Hakuna kitu kinachoitwa kipaji (kuzaliwa na uwezo wa kufanya kitu fulani)

Ni kweli hakuna mtu anaezaliwa na uwezo wa kufanya jambo fulani,.. bali uhalisia ni kwamba mtu "A" atakua vizuri na mtaalamu kwenye jambo fulani kuliko mtu "B" kutokana na sababu zifuatazo:-

1. Mazingira,,.. Mazingira yana nafasi kubwa sana ya kumfanya mtu apende jambo fulani kutokana na kuliona hapa kuna mtu atakuliwa kwenye jamii ya wapenda uvumbuzi, michezo na kadhalika... yaani Mtoto anayekua kwenye jamii ya wanamichezo au wasanii ana nafasi kubwa ya kuathiriwa na mazingira hayo.

2. Kupenda jambo fulani,.. hapa sasa kutokana na shughuli mbalimbali zinazoendelea kwenye mazingira inamfanya mtu kuwa na mapenzi na shughuli fulani ambayo ipo kwenye jamii hivyo atajikuta anajifunza shughuli hiyo na kujikuta akiongeza ujuzi zaidi hadi kuwa mtaalamu haswa...,Mtu anapopenda kitu, anakuwa tayari kutumia muda, nguvu, na maarifa kukiendeleza., hivyo utakuta anafanya mambo makubwa na kushagaza kwenye fani husika.

3. Akili ,.. hapa ndiyo panapoleta tofauti kubwa lazima tukubaliane kwamba kiwango cha akili kinatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine na ndiyo maana utaona watu 10 wanafanya jambo moja tuchukulie mfano ni wachoraji,. ila utakuta 1 au 2 kati ya hao anatoa kitu bora zaidi., hapa uwezo wa akili kukumbuka, kuamini kwenye uwezo wake na kufikiria kwa haraka zaidi umetengeneza gap kati ya watu.


so, kutokana na hivyo vitu vitatu hapo juu sisi ndiyo tunakosea kwa kusema kwamba mtu fulani amezaliwa na uwezo fulani(talent) kumbe haipo hivyo ni mazingira, mapenzi juu ya task fulani na akili ya mhusika.
 
📌📍📍🔨🔨🔨.
Siongezi neno hapa!
 
Useless thread,vipaji vipo na kama unabisha nenda kacheze mpira kama Messi tukuone
Lamine Yamal angezaliwa Tanzania asingekuwa na uwezo kama alionao Leo.
Hata Messi na Ronaldinho wangezaliwa Tanzania wasingekuja na uwezo kama ule japoku Tanzania Kuna mchezo wa soka.
 
Mkuu point ya vipaji kuendelezwa unaipotezea.
Lamine angekuwa Tanzania angecheza mpira lakini uwezo wake ungekuwa wa kawaida.

Lamine anashine si kwa sababu alizaliwa na uwezo wa kucheza boli bali mazingira yanamfavour.
 
Hayo mazingira kwanini yamfavour yeye na kuacha wengine?
Haya kwa nini wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza wana uwezo mkubwa kuliko wa timu ya taifa ya Tanzania?
Je ni Kawa sababu wenye vipaji ya soka wanazaliwa tu Uingereza?

Haya jibu la swali lako ni kwamba wote hamwezi kufanya jambo katika kiwango sawa. Yamal anawazidi baadhi ya wachezaji kama Feisal Salum anavyowazidi baadhi ya wachezaji wa hapa Tanzania.

Huyu fei toto ambe kwa huku mnasema ana kipaji na anafanya mazoezi akienda kwenye ligi kuu ya Uingereza anawekwa benchi na wachezaji ambao nyinyi mnadai kuwa hawana vipaji lakini wote wanafanya mazoezi😂😃😅.

Cc implicit memory Nomadix Al-mukheef
 
Mkuu swali ambalo linatakiwa kujibiwa kwamba ni kitu gani ambacho hufanya mchezaji mmoja kuonekana bora kuliko wenzake na hali ya kwamba watu wapo katika mazingira sawa na hufanya mazoezi sawa?
 
Mkuu swali ambalo linatakiwa kujibiwa kwamba ni kitu gani ambacho hufanya mchezaji mmoja kuonekana bora kuliko wenzake na hali ya kwamba watu wapo katika mazingira sawa na hufanya mazoezi sawa?
Mkuu ukisoma comments zangu toka mwanza hayo mambo nimashayaelezea vya kutosha na ukipata muda jaribu kuangalia zile comments nahisi utakubaliana na mimi kuwa hakuna kipaji.
 
Mkuu swali ambalo linatakiwa kujibiwa kwamba ni kitu gani ambacho hufanya mchezaji mmoja kuonekana bora kuliko wenzake na hali ya kwamba watu wapo katika mazingira sawa na hufanya mazoezi sawa?
Hakuna mtu aliyezaliwa akiwa anajua kuendesha Baiskeli,. ila ukiwachukua watu 10 na kuwashindanisha kwenye mchezo wa kuendesha baiskeli mmojawapo ataonekana bora kuliko wengine.

Je, hapo utakua sahihi ukisema huyo aliyeshinda amezaliwa na kipaji cha kuendesha baiskeli?
 
Akikujibu tafadhali unitag😎.

Niko chini ya mguu yako.
 
Sasa ni nini kinachomfanya Messi aonekane anajua kuliko wengine
 
Sasa ni nini kinachomfanya Messi aonekane anajua kuliko wengine
Ni kile kinachofanya Fei toto kuonekana mchezaji mzawa Bora kwa sasa kwenye NBC Premier league.

Niambie kwanza kinachofanya Feisal kuonekana bora kuliko wachezaji wengi (japo si wote) wazawa kwenye NBC Premier league.
 
Kaka ambaye ni miongoni mwa wachoraji wakubwa nchini na uliyejifunza uchoraji kwa siku mbili tu mbali na hongera zangu kwako. 🙏🏾Tupia hapa kazi kadhaa ulizochora ili kutuInspire sie tunaopambana kujifunza kuchora kwa miaka kenda bila mafanikio.
 
Ujuzi au uelewa wa kitu fulani unategemea vitu viwili. Brain plasticity au unaweza sema incremental web of information and adaptability. Na subject inclination au kitu ulichoamua kujifunza haijalishi causation ni nini. Inaweza kuwa inflicted/reinforced au personally.

Kwenye kujifunza kuna kitu kinaitwa learning curve. Ni muda unaotumia kujifunza kitu mpaka ukakielewa.
Kiasi cha web of information ulichonacho kinapunguza hiyo learning curve, haswa kwenye mambo related.

Hiyo ndio sababu inayosababisha watoto waliolelewa kwenye mazingira fulani au walio-enforced in certain subjects early, wanakuwa vizuri kwenye subject hiyo na subjects nyingi. Na uwezo wao wa kujifunza ndani ya muda mfupi ni mkubwa zaidi. Na vice-versa is true.

Hiyo ndio sababu watu wanaenda shule. To expand capacity and increase brain plasticity speed.

Hivyo as long as uta-stick na certain subject, depending on your level of web of related/information, ndani ya muda fulani lazima upate ujuzi hitajika.

In other words, unaweza sema, geniuses aren't born but intentionally created or results of environmental spontaneity.
 
Hiyo uwezo wa kufikiria nna ya kufanya kwa ubora zaid ndo kipaji sasa.
 
Pia naamin unaezajifunza fani na ukawa vizuri kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…