
Amini hivyo hivyo, ukweli utaupata siku ukiwa mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…