Hakuna kitu kinaleta Stress kama kuota Mvi au upara halafu bado hujajipata

Hakuna kitu kinaleta Stress kama kuota Mvi au upara halafu bado hujajipata

Kanuni za Afrika ni ngumu sana Mkuu.
Kuajiriwa tuu Watu wanaangalia vitu vingi ikiwemo Physical appearance ya MTU.
Hata kwenda kuchumbia ni vivyohivyo.

Ni kweli Upara na mvi ni ishu ya kijenetiki lakini huwezi kuvitenganisha na kuzeeka.
Kipara na Mvi ni sehemu ya uzee.
Acha Ujinga kwa kua huna upara ww. Nenda China uone vijana wadogo walivyo na upara.U para sio uzee.
 
Mkuu unanigusa,kipara kimeanza kuniota mwishoni mwa mwaka jana na umri (nina 30 to 40 yrs of old) umesonga,hata gari sina nimeishia kuwa na familia ya wake wawili na mji mmoja,kibaruani kazi tembo mshahara sungura,naishia kujishangaa tu.
Duh! Pole sana yaani
 
Formula ya Bongo kujipata ni miaka 50 msidanganyike, kinyume cha hapo hayo ni majizi tu.

Vijana msikate tamaa, hakuna tajiri yoyote Africa ambaye ni self made millionaire ambaye yuko under 50, hakuna.
Asante sana. Huyu jamaa anataka kukatisha vijana tamaa na hajui kuwa wanakumbana na changamoto nyingi sana. Kwenye maisha hakuna kitu kibaya kama kukata tamaa.
 
Unekaa zako na furaha kama zote ghafla Ubongo unakukumbusha umri wako, ""Bro!!! Una 35 wewe huna Kiwanja, huna Mke wala Mtoto wa kusingiziwa""
Unaweza uwe na kiwanja na usijenge.

Maisha ni vile mtu ameridhika yeye na nafsi yake; siyo kuwaridhisha wengine.

Kamwe huwezi kumridhisha mtu mwingine zaidi ya wewe mwenyewe.
 
Hiyo betting ni mbaya sana. Fikiria kijana anapiga mzigo na kutafuta maisha mpaka miaka 50 alafu bilabila. Ndio atake kuanzia familia. Binti wa nani atakuwa tayari kumkubali?
Mimi kila siku huwa nasema wewe ni kilaza. Unajua mtu aliyeanzisha KFC? Unajua alikuwa na miaka mingapi wakati anaanza? Wacha kukatisha vijana wa Tanzania tamaa. Kufanikiwa hakuna umri, kuna watu wanapiga mpaka miaka 80 ndiyo kinaeleweka.
 
Kwema Wakuu!

Ni Stress hapa!
Ni sonona hapa! Kihoro kinakaba kama pumu huku. Yaani hapa mambo sio mambo.

Kuna Watu wanakuambia umri ni number tuu lakini huko ni kufarijiana tuu!
Hakuna kitu kinauma na kuleta mfadhaiko na mtagusano kulinafsi kama kuona jua lile linazama halafu wewe mambo bilabila.

Nywele kunyonyoka kama mbwakoko mzee. Alafu ukicheki huna mbele wala nyuma sio Pouwa Washikaji.
Mvi kukuota wakati unaishi chumba kimoja sio lelemama ndugu zangu.

Fikiria mvi hizi hapa alafu huna hata mke wala mtoto. Kiumri ni miaka labda 35 hivi. Shida ni kuwa mpaka muda moja na mbili haikai.
Kila ukikumbuka ile kauli ya kusema nikiwa mkubwa nitafanya bla! Blah! Blah! Unapiga ngumi ukutani.
Nani akutake na mvi zako Budah! Yaani huna pesa alafu umejaza mvi kichwani. Ni binti gani yupo tayari kukubali kuwa nawe?
Binti gani atakubali kuwa na wewe na kipara chako na hauna Maisha.

wanasema vijana ndio huona maono bwashee! Wazee wenye mvi na vipara huota ndoto tuu. Yaani kila unaloliwaza kuna asilimia 70 kuwa ni ndoto uotayo ya alinacha.

Kipara sio shida. Shida ni pale huna mbele wala nyuma. Nyie ni mateso bila chuki. Hujui tawi gani ushike.
Yaani Upara na mvi vinakukuta ni Jobless mamaaaa! Hujui ufanye nini unafikiri Daah!

Unakipara chako kinamea polepole, au unamvi zako alafu huna pesa mbona lazima uwe introvert tuu. Yaani ndio ile unajikita mkimya maana nini sasa utaongea. Na hawa vijana wa 2000 hawana salia mtume, hawajui la muhazini wala mnadi Swala. Watakuona Babu yao ilhali hata miaka 40 huijui.
Utani utani wa kijinga na maneno ya kukutania vitazidi kushamiri.
Automatically kijiweni utaanza kupotea na utakuwa mtu wa kuwa bize for nothing.

Usiombe hiyo hali ikukute mazee! Kwanza hata ukienda vibaruani lazima uzinguliwe na matajiri kwa sababu wanajua huna chaguo, alafu mbaya zaidi lazima wakuzungushe kwenye malipo. Alafu ukijaribu kuwa mshari wanakuambia hayo mambo waachiw vijana ilhali wewe mwenyewe ndio kwanza upo miaka 35. Kudadadeki! Innalilah wainalilah Rajuun!

Chochote ukitaka kukifanya ukiwa kipara au mvi tena kwa mtaji mdogo lazima kikutie unyonge, Watu watakuwa wanakuona kama Budah fulani hivi.

Napendekeza, ukiwa below miaka 30 na umetoka familia maskini, kisha bado hauna ramani kivile.
Miaka 20- 30 ndio umri wako wa kujaribu kufanya kazi zózote na kujiweka sawa. Ndio umri wa kutafuta Pisikali moja uzae nayo yaani uanzishe familia ukiwa bado unamuonekano mzuri.

Usibeti kuwa ngoja utafute pesa Kwanza, huko ni kubet Ndugu yangu. Unaweza ukapata pesa au usipate. Lakini kwa umri wa miaka 20-30 huwezi kukosa Mwanamke mzuri wa kuanza naye familia akuzalie watoto angalàu mmoja au wawili.

Ili hata mambo yakibuma na mkeo akakuzingua uwe unafaida ya mtoto au watoto.
Lakini umechelewa kuanzisha familia kwa kubet kuwa unatafuta pesa Kwanza. Alafu umri umesogea, kipara na mvi zile alafu pesa hujapata. Ndugu yangu umekwisha!

This is Africa. Kanuni za huku ni za kipekee. Fanya kile ambacho unauhakika nacho kwa sasa na sio kubet kuwa unatafuta pesa kwanza kama vile uko Ulaya.

Elewa, huku Afrika unaweza ukawa na Juhudi, bidii na akili lakini bado maisha yakakupasua tuu. Lakini kwa Ulaya hilo haliwezekani.
Usijidanganye hapo na vishughuli vyako vya kujitafutia ambavyo vinakuingizia mia mbili mia tatu na kujipa moyo kuwa mambo yakikaa vizuri ndio utaanzisha familia. My friend, unajidanganya. Kwa Afrika labda uwe umeajiriwa tena serikalini ndio unaweza kufikiri kwa namna hiyo.

Biashara inabadilika muda wowote. Ni bora ibadilike ulishapata watoto tena na mke mzuri ambaye hata mkiachana haitalalia upande wako.

Uzee unatísha wazee! Uzee ambao haujajipata sio pouwa ndugu zanguni. Wanaosema Fainali uzeeni wanajua wanasema nini ndugu zanguni.

Tuombe Mungu atupe akili ya kutumia baraka zake lakini pia atupe uwezo wa kufanya mambo kwa wakati ili tusijetaabika.

Mwenye mvi nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
mie nilanza kuota mvi nyingi nikiwa mwaka wa3 chuo na hazikua zinaonekana vizuri nilipomaliza na hivyo nilionekana bado mdogo nikashindwa kuaminiwa na wananchi nikapigwa chini...
Awamu ilofata mvi zilikua zimekomaa vizur kuanzia kidevuni na kushoto na kulia mwa kichwa...

Mvi zimenisaidia sana mpaka apa nilipo kwakweli ...

saivi nazipenda nahisi zinanipendeza pia nikijichek halafu,

ila kaupara kanawasha hatar 🐒
 
Uwezo wa kung'amua mazingira yako ni muhimu sana kutiliwa mkazo katika malezi ya watoto. Unakuta mtu yeye ndio first generation educated kwenye ukoo na uzao wa kwanza kuishi mjini... Anajilinganisha kimafanikio na watu ambao Babu zao walizaliwa mijini, na biashara aliamza Babu yake Babu.... Kujitafutia stress tuu
Safi sana umeelewa nilikua namaanisha nini.
 
Back
Top Bottom